Kenya bado wana safari kuliko Tanzania, Kura zinapigwa kwa ushawishi wa ukabila

Acha uongo umejuaje yaani tuseme ww wakenya umewaweka kiganjani mwako?.
 
Acha uongo umejuaje yaani tuseme ww wakenya umewaweka kiganjani mwako?.

Ulishawahi kufika Kenya? Wakenya hata jina la Waziri Mkuu au hata Makamu wa raisi wa Tanzania hawalijui, wakati Mtanzania wa kawaida anajua majina ya karibia Viongozi wote Kenya, Samia mwenyewe hawakumjua mpaka alipokuwa raisi, hawakuwahi kumsikia na mpaka leo wengi hata jina lake hawalijui vizuri ukiondoa tu raisi aliyemrithi Magufuli ni Mwanamke, kwa maana Magufuli tu ndiyo anajulikana, …
 
Kwa kweli Magufuri hakuwa mtu mzuri angetawala zaidi ya pale na sisi Tanzania matabaka mengi yangezaliwa mfano ukabila,ukanda,ubinafsi,uchoyo,udini,uchama,na hata usalama ulikuwa hati hati.
 
Pascal Mayalla alianza kupandikiza mambo ya namna hii humu, kuna uzi wake mmoja ulikuwa na element za ukabila, akiwapalilia watu kutoka kanda yake sikuupenda abadani.

Tanzania tulivyo sasa tumechanganyika sana kwa kuoleana kwa makabila na hata imani na itikadi, hii notion ya watu wa kabila fulani ni .... siyo ya kuendekeza
 
Nyerere alitufundisha tukatae ukabila ili tukubali Ujamaa. Wakati Ujamaa ndiyo unaharibu nchi kuliko ukabila. Kihistoria Ujamaa na Ukomunisti umeuwa na kutesa mamilioni ya watu. Sisi tuna mfumo mbovu wa Ujamaa kulko hata huo ukabila wa Kenya.
 
Kweli kabisaaa,Magufuli ndio walikua wanamfatilia.hata tv zetu hawaangalii.
 
Bora hata ukabila wa Wakenya kuliko unafiki na ubaguzi wa kisiasa wa Watanzania.
Watu wanaikumbatia ccm na ccm inawarubuni huku ikiua matarajio yao ya leo na baadae!
Hivi uzalendo ni kuwa ccm? Na je kiongozi ni lazima awe wa ccm??
 
Nyerere alitufundisha tukatae ukabila ili tukubali Ujamaa. Wakati Ujamaa ndiyo unaharibu nchi kuliko ukabila. Kihistoria Ujamaa na Ukomunisti umeuwa na kutesa mamilioni ya watu. Sisi tuna mfumo mbovu wa Ujamaa kulko hata huo ukabila wa Kenya.
Badala ya ujamaa tukaambulia uchama na uchawa!
Hatuna malengo ya pamoja!
Hatumjui adui...
Tunajiangamiza wenyewe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…