Kenya bado wana safari kuliko Tanzania, Kura zinapigwa kwa ushawishi wa ukabila

Kenya bado wana safari kuliko Tanzania, Kura zinapigwa kwa ushawishi wa ukabila

Hakuna Mkenya anayejadili Uchaguzi wa Tanzania achilia mbali hata kujua majina ya Viongozi wa Tanzania ukiondoa Magufuli kwa nini wewe uko obsessed na Uchaguzi wao? Nchi nzima ya Tanzania imeganda kwenye TV tena za Kenya kufwatilia Uchaguzi wa Kenya hauoni kwamba tatizo liko zaidi kwako labda kuliko kwa Wakenya?

Hakuna Mkenya anayeweza kuangalia TV ya Tanzania akiwa Kenya achilia mbali hata kujua tu Jina la TV za TZ lkn Tanzania ni kawaida kuangalia TV za Kenya, sasa nani ana safari ndefu kuliko mwingine?
Acha uongo umejuaje yaani tuseme ww wakenya umewaweka kiganjani mwako?.
 
Acha uongo umejuaje yaani tuseme ww wakenya umewaweka kiganjani mwako?.

Ulishawahi kufika Kenya? Wakenya hata jina la Waziri Mkuu au hata Makamu wa raisi wa Tanzania hawalijui, wakati Mtanzania wa kawaida anajua majina ya karibia Viongozi wote Kenya, Samia mwenyewe hawakumjua mpaka alipokuwa raisi, hawakuwahi kumsikia na mpaka leo wengi hata jina lake hawalijui vizuri ukiondoa tu raisi aliyemrithi Magufuli ni Mwanamke, kwa maana Magufuli tu ndiyo anajulikana, …
 
Na Magufuli alikuwa anaipeleka nchi kwenye ukabila na amewachonganisha wasukuma na makabila mengine nchini mpk wakaanza kudhani wasukuma Ni watu wa hovyo hovyo.

Wasukuma ni watu poa sana tena sana na hawana shida na mtu, tabia za ajabu ajabu alikuwa nazo yule bwana wa Chato tu.
Kwa kweli Magufuri hakuwa mtu mzuri angetawala zaidi ya pale na sisi Tanzania matabaka mengi yangezaliwa mfano ukabila,ukanda,ubinafsi,uchoyo,udini,uchama,na hata usalama ulikuwa hati hati.
 
Mosi, Mkikuyu hawezi kumpigia kura mtu ambaye sio Mkikuyu Mwenzake, Ikitokea hakuna Mkikuyu anayegombea basi hata siku moja haitakuja tokea Mkikuyu kumpigia kura Mjaluo, Kwa Kenya ni mwiko Mkikuyu hata akikosa Mkikuyu Mwenzake kuchagua Mjaluo

Kuna ugomvi mkubwa kati ya wakikuyu na wajaluo, Wakikuyu ni kabila la kwanza kwa ukubwa Kenya na wajaluo ni kabila la nne kwa ukubwa Kenya, Wajaluo wanaamini wakikuyu wamehodhi njia zote za uchumi Nchini Kenya na kuyafanya maeneo ya wajaluo kuwa maskini sana hasa baadhi ya maeneo ya katikati ya
Pascal Mayalla alianza kupandikiza mambo ya namna hii humu, kuna uzi wake mmoja ulikuwa na element za ukabila, akiwapalilia watu kutoka kanda yake sikuupenda abadani.

Tanzania tulivyo sasa tumechanganyika sana kwa kuoleana kwa makabila na hata imani na itikadi, hii notion ya watu wa kabila fulani ni .... siyo ya kuendekeza
 
Nyerere alitufundisha tukatae ukabila ili tukubali Ujamaa. Wakati Ujamaa ndiyo unaharibu nchi kuliko ukabila. Kihistoria Ujamaa na Ukomunisti umeuwa na kutesa mamilioni ya watu. Sisi tuna mfumo mbovu wa Ujamaa kulko hata huo ukabila wa Kenya.
 
Hakuna Mkenya anayejadili Uchaguzi wa Tanzania achilia mbali hata kujua majina ya Viongozi wa Tanzania ukiondoa Magufuli kwa nini wewe uko obsessed na Uchaguzi wao? Nchi nzima ya Tanzania imeganda kwenye TV tena za Kenya kufwatilia Uchaguzi wa Kenya hauoni kwamba tatizo liko zaidi kwako labda kuliko kwa Wakenya?

Hakuna Mkenya anayeweza kuangalia TV ya Tanzania akiwa Kenya achilia mbali hata kujua tu Jina la TV za TZ lkn Tanzania ni kawaida kuangalia TV za Kenya, sasa nani ana safari ndefu kuliko mwingine?
Kweli kabisaaa,Magufuli ndio walikua wanamfatilia.hata tv zetu hawaangalii.
 
Bora hata ukabila wa Wakenya kuliko unafiki na ubaguzi wa kisiasa wa Watanzania.
Watu wanaikumbatia ccm na ccm inawarubuni huku ikiua matarajio yao ya leo na baadae!
Hivi uzalendo ni kuwa ccm? Na je kiongozi ni lazima awe wa ccm??
 
Nyerere alitufundisha tukatae ukabila ili tukubali Ujamaa. Wakati Ujamaa ndiyo unaharibu nchi kuliko ukabila. Kihistoria Ujamaa na Ukomunisti umeuwa na kutesa mamilioni ya watu. Sisi tuna mfumo mbovu wa Ujamaa kulko hata huo ukabila wa Kenya.
Badala ya ujamaa tukaambulia uchama na uchawa!
Hatuna malengo ya pamoja!
Hatumjui adui...
Tunajiangamiza wenyewe!!
 
Back
Top Bottom