KENYA: Askofu asilimu na wafuasi wake, ageuza kanisa lake kuwa msikiti

KENYA: Askofu asilimu na wafuasi wake, ageuza kanisa lake kuwa msikiti

ASKOFU ASILIMU KENYA NA WAFUASI WAKE, AGEUZA KANISA LAKE KUWA MSIKITI

Habari zilizotufikia kutoka Kenya, Askofu Charles Okwany ambaye baada ya kuichagua dini ya Kiislamu kuwa mwongozo wake wa wokovu duniani na Akhera amechagua jina la Ismail Okwany.

Amesema amesilimu baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu Uislamu. Amesema baada ya kusilimu, kanisa alilokuwa akihurbiri, lililoko katika eneo la Nyalgosi kaunti ya Homa Bay magharibi mwak Kenya, ambalo lilijulikana kwa jina la God’s Call Church of East Africa sasa limegeuzwa jina na kuwa Msikiti wa Jamia wa Nyalgosi.

Katika mahojiano na Jarida la Nairobian, Ismail Okwany amesema, wakati alipokuwa muhubiri wa Kikristo alikuwa akisafiri katika miji mbali mbali ya Kenya na Tanzania hasa katika maeneo ya pwani na alipata fursa ya kufanya utafiti kuhusu maisha ya Waislamu. Ismail Okwany anaongeza kuwa aliweza kulinganisha Uislamu na Ukristo na akaamua kufuatia Uislamu.

Aidha anasema moja ya mambo yaliyokuwa yakimkera sana wakati akiwa muhubiri wa Ukristo ni tabia ya wanawake kuingia ndani ya kanisa wakiwa wamevaa sketi fupi katika hali ambayo wanawake Waislamu wanakuwa wamejisitiri kwa Hijabu wakati wa ibada msikitini na hata nje ya msikiti.

Okwany mwenye umri wa miaka 65 alisilimu tarehe 26 Septemba akiwa na wafuasi wengine 23 wa kanisa lake na sasa wako mbioni kusajili rasmi msikiti wao.

Anasema Allaah (Subhanahu wa Ta’ala):

“Nyinyi ndio Ummah bora kuliko Ummah zote zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni) mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamuamini Allaah.” Aal ‘Imraan: 110

“Sema hii ndio njia yangu, ninaita (ninalingania) kwa Allaah kwa ujuzi wa kweli, mimi (nafanya hivi) na (kila) wanaonifuata. Na Allaah Ametakasika na kila upungufu, wala mimi simo miongoni mwa wanaomshirikisha (Allaah).” Yuusuf: 108

UNGANA NASI :

Kwa matukio na uchambuzi wa habari mbalimbali za kiislam ulimwenguni usikose kutembelea account yetu ya facebook ya Habari Za Kiislamu na pia jiunge na group letu la facebook la Uislamu Sahihi ni Qur'an na Sunnah.

Wabillahi at-Tawfiyq
Eti..!!?Askofu wa Church of East Africa? alafu ana waumini 23!! ? Africa will remain the continent full of adventures.
 
Najaribu kuwaza kwa sauti kama shekhe angesilimu na kubadiri msikiti kuwa kanisa ingekuwa vp
 
Nguo fupi za wanawake,wakiwa kanisani!! Yaani hiki ndio kilichomkera akahamia upande wa pili!!
Kuna sababu zingine za kimafundisho au ni hii moja?,
Yaani kwa upande wangu,uende Buddha,uhindu,yote ni yaleyale,
Wengi hizi kwenye hizi imani,tumejikuta,kwa sababu wazazi wetu tuliwakuta humo,nasi tunaamini imani ya wazazi wetu,
Imani hizi,zilikuwepo miaka mingi kabla ya uwepo wetu,no proof kwamba hipi ni sahihi
Waumini wenyewe anao 23 ameshindwa kuwacontrol
 
Ila Hawa waislamu wanajitahidi ,ukiwatizama wanaonekana kweli wanakijua wanachofanya.ila sie wakristu ni kama dini yetu inamashaka hivi.kila kukicha wanaibuka manabii na watumishi wanaopingana.huwa nakasirika kuona mwanamke kaposti picha yake kavaa sket fupi na maziwa nje alafu anaandika yesu kanifanya ning'are.
Imani yetu si kwenye mavazi
Kumwabudu katika roho na kweli
Ijue kweli nayo kweli itakuweka huru
 
Uyo jamaa angalau kapata muelekeo kwa sababu alianzisha dhehebu lake likamshinda. Natumai amefika kweny destiny yake, isije tokea akaanzisha dhehebu jingine trip hii la kiislamu.
 
Huyo hakukuwa askofu ,alikuwa mbwa mwitu kavalia ngozi ya kondoo na hatimaye amejitokeza wazi ,alioyatenda hayo yaliandikwa kwenye kitabu kitukufu cha mungu Bibilia , Amemkana Yesu hadharani lakini siku inakuja ambapo Yesu pia atamkana mbele ya Babake .laiti asingalijuwa Yesu ,Ameipoteza nafsi yake kwa tamaa za ulimwengu.
 
Miaka 65? Nina wasiwasi ametishiwa jambo. Serikali ya Kenya imfuatilie.
 
Soma andiko langu usinijibu tu utakavyo. Ati uislam ni dini inayoenezwa kwa maneno!! Umesoma kitabu gani wewe? Tunasikiaga wahubiri wa injili hatujasikia wahubiri wa kiislam bali mihadhara. Mihadhara kazi yake ni kuueneza uislam kwa nguvu na hao wakiwakataa muwaue haswa kwa kuchinja. Sasa hayo ndo maneno? Akheri rushwa kuliko mauti. Unayaona wanayofanya hao Al shabab kule Kenya? Huko ni kuueneza uislam kwa amani/maneno au?
ebana hiyo ndo maana ya muhadhara??[emoji3] [emoji13] mpk huku jf kuna vilaza sikuiz
 
Nadhani hiyo ya kuongeza kwa kuwazalisha wanawake ndicho kimempelekea huyu askofu kusilimu. Awawahi hao wanawake 32 aliokuwa nao awazalishe kihalali kwa sababu ya ruksa ya dini yake mpya. Kule alikokuwa si wanamwambia mume mmoja na mke mmoja?? Aksante kwa kutufungua macho
wake 32 ni wap huko mzee?
 
ASKOFU ASILIMU KENYA NA WAFUASI WAKE, AGEUZA KANISA LAKE KUWA MSIKITI

Habari zilizotufikia kutoka Kenya, Askofu Charles Okwany ambaye baada ya kuichagua dini ya Kiislamu kuwa mwongozo wake wa wokovu duniani na Akhera amechagua jina la Ismail Okwany.

Amesema amesilimu baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu Uislamu. Amesema baada ya kusilimu, kanisa alilokuwa akihurbiri, lililoko katika eneo la Nyalgosi kaunti ya Homa Bay magharibi mwak Kenya, ambalo lilijulikana kwa jina la God’s Call Church of East Africa sasa limegeuzwa jina na kuwa Msikiti wa Jamia wa Nyalgosi.

Katika mahojiano na Jarida la Nairobian, Ismail Okwany amesema, wakati alipokuwa muhubiri wa Kikristo alikuwa akisafiri katika miji mbali mbali ya Kenya na Tanzania hasa katika maeneo ya pwani na alipata fursa ya kufanya utafiti kuhusu maisha ya Waislamu. Ismail Okwany anaongeza kuwa aliweza kulinganisha Uislamu na Ukristo na akaamua kufuatia Uislamu.

Aidha anasema moja ya mambo yaliyokuwa yakimkera sana wakati akiwa muhubiri wa Ukristo ni tabia ya wanawake kuingia ndani ya kanisa wakiwa wamevaa sketi fupi katika hali ambayo wanawake Waislamu wanakuwa wamejisitiri kwa Hijabu wakati wa ibada msikitini na hata nje ya msikiti.

Okwany mwenye umri wa miaka 65 alisilimu tarehe 26 Septemba akiwa na wafuasi wengine 23 wa kanisa lake na sasa wako mbioni kusajili rasmi msikiti wao.

Anasema Allaah (Subhanahu wa Ta’ala):

“Nyinyi ndio Ummah bora kuliko Ummah zote zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni) mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamuamini Allaah.” Aal ‘Imraan: 110

“Sema hii ndio njia yangu, ninaita (ninalingania) kwa Allaah kwa ujuzi wa kweli, mimi (nafanya hivi) na (kila) wanaonifuata. Na Allaah Ametakasika na kila upungufu, wala mimi simo miongoni mwa wanaomshirikisha (Allaah).” Yuusuf: 108

UNGANA NASI :

Kwa matukio na uchambuzi wa habari mbalimbali za kiislam ulimwenguni usikose kutembelea account yetu ya facebook ya Habari Za Kiislamu na pia jiunge na group letu la facebook la Uislamu Sahihi ni Qur'an na Sunnah.

Wabillahi at-Tawfiyq
Akapimwe mkojo
 
Uyo jamaa angalau kapata muelekeo kwa sababu alianzisha dhehebu lake likamshinda. Natumai amefika kweny destiny yake, isije tokea akaanzisha dhehebu jingine trip hii la kiislamu.
afu aone cha mtemakuni..hakunaga upuuz huku
 
Mkristo anaye mwacha Yesu Kristo na kwenda nje.
Huyo hakuwahi kumwelewa Kristo wala hakuwahi kuwa
Mkristo bali alikuwa Mkristo jina.
Kubadili imani ni siyo kosa la jinai mtu ana uhuru wa kuamini na kufuata imani yoyote ile.
Ila kwa wale wanayoifuata imani inayotokana na Kulitii Neno la Kristo Yesu kamwe hawawezi kuiacha imani hiyo takatifu.
Kwakuwa Roho Mtakatifu anawasaidia kuwaimarisha kiimani kila siku.
Bila kuwa na Roho Mtakatifu ambaye ndiye Msaidizi wetu wa Imani huwezi kumwelewa Yesu Kristo.
Mwisho wake unaamua kutangatanga kiimani, mara leo ni Mbudha, kesho unahamia kuwa Mbahaullah, keshokutwa Mrastafariani, mtondogoo Mhindu mwisho wa siku unaingia Freemasonry.
Kwani mkristo ana sifa gani? ni zipi sifa za kuwa mkristo na si mkristo jina?
 
Back
Top Bottom