Kenya bado wana safari kuliko Tanzania, Kura zinapigwa kwa ushawishi wa ukabila

Kenya bado wana safari kuliko Tanzania, Kura zinapigwa kwa ushawishi wa ukabila

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Safari yangu ya kukaa hapa Kenya inahitimishwa leo rasmi, kesho narejea Tanzania.

Wagombea wote wakubwa ndani ya Kenya wana tuhuma za ufisadi kwa Raila na Ruto. Hivyo ajenda ya ufisadi haikuwa ishu kubwa sana kwa wakenya walio wengi, bali ajenda kubwa ya wakenya wengi kwenye uchaguzi huu ilikuwa ni mageuzi ya kiuchumi.

Niliandika huu uzi Utofauti wa siasa za Dar es Salaam na Nairobi, Diamond Platinum amekiwasha hapa Kasarani
wakati tulipotembelea wagombea walipohitimisha kampeni zao. Mimi nilipangwa kuhudhuria mwenendo wa kampeni za Raila Odinga pale Kasarani hivyo habari za upande wa Ruto wanazo wenzangu waliongea na wafuasi wa Ruto.

Siku ya kupiga kura tulipotembelea vituo vya kupiga kura na kuongea na baadhi ya wazee wa makamo kuna mambo yalinishangaza kidogo.

Mosi, mkikuyu hawezi kumpigia kura mtu ambaye sio mkikuyu mwenzake. Ikitokea hakuna mkikuyu anayegombea basi hata siku moja haitakuja tokea mkikuyu kumpigia kura mjaluo. Kwa Kenya ni mwiko mkikuyu hata akikosa mkikuyu mwenzake kuchagua mjaluo.

Kuna ugomvi mkubwa kati ya wakikuyu na wajaluo, wakikuyu ni kabila la kwanza kwa ukubwa Kenya na wajaluo ni kabila la nne kwa ukubwa Kenya. Wajaluo wanaamini wakikuyu wamehodhi njia zote za uchumi nchini Kenya na kuyafanya maeneo ya wajaluo kuwa maskini sana hasa baadhi ya maeneo ya katikati ya mji.

Kwenye uchaguzi wa sasa wakenya wenye asili ya Kikuyu wamempigia kura William Ruto mkarenjini. Wakikuyu hawana shida na wakarenjini kiasili kwa mujibu wa wazee niliowahoji.

Pili, muungano wa vyama unaoanzishwa Kenya hauna lengo la kuwa muungano wa kiafya bali ni muungano unaolenga ukabila tu. Ni Muungano unaoangazia ni mtu wa kabila gani na ana watu wangapi wanaweza kuniunga mkono. Kinachoangaliwa unayeungana naye ana watu wa kabila gani na kiasi gani!

Tatu, uchaguzi unahitaji uwe na pesa za kutisha sana Kenya, mgombea hata wa nafasi ya chini bado inakuhitaji mamilioni ya pesa za Kenya kugombea uongozi. Hakika hao Ruto na Raila ni matajiri sana na sio watu wa mchezo mchezo. Kama watu wa chini na vijana tuliongea nao ni ngumu sana kupata fedha na nafasi za uongozi nchini Kenya bila pesa za kugawa. Kugawa pesa kwenye chaguzi Kenya sio hoja ya msingi.

Vyovyote itakavyokuwa mshindi atatangazwa, lakini Kenya ina ukabila mbaya ambao sijawahi kuushuhudia kwenye maisha yangu Tanzania.

Tunamshukuru Mwenyekiti wa Tume ya Uangalizi wa Afrika mashariki Jakaya Kikwete kwa kutuamini na kutuelekeza kilichotupeleka Kenya, riport ya maoni na nini cha kuboreshwa watakabidhiwa Tume ya IEBC.
 
Na Magufuli alikuwa anaipeleka nchi kwenye ukabila na amewachonganisha wasukuma na makabila mengine nchini mpk wakaanza kudhani wasukuma Ni watu wa hovyo hovyo.

Wasukuma ni watu poa sana tena sana na hawana shida na mtu, tabia za ajabu ajabu alikuwa nazo yule bwana wa Chato tu.
 
Hakuna Mkenya anayejadili Uchaguzi wa Tanzania achilia mbali hata kujua majina ya Viongozi wa Tanzania ukiondoa Magufuli kwa nini wewe uko obsessed na Uchaguzi wao? Nchi nzima ya Tanzania imeganda kwenye TV tena za Kenya kufwatilia Uchaguzi wa Kenya hauoni kwamba tatizo liko zaidi kwako labda kuliko kwa Wakenya?

Hakuna Mkenya anayeweza kuangalia TV ya Tanzania akiwa Kenya achilia mbali hata kujua tu Jina la TV za TZ lkn Tanzania ni kawaida kuangalia TV za Kenya, sasa nani ana safari ndefu kuliko mwingine?
 
Kwa kiasi upo sahihi lakini pia umepotosha, ukiangalia ODM kina nguvu Pwani, Kwa wasomali, Nyanza, Nairobi na Western kwa Waluhya je huko kote ni kwa Wajaluo?? So kwa Odinga ukabila haujawahi kumbeba.

Mfano Kiongozi wa Waluhya yaani Mudavadi alienda Kwa Ruto ila Bado Raila kabeba kura za Waluhya wote kwa zaidi ya 70%.

Kwa Ruto licha ya kwamba chama chake kipo kwa wakalenjin na Wakikuyu ila naye anataka kukijenga kitaifa tofauti na ilivyokua Jubilee au CCM ambavyo viliundwa kikabila tu ila kitaifa havikuwepo.

Kwa hapo Nairobi mgombea Ugavana Sakkajja anatoka kabila dogo sana huko Trans Nzoia ila mbona kamuangusha mkikuyu wa Azimio ilihali Nairobi ni ya Wakikuyu, wakamba na waluhya!?
 
Hata kikwete anakubali wametuzidi sana kwenye mfumo. Kuna tofauti ya wapiga kura na serikali na utaratibu. Kenya tatizo la ukabila ni la watu lakini tatizo letu ni demokrasia 😂 unachanganya vitu

Mfumo wa serikali wa Kenya ni mzuri na wa wazi kuliko wetu. Ukabila wa watu hauna uhusiano na mfumo wa nchi. Ni sawa na sehemu zenye ubaguzi wa rangi lakini bado wanaweza kuwa na mfumo mzuri wa serikali, bunge na mahakama.

Tumekuwa na utamaduni wa kutafuta uongo na mabaya badala ya kujitahidi tuwe na mfumo mzuri.

Unavyosema bado kwenye lipi? Serikali haiwezi pekee kutoa ukabila ni wananchi wenyewe ndiyo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele. Tatizo letu ni mfumo na ubinafsi maana sisi ni wabinafsi kuliko hao wakenya kwa mbali
Sana
 
Na Magufuli alikua anaipeleka nchi kwny ukabila na amewachonganisha wasukuma na makabila mengine nchini mpk wakaanza kudhani wasukuma Ni watu wa hovyo hovyo.

Wasukuma Ni watu poa sana tena Sana na hawana shida na mtu,tabia za ajabu ajabu alikua nazo yule bwn wa Chato tu.
Jinga tu. Hadi umseme vibaya magufuli. Magufuli na ukabila wapi na wapi. Chuki yenu ni kuwakomesha nyie fisadi wa umma.
 
Safari yangu ya kukaa hapa Kenya inahitimishwa Leo rasmi, Kesho narejea Tanzania

Wagombea wote wakubwa ndani ya Kenya wana tuhuma za ufisadi kwa Raila na Ruto, Hivyo ajenda ya ufisadi haikuwa ishu kubwa sana kwa wakenya walio wengi bali ajenda kubwa ya wakenya wengi kwenye uchaguzi huu ilikuwa Mageuzi ya kiuchumi

Niliandika huu uzi Utofauti wa siasa za Dar es Salaam na Nairobi, Diamond Platinum amekiwasha hapa Kasarani
wakati tulipotembelea wagombea walipohitimisha kampeni zao, Mimi nilipangwa kuhudhuria mwenendo wa kampeni za Raila Odinga pale kasarani hivyo habari za upande wa Ruto wanazo wenzangu waliongea na wafuasi wa Ruto

Siku ya kupiga kura tulipotembelea vituo vya kupiga kura na kuongea na baadhi ya wazee wa makamo kuna mambo yalinishangaza kidogo

Mosi, Mkikuyu hawezi kumpigia kura mtu ambaye sio Mkikuyu Mwenzake, Ikitokea hakuna Mkikuyu anayegombea basi hata siku moja haitakuja tokea Mkikuyu kumpigia kura Mjaluo, Kwa Kenya ni mwiko Mkikuyu hata akikosa Mkikuyu Mwenzake kuchagua Mjaluo

Kuna ugomvi mkubwa kati ya wakikuyu na wajaluo, Wakikuyu ni kabila la kwanza kwa ukubwa Kenya na wajaluo ni kabila la nne kwa ukubwa Kenya, Wajaluo wanaamini wakikuyu wamehodhi njia zote za uchumi Nchini Kenya na kuyafanya maeneo ya wajaluo kuwa maskini sana hasa baadhi ya maeneo ya katikati ya mji

Kwenye uchaguzi wa sasa wakenya wenye asili ya Kikuyu wamempigia kura William Ruto Mkarenjini, Wakikuyu hawana shida na wakarenjini kiasili kwa mujibu wa wazee niliowahoji

Pili, Miungano ya vyama inayoanzishwa Kenya haina lengo kuwa Miungano ya kiafya bali ni Miungano inayolenga ukabila tu, Ni Miungano inayoangaziwa ni mtu wa kabila gani na ana watu wangapi wanaweza kuniunga mkono. Kinachoangaliwa unayeungana naye ana watu wa kabila gani kiasi gani?

Tatu, Uchaguzi Unahitaji uwe na pesa za kutisha sana Kenya, Mgombea hata wa nafasi ya chini bado inakuhitaji mamilioni ya pesa za Kenya kugombea uongozi, Hakika hao Ruto na Raila ni matajiri sana na sio watu wa mchezo mchezo, Kama watu wa chini na vijana tuliongea nao ni ngumu sana kupata Fedha na nafasi za uongozi Nchini Kenya bila pesa za kugawa, Kugawa pesa kwenye chaguzi Kenya sio hoja ya msingi

Vyovyote itakavyokuwa mshindi atakaye tangazwa lakini Kenya ina ukabila mbaya ambao sijawahi kushuhudia kwenye maisha yangu Tanzania

Tunamshukuru mwenyekiti wa Tume ya uangalizi wa Afrika mashariki Jakaya Kikwete kwa kutuamini na kutuelekeza kilichotupeleka Kenya, Riport ya maoni na nini cha kuboreshwa watakabidhiwa Tume ya IEBC
Ukabila au mtu wa nyumbani iko Dunia nzima, unazani kule Marekani mfano Texas kwa nini ni Republican? Au tafutavkura alizo pata Obama jimbo alilo zaliwa.
 
Hakuna Mkenya anayejadili Uchaguzi wa Tanzania achilia mbali hata kujua majina ya Viongozi wa Tanzania ukiondoa Magufuli kwa nini wewe uko obsessed na Uchaguzi wao? Nchi nzima ya Tanzania imeganda kwenye TV tena za Kenya kufwatilia Uchaguzi wa Kenya hauoni kwamba tatizo liko zaidi kwako labda kuliko kwa Wakenya?

Hakuna Mkenya anayeweza kuangalia TV ya Tanzania akiwa Kenya achilia mbali hata kujua tu Jina la TV za TZ lkn Tanzania ni kawaida kuangalia TV za Kenya, sasa nani ana safari ndefu kuliko mwingine?
Kwa Nini hii iko hivi?
 
Na Magufuli alikua anaipeleka nchi kwny ukabila na amewachonganisha wasukuma na makabila mengine nchini mpk wakaanza kudhani wasukuma Ni watu wa hovyo hovyo.

Wasukuma Ni watu poa sana tena Sana na hawana shida na mtu,tabia za ajabu ajabu alikua nazo yule bwn wa Chato tu.
Acha uongo ndugu walioanzisha swala la ukabila na udini wanajijua na m nawajua wala usisingizie jiwe la watu mmeona mmeshindwa kutumia hyo propaganda mkageuza gia.
 
Ficha ujinga wako.
 
Acha uongo ndugu walioanzisha swala la ukabila na udini wanajijua na m nawajua wala usisingizie jiwe la watu mmeona mmeshindwa kutumia hyo propaganda mkageuza gia.
Mwanza: Hawa ndio walionipigia kura, msiwabomoleeeeeeeeee nyumba zao.

Kimara:Hao wabomoleeni tu,wamejenga kwny hifadhi za barabara

😄😄😄😄😄
 
Na Magufuli alikua anaipeleka nchi kwny ukabila na amewachonganisha wasukuma na makabila mengine nchini mpk wakaanza kudhani wasukuma Ni watu wa hovyo hovyo.

Wasukuma Ni watu poa sana tena Sana na hawana shida na mtu,tabia za ajabu ajabu alikua nazo yule bwn wa Chato tu.
Ko huyu mwamba hakuwa msukuma ila alitumia usukuma kutafuta popularity
 
Hakuna Mkenya anayejadili Uchaguzi wa Tanzania achilia mbali hata kujua majina ya Viongozi wa Tanzania ukiondoa Magufuli kwa nini wewe uko obsessed na Uchaguzi wao? Nchi nzima ya Tanzania imeganda kwenye TV tena za Kenya kufwatilia Uchaguzi wa Kenya hauoni kwamba tatizo liko zaidi kwako labda kuliko kwa Wakenya?

Hakuna Mkenya anayeweza kuangalia TV ya Tanzania akiwa Kenya achilia mbali hata kujua tu Jina la TV za TZ lkn Tanzania ni kawaida kuangalia TV za Kenya, sasa nani ana safari ndefu kuliko mwingine?
Kenya wanafuatilia sana chaguzi za Tanzania kuliko watanzania wanavyofuatilia chaguzi za Kenya. Nimekaa Kenya kipindi 2015.
 
Back
Top Bottom