Kenya: Ajali ya Basi linalomilikiwa na kampuni ya Western Express yaua watu 50

Ajali: Watu zaidi ya 50 wafariki katika ajali ya basi Kenya wakielekea Kisumu

_103782835_89e8c5f6-cff3-4fec-a270-84341e9dfbaf.jpg
Haki miliki ya pichaAFP

Watu 50 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi-Kisumu.
Walioshuhudia wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea leo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.
Vyombo vya Habari nchini Kenya vinaripoti Kuwa ajali hiyo mbaya ilitokea katika eneo la Fort Ternan Kaunti ya Kericho.

Kwa mjibu wa kamanda wa polisi Kaunti ya Kericho, James Mogera, basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 67, lilitoka barabarani baada ya dereva kushindwa kulimudu kisha kugonga vizuizi vilivyokuwa kando ya barabara na kubiringia mita 20 kwenye bonde.
Kwa mjibu wa Gazeti la Daily Nation, miongoni waliofariki ni watoto wanane wa chini ya umri wa miaka mitano.
Awali idadi ya waliofarini ilikuwa 40 lakini polisi walielezae hofu yao juu ya vifo kuongezeka kutokana na hali ya baadhi ya majeruhi kuwa mbaya.
"Bahati mbaya sana tumepoteza watu 51," Mkuu wa Polisi Kenya Joseph Boinnet ameiambia redio ya Capital FM.
_103792102_9ea9585a-c6b8-406d-aadd-e73edffb05df.jpg
Haki miliki ya pichaAFPImage captionPaa la gari hiyo lilifumuka baada ya kupinduka na kubiringia mara kadhaa.

Shuhuda mmoja anasema alisikia honi, ikifuatwa na mlio mkubwa wa breki, kisha akawasikia abiria wakipiga kelele.
Baadhi ya majeruhi wanatibiwa katika Zahanati ya Fort Ternan, huku wengine wakikimbizwa hadi kwenye Hospitali ya Kaunti mjini Muhoroni kwa matibabu.
Taarifa zaidi zinasema miili ya baadhi ya watu waliofariki ingali imekwama ndani ya mabaki ya basi hilo.
Source: BBCswahili
 
Hii dunia tunapita...
Ya duniani tumeyakuta lazima tuyaache.

Mungu akawe faraja kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu pamoja na kwa wakenya kwa ujumla.
AMINA.
 
Nimeona hii habari Aljazeera ila wao walisema basi lilikuwa linaenda Kakamega.

Poleni sana majirani
 
Yaani 50 wamededi na wengine wako hospitali... hili basi linabeba abiria wangapi?

Mungu awarehemu marehemu na awape wepesi majeruhi..

Mzee baba asituangushe kwenye rambi rambi
 
My deepest and heartfelt condolences go to all those who have lost loved one’s and have been affected by this awfull tragedy. Those lost will always be remembered. R.I.P
 
Yaani 50 wamededi na wengine wako hospitali... hili basi linabeba abiria wangapi?

Mungu awarehemu marehemu na awape wepesi majeruhi..

Mzee baba asituangushe kwenye rambi rambi
Wame andika kuwa, basi hilo uwezo wake ni abiria 67
 
Back
Top Bottom