GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Safari yangu ya kukaa hapa Kenya inahitimishwa leo rasmi, kesho narejea Tanzania.
Wagombea wote wakubwa ndani ya Kenya wana tuhuma za ufisadi kwa Raila na Ruto. Hivyo ajenda ya ufisadi haikuwa ishu kubwa sana kwa wakenya walio wengi, bali ajenda kubwa ya wakenya wengi kwenye uchaguzi huu ilikuwa ni mageuzi ya kiuchumi.
Niliandika huu uzi Utofauti wa siasa za Dar es Salaam na Nairobi, Diamond Platinum amekiwasha hapa Kasarani
wakati tulipotembelea wagombea walipohitimisha kampeni zao. Mimi nilipangwa kuhudhuria mwenendo wa kampeni za Raila Odinga pale Kasarani hivyo habari za upande wa Ruto wanazo wenzangu waliongea na wafuasi wa Ruto.
Siku ya kupiga kura tulipotembelea vituo vya kupiga kura na kuongea na baadhi ya wazee wa makamo kuna mambo yalinishangaza kidogo.
Mosi, mkikuyu hawezi kumpigia kura mtu ambaye sio mkikuyu mwenzake. Ikitokea hakuna mkikuyu anayegombea basi hata siku moja haitakuja tokea mkikuyu kumpigia kura mjaluo. Kwa Kenya ni mwiko mkikuyu hata akikosa mkikuyu mwenzake kuchagua mjaluo.
Kuna ugomvi mkubwa kati ya wakikuyu na wajaluo, wakikuyu ni kabila la kwanza kwa ukubwa Kenya na wajaluo ni kabila la nne kwa ukubwa Kenya. Wajaluo wanaamini wakikuyu wamehodhi njia zote za uchumi nchini Kenya na kuyafanya maeneo ya wajaluo kuwa maskini sana hasa baadhi ya maeneo ya katikati ya mji.
Kwenye uchaguzi wa sasa wakenya wenye asili ya Kikuyu wamempigia kura William Ruto mkarenjini. Wakikuyu hawana shida na wakarenjini kiasili kwa mujibu wa wazee niliowahoji.
Pili, muungano wa vyama unaoanzishwa Kenya hauna lengo la kuwa muungano wa kiafya bali ni muungano unaolenga ukabila tu. Ni Muungano unaoangazia ni mtu wa kabila gani na ana watu wangapi wanaweza kuniunga mkono. Kinachoangaliwa unayeungana naye ana watu wa kabila gani na kiasi gani!
Tatu, uchaguzi unahitaji uwe na pesa za kutisha sana Kenya, mgombea hata wa nafasi ya chini bado inakuhitaji mamilioni ya pesa za Kenya kugombea uongozi. Hakika hao Ruto na Raila ni matajiri sana na sio watu wa mchezo mchezo. Kama watu wa chini na vijana tuliongea nao ni ngumu sana kupata fedha na nafasi za uongozi nchini Kenya bila pesa za kugawa. Kugawa pesa kwenye chaguzi Kenya sio hoja ya msingi.
Vyovyote itakavyokuwa mshindi atatangazwa, lakini Kenya ina ukabila mbaya ambao sijawahi kuushuhudia kwenye maisha yangu Tanzania.
Tunamshukuru Mwenyekiti wa Tume ya Uangalizi wa Afrika mashariki Jakaya Kikwete kwa kutuamini na kutuelekeza kilichotupeleka Kenya, riport ya maoni na nini cha kuboreshwa watakabidhiwa Tume ya IEBC.