Askari Kanzu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 4,596
- 1,234
- Thread starter
-
- #1,401
Ok, now I think you start to understand who you are dealing with!haha...(am suspending rules of engagement but briefly) how does it feel to be on the receiving end, nkt!!...wats the nikune shit u trying to propose, DUDE!! tema hiyo mate, ua msemo sounds so gay. Rearrange ua thots and engage, i.e. if u got anything to do with combat, alshabaab or somalia. READ TITLE.
Nyie mmeenda vitani dhidi ya alshabab halafu mnaanza kufuata ushauri wa Uganda ina maana vita imewashinda sasa mnataka kubadili shughuli na kuanza kulinda amani chini ya majenerali wa Uganda. .
Wakati huo TFG ilibaki Baidoa tu lakini Ethiopia wakasambaratisha ICU ndani ya wiki mbili na kuiteka Mogadishu na mpaka leo hatujasikia tena kitu kinaitwa ICU pale somalia.
Sasa alshabab ikaibuka lakini sio kitisho kwa Ethiopia ila sasa ni kitisho kwa kenya maana wanawashambulia mpaka ndani ya nchi yenu, na nyie mmetangaza vita na alshabab cha ajabu mpaka sasa bado mnajikanyaga miezi miwili imeshapita maana yake mmefeli japo mtakataa.
kwa nchi dhaifu kama somalia mnaweza mkakaa hata miaka ishirini hakuna atakayewauliza lakini kitendo cha mpaka sasa kushindwa kuteka maeneo yote ya alshabab inaonesha mlivyo dhaifu, mnaposingizia mvua inamaana KDF haina wataalam wa hali ya hewa ambao wangewashauri aina ya vifaa vya kutumia wakati wa mvua na kama mmenunua vifaa kama kasuku kwanini msisubiri kiangazi ndo muanzishe vita? .
Sidhani kama hiyo ndio sababu halisi. Kwanza hao al-Shabaab wameshakataa kwamba sio wao waliowateka hao watalii etc. Kama al-Shabaab wangekuwa wamefanya hivyo wasingechelewa kutangaza kwa kishindo kwa sababu kama inavyofahamika hawa jamaa wanapenda kujisifia kila wafanyapo uharamia.Sikiza, Lengo kuu la KDF kuingia msituni somalia kupigana, ni kuwaondoa kundi haramu la wanamgambo wa alshabaab ambao kama vile vyombo vya habari zimeripoti, ni kwasababu ya visa vya utekaji nyara wa watalii na wafanyi kazi wawili wa uraia wa Uhispania wa shirika la msaada nchini Kenya...
Sidhani kama hiyo ndio sababu halisi. Kwanza hao al-Shabaab wameshakataa kwamba sio wao waliowateka hao watalii etc. Kama al-Shabaab wangekuwa wamefanya hivyo wasingechelewa kutangaza kwa kishindo kwa sababu kama inavyofahamika hawa jamaa wanapenda kujisifia kila wafanyapo uharamia.
Uvamizi wa Somalia ulishapangwa miezi kadhaa kabla ya matukio ya utekaji nyara. Hicho kilikuwa ni kisingizio tu. Hata ukisoma dondoo za Wikileaks utaona wamarekani wanadai waliwashauri wakenya kutokutekeleza huo mpango wa uvamizi. Hayo yaandikwayo na vyombo vya habari ni propaganda za kivita. Lazima kutakuwepo na sababu nyingine za kimsingi za kuvamia Somalia ambazo wanasiasa wa Kenya wanazijua lakini wamezificha!
Ok, unayo haki ya kuamini kile uaminicho. Inaonekana umesoma mchango wangu kwa papara. Nilichosema ni kwamba "wamarekani wanadai waliwashauri wakenya kutokutekeleza huo mpango wa uvamizi" na sio kwamba waliwashinikiza wakenya waingie vitani. Wakati mwingine tuliza akili ili upate kuelewa!Serikali ya marekani walikataa na kupinga wazi wazi kuwa haina lolote linlohusiana na oparesheni ya kenya nchini Somalia. Na kama ni hivyo, put links here to back up your claims. Website ya wikileaks is a propaganda website, jua hivyo. Somali pirates or kidnappers are alshabaab. kwanini usiangmize magaidi ikiwa wanaingia kenya kutekeleza maovu. That is quite ordinary
Kwanza ondoa mtazamo kuwa mie nina picha mbaya kwa kenya, kitu kimoja nikufafanulie ni kuwa Kenya na Ethiopia zina malengo tofauti kuelekea Somalia. Ujue kitu kimoja kuwa Ethiopia imekuwa imechangia sana kuisambaratisha Somalia sababu kubwa ni jimbo la Ogaden huko Ethiopia, bila shaka unajua kuwa Ethiopia ilipigana vita virefu na Somalia juu ya Ogaden. Baada ya vita Ethiopia ilijiwekea malengo kuwa haitaruhusu Serikali yoyote itakayoendelea kudai kuwa Ogaden ni sehemu ya somalia iwepo Mogadishu. Na utakubaliana nami kuwa Serikali yoyote yenye nguvu ya somalia itaendelea kudai Ogaden, kwahiyo matokeo yake ni kuwa Ethiopia inafanya kazi ya kuidistabilize Somalia kwa ajili ya usalama wake. Hapa ni tofauti na malengo ya Kenya ambayo ni kuifanya Somalia iwe na amani ina maana mnaposhindwa sasa kuleta amani maana yake mmeshindwa. Nadhani unanielewa sasa kwanini nasema Ethiopia ilitimiza malengo yake, nyie mnasema Ethiopia imeongeza matatizo kwasababu mnataka amani lakini mngejiuliza hivi ni kwanini Ethiopia iliingia kusambaratisha ICU wakati ICU ilikuwa imeanza kuidhibiti vizuri Somalia? hata kama walikuwa wanatumia sharia za kiislam siyo shida kwa nchi nyingine maana kwanza wasomali wanajifanya wana uchungu na uislam kwa hiyo sharia ni moja ya faida ambazo mtu huvuna anapoupigani uislam. Nakubali kuwa alshabab iliibuka wakati Ethiopia iko somalia lakini ujue kuwa alshabab sio kitisho kwa ethiopia mpaka pale Alshabab itakapokuwa imeichukua mogadishu na kuunda serikali. Hata kama msingeenda nyie Ethiopia ingeingia kuisambaratisha alshabab kama alshabab ingefikia kiwango cha kuunda serikali.Sikiza, Lengo kuu la KDF kuingia msituni somalia kupigana, ni kuwaondoa kundi haramu la wanamgambo wa alshabaab ambao kama vile vyombo vya habari zimeripoti, ni kwasababu ya visa vya utekaji nyara wa watalii na wafanyi kazi wawili wa uraia wa Uhispania wa shirika la msaada nchini Kenya. Ni kweli kwamba Meles na kundi lake la Jeshi Ethiopia waliingia kwa kishindo nchini Somalia na wakaweza kuwa sambaratisha ICU (somali council of islamic courts) katika mji Mkuu wa mogadishu kwa wiki mbili jinsi walivyo sema. Lakini wewe kama uko makini na uliona kilichotendeka baadaye, Ethiopia walikutana na maadui wegine, Alshabaab, na kupigana na wanamgambo hao wasiweze kuwahimidi, maana Ethiopia walishindwa. Mwishowe walitimuliwa mbio kutoka somalia bila kutimiza lengo lao kuu.
Umezuwa wazo zuri mno ya kujadili, kwamba KDF wako km 17 kutoka kwa wanamgambo hao, ingali jeshi inashindwa kuwaangamiza kundi hilo haramu. Tukipiga darubini utaona kuwa ubabe wao (Ethiopia), ulileta kuzaliwa kwa kundi haramu la alshabaab. Ujasiri huo wa vita haukuwaletea wakazi wa Somalia suluhisho, bali iliwaongezea jangaa lingine kubwa la njaa, maana alshabaab waliwafukuza shirika za misaada huku wakazi wakifa kwa njaa na magonjwa. Shida nyingine ilikuwa kuzorota kwa amani, maana alshabaab walileta kuundwa kwa sheria sugu za kiislamu za "sharia", hivyo kuwaweka mateka na kuwatesa wakazi wa somalia.
My Take on the above point:
Hawa vigogo wa vita (Ethiopia), ubabe wao haukuleta suluhisho nchini somalia, bali iliongeza shida chungu nzima. kama kuzorota kwa amani na kufanya wasomalia kuwa mateka wa alshabaab.
Ushauri wa kenya kujiunga na Amisom kulinda amani, sio ushauri wa kenya, ni ushauri wa IGAD (inter-governmental authority-development). Hebu tazama hii link na kuwa makini na usome utajua ni IGAD sio Kenya, tafadhali! http://www.securitycouncilreport.org/site/pp.aspx?c=glKWLeMTIsG&b=7886221&printmode=1
Mengi kuhusu IGAD itapatikana hapa
http://en.wikipedia.org/wiki/IGAD
Kenya, kuligana na Chief of defense forces wa KDF Mj. Gen Julius Karangi, alisema the misson will be completed as started. Ikiwa KDF itajiunga na AMISOM, ni wakati shughuli za kuwasambaratisha alshabaab itakapokamilika. Hata kama TFG wanapigana hadi kifo, ni kwa manufaa ya nchi yao wenyewe, kuleta ukombozi kwa nchi yao ambayo imekuwa mateka chini ya kundi haramu la alshabaab. Maisha na shughuli yao wasomalia itaendelea kama kawa...
Just remove the blurred picture you have about Kenya in this whole issue of the Somalia issue & you will see it is for the greater benefit of the nation of somalia in general to get rid of the hooligans & terrorists.
Pamoja na hizo kumbukumbu bado kubaliana nami kuwa Somalia ni dhaifu sana. Ktk hizo kumbukumbu zako hakuna mahali umeonesha kama kulikuwa na jeshi rasmi la Somalia, mwaka 1993 ni vikundi vya kina Aideed na Mahdi ambavyo vilikuwa hata havina kombati, walikuwa wanavizia tu kwahiyo kuwauwa wamarekani haimaanishi wasomali walikuwa na nguvu kuwazidi wamarekani.Hawa Wasomalia ambao unasema ni dhaifu, sitakuelekeza mbali. Unakumbuka "operation-blackhawk-down" 1993, Wanjeshi wa Marekani kumi na wanane walisambaratishwa na hawa unaowaita wasomalia dhaifu.
Halafu, ndege mbili za kivita za "black hawk" zikasambaratishwa zikiwa angani na hawa hawa watu dhaifu. Ikiwa Alshabaab si tisho kwa Ethiopia, mbona hivi sasa kawatuma majeshi yao nchini somalia?
Hata hivyo, jua Ethiopia hawakushinda vita hivyo vya mogadishu dhidi ya ICU. Ama kweli, kama wangeshinda, Amisom ikiongozwa na Waganda hawangekuwa humo Mogadishu wakilinda amani.
Jeshi la KDF haininui vifaa kama "kasuku". vifaa hivyo ambavyo jeshi inanunua ni vya kujilinda kutokana na adui. Kama nilivyo sisitiza awali, this is more than a physical warfare.
Sidhani kama hiyo ndio sababu halisi. Kwanza hao al-Shabaab wameshakataa kwamba sio wao waliowateka hao watalii etc. Kama al-Shabaab wangekuwa wamefanya hivyo wasingechelewa kutangaza kwa kishindo kwa sababu kama inavyofahamika hawa jamaa wanapenda kujisifia kila wafanyapo uharamia.
Uvamizi wa Somalia ulishapangwa miezi kadhaa kabla ya matukio ya utekaji nyara. Hicho kilikuwa ni kisingizio tu. Hata ukisoma dondoo za Wikileaks utaona wamarekani wanadai waliwashauri wakenya kutokutekeleza huo mpango wa uvamizi. Hayo yaandikwayo na vyombo vya habari ni propaganda za kivita. Lazima kutakuwepo na sababu nyingine za kimsingi za kuvamia Somalia ambazo wanasiasa wa Kenya wanazijua lakini wamezificha!
Pamoja na hizo kumbukumbu bado kubaliana nami kuwa Somalia ni dhaifu sana. Ktk hizo kumbukumbu zako hakuna mahali umeonesha kama kulikuwa na jeshi rasmi la Somalia, mwaka 1993 ni vikundi vya kina Aideed na Mahdi ambavyo vilikuwa hata havina kombati, walikuwa wanavizia tu kwahiyo kuwauwa wamarekani haimaanishi wasomali walikuwa na nguvu kuwazidi wamarekani.
Kuhusu Ethiopia ukumbuke kuwa ni kenya na wanachama wa IGAD walioipigia magoti Ethiopia iingie kusaidia somalia japo mpaka sasa Ethiopia haijasema imeshapeleka majeshi zaidi ya habari za kwenye vyombo vya habari.
Kuhusu kushinda vita somalia, kama tunakubaliana kuhusu lengo la Ethiopia ktk somalia basi utakubali kuwa Ethiopia imeshinda, lakini kama unadhani Ethiopia inataka kuiona somalia ikiwa imara basi utadhani pia imeshindwa.
Kama haukupangwa mbona umesubiri kuzaliwa kwa Sudan kusini? Hapa usisingizie kuteka watalii maana hata sasa KDF hawasemi wanawatafuta mateka bali wanasema wanataka kusambaratisha alshabab, kutoa misaada ya kiutu na kuleta amani somalia.Uvamizi huo haukua umepangwa. Uvamizi huo ulifanywa kwa sababu ya shughuli za magaidi wa Alshabaab ndani na karibu na mipaka ya kenya na katika pwani ya bahari. Ikiwa Kenya ingalikuwa na joto sana na Alshabaab, believe me, tungekuwa wa kwanza kuingia humo hata kabla ya Amisom na Ethiopia.
'Enemy at the Gates' situation
Somalia ni wadhaifu kwasababu wana silaha dhaifu kulinganisha na nchi nyingine, wamekosa mafunzo rasmi ya kijeshi tangu mwaka 1991, hawana kabisa mfumo wa ujasusi kwa sasa. Walichonacho ni itikadi ya kiimani tu kwa sasa inayowafanya wawe tayari kujitolea maisha kirahisi zaidi kuliko majeshi mengine.The "dynamics" of this war Kibona ni tofauti sana ndugu yangu na vita vingine vilvyopiganwa zamani hapa afrika tuseme, mbali na somalia kuwa dhaifu. Tukisema "dhaifu" in the context of somalia tunamaanisha nini? Hebu nijibu, halafu nitaona kama tuko katika ukurasa mmoja.
Kama haukupangwa mbona umesubiri kuzaliwa kwa Sudan kusini? Hapa usisingizie kuteka watalii maana hata sasa KDF hawasemi wanawatafuta mateka bali wanasema wanataka kusambaratisha alshabab, kutoa misaada ya kiutu na kuleta amani somalia.