Kitu kinachowashinda wakristo,ni kutofahamu kama waislamu hawamuabudu Mtume Muhammad,mtume Muhammad katika uislamu,ni mfikishaji tu,ya kile alichotumwa na Mungu,kukifikisha kwetu wanadamu,na ndio hivyo kwa mitume mingine kama Yesu,Musa,Ibrahim,Ishaka,Yaakubu,Yohana nk,hawa wote pamoja na huyo Yesu unayamuamini wewe tunawaombea rehema na amani,mbele za Mungu,wakati wakitajwa majina yao.Kwa hiyo kwanza ujuwe:
1:Waislamu hawamuabudu Mtume Muhammad,wanamuabudu Mungu(hakuna haja ya kutwajwa Mungu Wa kweli ,wala Mungu wa haki,kwasababu anazo sifa hizo,bila kuwa na umuhimu wa kuzitaja).
2.Yesu,pamoja na mitume mingine tunawaombea rehema na amani.
Kwa hiyo uelewe,hata Yesu,katika uislamu anaombewa rehema na amani,kwasababu yeye pia ni mtume ndani ya uislamu.