Kenya bado kidogo itakuwa nchi ya mfano kwa demokrasia katika Afrika

Kenya bado kidogo itakuwa nchi ya mfano kwa demokrasia katika Afrika

Democracy ni njia moja wapo iliyoletwa na wazungu ili waweze kutawala nchi za Africa. Kwa huu ujanja unaofanywa na Jubilee na IEBC hakuna kitu hapo. Kenya hadi chokoraa wa miaka 12 atapiga kura.
Sisi kama CCM tutatawala milele kama chama cha China. Chupa ilele ila mvinyo tofauti. Kwa hiyo kuweni wapole kwani ndokwanza tunavuta shuka.
IMG_20170803_121406.jpg
IMG_20170803_115846.jpg
IMG_20170802_183529.jpg
IMG_20170802_183515.jpg
 
Mh! Kweli inavyoenda kwa majirani zetu, nahofia watacharangana mapanga kupita kiasi katika kugombea kutinga Ikulu. Mauaji yaliyotokea hivi karibuni si dalili nzuri hata kidogo.
 
Kenya wako na Independent candidate ambao Tz hakuna licha ya marehemu Mch Mtikila kushinda kesi mahakamani. - -- Kenya wana Tume huru ya Uchaguzi, uundwaji wa tume upo huru. Haichaguliwi na Rais.
Matokeo ya chaguzi zote hutangazwa kituo cha kupiga kura. Tume hufanya majumuisho tu, pia vyombo vya habari vinaruhusiwa kufanya majumuisho.
Matokeo ya Uraisi na mengine yote yanahojiwa mahakamani.
Kenya ina mahakama iliyo huru kwasababu ya mchakato wa kuunda mahakama upo huru.
Wakuu wa mikoa {governers), na wilaya huchaguliwa na wananchi.
Kenya kuna mabunge mawili kama zilivyo nchi nyingi zenye ustawi.
Wabunge wanafanya kazi zao za kibunge za kusimamia serikali, hawaingizwi serikalini yaani kufanywa mawaziri.
Serikali kwa maana ya mawaziri hawatokani na wabunge na waziri akiteuliwa ni lazima apate confirmation ya bunge.
Raisi hana madaraka ya kifalme.
Wabunge wa viti maalum vya wananawake huchaguliwa na wananchi.
Na mambo mengi, hayo ni machache tu ya kujifunza.
Nimepata kitu hapa.Hongeren Kenya.
 
Ndo katiba yetu waliyoizika Lumumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefuatilia siasa za Kenya toka wameanza kampeni za kupata viongozi katika 2017, kwa hakika hawa jamaa ukiondoa kitendo kimoja kibaya cha kuuawa kwa mfanyakazi wa tume ya uchaguzi nimewakubali wakenya.Hawa jamaa wanashindana kwa hoja. na mtazamaji ukiwasikiliza wagombea unawatofautisha bila shida yoyote. Kwamba unajua yupi anatete na yupi anataka kuingia.

Hapa kwetu huwa lazima ufanye kazi ya ziada ili ujue yupi anatetea na yupi anataka kuingia, na hii inachagizwa na kila mmoja kusema "nita". Katika kampeni za Kenya Uhuru anasema "nime" na hata wale wa ngazi za chini waliokuwepo madarakani wanasema "nime" wanaotaka madaraka wanasema "nita". Kitu kingine sijaona upande fulani kutumia dola kuhujumu upande mwingine na hata kulipo tokea rabsha za kuzomeana kwa kulipa kisasi walipogundua shida inayo wanyemelea viongozi wote walilizima hilo, jambo ambalo ni tofauti na nchi nyingine za Africa pale ambapo aliyekuwepo madarakani akiona anazidiwa hutumia dola kuhujumu upande shindani. Hii ni sawa na pale watu wawili wanapigana ngumi mmoja akiona anazidiwa anakimbilia kuchukua panga kwa matumizi dhidi ya mgomvi wake.

Siku Kenya wakiondoa jinamizi la ukabila wataziacha mbali nchi nyingi za Afrika kisiasa lakini pia kiuchumi.Uhuru ni mwanasiasa wa kweli pamoja na ushindani mkubwa kutoka kwa Raila huoni dhahiri kutumia dola na unamuona anaminyana kweli kweli arudi ofisini ingawa Raila amekomaa naye anataka kuingia ofisini.

Kenya wakirekebisha hizo kasoro kiduchu hatuwakuti, nawaombea wamalize kampeni kesho kutwa na wachaguane salama na waendelee na maisha. matokeo yasiwagombanishe na kwa mwelekeo kura zikipigwa, hesabiwa na kutangazwa washindi katika hali uhuru na haki wakenya watatoka wakiwa imara sana safari hii.TUWAOMBEEE
Lazima iwe hivyo vinginevyo wakumbane na mkono wa The Hague!
Pili, ukitaka kujua kwamba hawa jamaa bado sana kufikia huko unakozungumzia nenda uone maduka yalivyofungwa katika msimu huu wa kura. Aidha unatakiwa siku ya uchaguzi uje utuambie kama baada ya kupiga kura watu wataendelea na shughuli zao hususan sehemu za biashara ili kupima ukomavu wa kidemokrasia unaouzungumzia!
 
Mh! Kweli inavyoenda kwa majirani zetu, nahofia watacharangana mapanga kupita kiasi katika kugombea kutinga Ikulu. Mauaji yaliyotokea hivi karibuni si dalili nzuri hata kidogo.

Mkuu, demokrasia hasa huku kwetu Africa ni safari ndefu, sisi bado tunakabiliana na changamoto nyingi sana kwa kuwa bado tunangangana kufika, naamini bado hatujapoteza dira na tuko on the right track. ukiangalia tulipotoka, na watu wote tuliopoteza tukipigania multipartism na katiba labda utatuelewa. Wakenya hatupendi kuburuzwa na kama hatujafurahia matokeo lazima tutaandamana hadi haki itendeke.

Uchaguzi huu umeonyesha nguvu ya judiciary ambapo imeamua na kuondoa vikwazo vingi ambavyo vingezuia uchaguzi wa kweli na haki, decisions zingine raisi Uhuru hakufurahia lakini independence ya institution ilimlazimu kukubali tu.

Saa hizi kuna movement inayoitwa [HASHTAG]#fagiawote[/HASHTAG] , mostly ita affect sitting mps, governors, MCA and senators ambao wengi watashindwa ku retain position zao kwa kuwa wananchi wameshaonja utamu wa ugatuzi na wanajua what is expected of their leaders.

Safari ya democrasia ni ndefu, watu hupoteza maisha yao, watu hujeruhiwa vibaya lakini azma ya a better kenya lazima itimizwe. Inshallah 2022 utaona tofauti kubwa sana ya siasa na voting patterns and processes, we have learnt a lot since the 2007 elections, we continue to improve our political processes and eventually no one will have to die for politicians to take or retain power.

Nikimaliza, hakuna watu watakao pigana mapanga mwaka huu, it'll all run smoothly and we will serve as an example on how to conduct a credible, tightly contested election.

Ijumaa Karim.
 
Democracy ni njia moja wapo iliyoletwa na wazungu ili waweze kutawala nchi za Africa. Kwa huu ujanja unaofanywa na Jubilee na IEBC hakuna kitu hapo. Kenya hadi chokoraa wa miaka 12 atapiga kura.
Sisi kama CCM tutatawala milele kama chama cha China. Chupa ilele ila mvinyo tofauti. Kwa hiyo kuweni wapole kwani ndokwanza tunavuta shuka.View attachment 557664View attachment 557665 View attachment 557666View attachment 557667
[emoji1] [emoji2] [emoji3] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji2] [emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom