Japo natambua wajibu wa serikali ya Kenya kuilinda sekta ya utalii iliyokuwa kwenye tishio la utekaji nyara wa Watalii, lakini naamini serikali ya Kenya ilikurupuka kuingia vitani ata kabla ya kujaribu hatua zingine za kuhakikisha usalama huo.
Al-Shababy sio tishio kwa Kenya peke yake, ni tishio kwa nchi zote za Africa Mashariki, Africa na Ulimwengu wa Magharibi kwa ujumla, hivyo uamuzi wa Kenya kwenda vitani peke yake, na hivyo kubeba gharama zote za vita hivyo haukupaswa kufanyika wakati huu ambapo uchumi wa Kenya upo kwenye hali mbaya, wakati kenya inashuhudia mlipuko mkubwa wa bei ya bidhaa muhimu, wakati thamani ya pesa imeshuka sana, haukuwa wakati sahihi kuanzisha vita visivyo na mwisho dhidi ya Al-Shababy..
Walichopaswa kufanya kwa sasa ni kuongeza ulinzi wa mipaka yao, kuanzisha kampeni ya kuwasaka wafuasi wa al-shababy ndani ya Kenya, na kuongeza ushawishi wa kuongeza majeshi ya AU ya kuusaidia utawala wa Somalia, na kulinda usalama kwa ujumla.
Sasa wapo vitani ndani ya mipaka ya somalia kinyume cha katiba ya Kenya, vita vimetangazwa na Waziri badala ya Rais, Bunge halijahusisha kama katiba yao inavyoelekeza, wanapambana na jeshi lisilo na organization maalum,na wakati huohuo serikali inayotambulika ya Somalia inapinga uwepo wa Jeshi la Kenya ndani ya mipaka yao, nasharia kuwa pamoja na gharama kubwa ambazo Kenya itaingia, gharama kubwa zinazoweza kuwakumbumba viongozi wakuu wa Kenya kisiasa, gharama kubwa zaidi ya kiusalama ndani ya mipaka ya Kenya, siamini kama lengo lao litatimia, muda utaongea..