Alex Mbwilo
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 351
- 290
Nimefuatilia siasa za Kenya toka wameanza kampeni za kupata viongozi katika 2017, kwa hakika hawa jamaa ukiondoa kitendo kimoja kibaya cha kuuawa kwa mfanyakazi wa tume ya uchaguzi nimewakubali wakenya.Hawa jamaa wanashindana kwa hoja. na mtazamaji ukiwasikiliza wagombea unawatofautisha bila shida yoyote. Kwamba unajua yupi anatete na yupi anataka kuingia.
Hapa kwetu huwa lazima ufanye kazi ya ziada ili ujue yupi anatetea na yupi anataka kuingia, na hii inachagizwa na kila mmoja kusema "nita". Katika kampeni za Kenya Uhuru anasema "nime" na hata wale wa ngazi za chini waliokuwepo madarakani wanasema "nime" wanaotaka madaraka wanasema "nita". Kitu kingine sijaona upande fulani kutumia dola kuhujumu upande mwingine na hata kulipo tokea rabsha za kuzomeana kwa kulipa kisasi walipogundua shida inayo wanyemelea viongozi wote walilizima hilo, jambo ambalo ni tofauti na nchi nyingine za Africa pale ambapo aliyekuwepo madarakani akiona anazidiwa hutumia dola kuhujumu upande shindani. Hii ni sawa na pale watu wawili wanapigana ngumi mmoja akiona anazidiwa anakimbilia kuchukua panga kwa matumizi dhidi ya mgomvi wake.
Siku Kenya wakiondoa jinamizi la ukabila wataziacha mbali nchi nyingi za Afrika kisiasa lakini pia kiuchumi.Uhuru ni mwanasiasa wa kweli pamoja na ushindani mkubwa kutoka kwa Raila huoni dhahiri kutumia dola na unamuona anaminyana kweli kweli arudi ofisini ingawa Raila amekomaa naye anataka kuingia ofisini.
Kenya wakirekebisha hizo kasoro kiduchu hatuwakuti, nawaombea wamalize kampeni kesho kutwa na wachaguane salama na waendelee na maisha. matokeo yasiwagombanishe na kwa mwelekeo kura zikipigwa, hesabiwa na kutangazwa washindi katika hali uhuru na haki wakenya watatoka wakiwa imara sana safari hii.TUWAOMBEEE