KENYA: Askofu asilimu na wafuasi wake, ageuza kanisa lake kuwa msikiti

Askofu asilimu Kenya na wafuasi wake, ageuza kanisa lake kuwa msikiti
Askofu mmoja nchini Kenya amesilimu akiwa na wafuasi wake na kulibadilisha kanisa lake kuwa msikiti.
Kwa mujibu Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), Askofu Charles Okwany ambaye baada ya kuichagua dini ya Kiislamu kuwa mwongozo wake wa wokovu duniani na Akhera amechagua jina la Ismail Okwany. Amesema amesilimu baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu Uislamu. Amesema baada ya kusilimu, kanisa alilokuwa akihurbiri, lililoko katika eneo la Nyalgosi kaunti ya Homa Bay magharibi mwa Kenya, ambalo lilijulikana kwa jina la God’s Call Church of East Africa sasa limegeuzwa jina na kuwa Msikiti wa Jamia wa Nyalgosi.
Katika mahojiano na Jarida la Nairobian, Ismail Okwany amesema, wakati alipokuwa muhubiri wa Kikristo alikuwa akisafiri katika miji mbalimbali ya Kenya na Tanzania hasa katika maeneo ya pwani na alipata fursa ya kufanya utafiti kuhusu maisha ya Waislamu. Ismail Okwany anaongeza kuwa aliweza kulinganisha Uislamu na Ukristo na akaamua kufuatia Uislamu.
Aidha anasema moja ya mambo yaliyokuwa yakimkera sana wakati akiwa muhubiri wa Ukristo ni tabia ya wanawake kuingia ndani ya kanisa wakiwa wamevaa sketi fupi katika hali ambayo wanawake Waislamu wanakuwa wamejisitiri kwa Hijabu wakati wa ibada msikitini na hata nje ya msikiti. Okwany mwenye umri wa miaka 65 alisilimu tarehe 26 Septemba akiwa na wafuasi wengine 23 wa kanisa lake na sasa wako mbioni kusajili rasmi kuwa msikiti
Source;parstoday
 
Aisee! Kisa cha kuhamia kwenye huo ushetani ni nini? hebu tujuze mkuu
...mmmh labda ndio katoka kwenye ushetani babu kubwa. Binafsi ni Catholic but naomba nikuambie waislamu wana mengi mazuri sana hasa kwenye mambo ya kijamii kama misiba (tunafukia fasta slogan), ndoa (haina kuumizana kichwa....na hufungwi na mke mmoja kama ndugu zangu....with 100 side chicks huku wanajifanya wana ndoa). Tuwe tunabalance comments.
 
kakutanana na mwanamke muislamu akasepa speed 360.
 
Ameona kanisa halina sadaka na michango mingi,huenda ana waumini wachache na ameona fursa ya yeye kuwa muislamu na kuongoza msikiti itamlipa.
Hakuna kingine zaidi ya kuona fursa!! Labda kuna mfadhili wa kujenga msikiti yupo,ndio maana kaona isiwe tabu!!
 
Nyie huwa mna matatizo mtu kaamua kusilimu ni haki yake kabisa ila angekuwa ni sheikh kawa mkristo angeisoma namba
 

Kulichokuvutia hapo nahisi ni kuoa wake wengi
Samahani lakini
 
Kwa maelezo yake n kwmb uislamu n dini ya Duniani na Ukristo ni din ya Mbinguni
 
Kulichokuvutia hapo nahisi ni kuoa wake wengi
Samahani lakini
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€...wala usijali na hujakosea....nilichotaka kusema Ukristu una unafiki kiaina wakati tunazini nje kinoma (sisemi kuoa mke zaidi ya mmoja huwezi zini..la hasha yapunguza matamanio kwetu wanaume)...haya mfano Father haoi....mind you ni active man huyo....nk. Waislamu kama umegundua sio watu wa show kama ndugu zangu...kuna mambo tunafanya wakristu kujiboost tu huku hatuna future....mfano budget ya harusi TZS 50m say...halafu labda hata kiwanja maharusi hawana. Hiyo ni budget ya simulizi za "after wedding"..."harusi ilinoga...ooh nilikunywa bia nyingi zijapata kuona...wamefunika nk". Ndoa ni ya wawili...kutafuta sifa kwa jamii ni kama kutafuta mikosi at times....kuna watu wanalala njaa eti nyie mwa-tie knot for TZS 50m budget kwa pombe na keki...na picha lukuki...............mbaya zaidi after 6 months mnapigana chini.
 
Naona upo Kidunia zaid
 
Hii habari imenikumbusha mwaka 2014 wakati nasilimu katika dini ya haki na nikaachana kabisa na Upadri na Ukatoliki.
Al islam huadin ullaydhi baa Saallahu biyh
Kumbe ustadhi mcharo nawe umetoka huko!!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…