Kenya Election 2007: Outcomes

Haya matokeo sasa naona yanapikwa kwa nini kumekuwa na uchwelewaji namna hii? Jana waliahidi kwamba angalau leo asubuhi wangetoa matokeo ya awali yaani at least 50% lakini kimya hadi sasa, kuna nini?

Kuna mtu anaibiwa hapa na italeta shida sana baadaye, tuendelee kusubiri.
 
Ninadhani kuwa Odinga ni mtu mwenye integrity ya hali ya juu. Niliwahi kusoma kuwa ni yeye aliyeunda ile rainbow coalition ya mwaka 2002 ili kuiondoa KANU madarakani, ambapo alikubali kumsimamisha Kibaki. Sababu yake kufanya hivyo ilikuwa ni kujenga umoja imara kwa manufaa ya Taifa lao wala hakuwa na uroho wa madaraka kwani angeweza kusimama wakati ule bila ya kuwa Kibaki na kushinda, ila wangekuwa fragmented sana. Kibaki pamoja na kusimamia uchumi vizuri, amekuwa na u-"bwana kubwa" na "ulafi wa utajiri" zaidi kiasi cha kulea ufisadi. Pamoja na kuwa siwajui wanasiasa hawa sawasawa, nitafurahi sana iwapo Odinga atashinda kwani hilo litakuwa fundisho kubwa sana kwa Tanzania. Kwanza, itawafaundhisha viongozi wetu kuwa madaraka hayo siyo yao milele, hivyo wayatumie kulingana na dhamana waliyopewa. Pili litafundisha raia wetu kuwa viongozi wako pale kutokana na utashi wa raia wenyewe; wasipotekeleza waliotumwa kufanya wanaweza kung'olewa madarakani na raia kwa nguvu ya kura.
 

Mkuu KT,

Ikiwezekana tuwekee na ya Kalonzo, inasaidia kujua kura ngapi zimehasabiwa na hivyo ngapi zimebaki.
 
Duh! the gap is becoming narrower by the minute!

K-T hebu tuambie kura za sasa zatoka mikoa gani? Maana kama ni central na Upper eastern tuweze jua pia kiasi gani hakijahesabiwa Western, Nyanza na Rift Valley. North Eastern naona Kibaki anaongoza. Wananishangaza sana wasomali hawa maana only social democrats can rescue them. That is the Orengos and Nyong'os. Not Kimunya's etc.

Tuambie kura za sasa zatoka wapi K-T?
 

Nilipoangalia data kwa makini jana, nilisema kuwa ushindi kwa Odinga haukuwa guranteed kwa vile amakataliwa kabisa katika jimbo la Central (ambayo ni stronghold ya Kibaki) wakati Kibaki anapatapata Kura katika strongholds za Odinga. Stronghold population advantage aliyo nayo Odinga dhidi ya Kibaki ni 1.22 to 1. Ukichukulia kuwa hiyo 0.22 ndiyo imempigia Kibaki katika maeneo yatawaliwayo na Odinga basi ni dhahiri kuwa Kibaki anaweza kushinda, japo kwa margin ndogo sana.
 

Zitto ndio demokrasia hiyo na usiwalaumu sana kwa walichofanya ingawa mie naona kuwa kura nyingi za waliopiga kwa ODM hata huko eastern hazijaletwa bado. Usisahau pia factor ya Kalonzo maana naona ataaffect eastern tu labda na north eastern lakini sio rift valley na sehemu zingine.

Raila bado ananafasi kubwa sana ya kushinda labda Kibaki afanye hicho Saitoti alichojaribu kufanya jimboni kwake kabla vijana wa ODM hawajamtimua mbio - kuiba kura
 
Kichuguu soma PM yako

Asante nimeshasahihisa; unajua nilikuwa najua kuwa aliwahi kuwa Waziri wa Fedha, Vice president, na Waziri wa Afya, ndiyo maana nilidhani alitoka KANU wakati huo. Sikuwa karibu sana na politics za Kenya tangu walipomwua Dr. Ouko.
 
Japo gap kwenye kura inapungua lakini kwenye asilimia inapungua kidogo sana kwasababu Kalonzo naye anaanza kufanya vizuri kule kwao na hivyo kupunguza makali ya Kibaki.

Bado tofauti ya laki tano ni kubwa sana kwenye idadi ya wapiga kura ya 14M.

Mimi naamini Raila bado atashinda kwa tofauti ya asilimia kama tano
 

Mwafrika wa Kike,
Nakubaliana nawe kuhusu factor ya Kalonzo. Wasiwasi wangu ni kuwa Kalonzo atapunguza kura za Kibaki Ukambani tu lakini kuna maeneo ya eastern ambayo kuna wakikuyu. Ndiko wanakotoka kina Murungi Kiraitu huko na kina Cecily Mbarire ie Runyezes. Ila bado nina matumaini makubwa sana kwani bado Kibaki hafanyi vema Magharibi inagawa wamejitokeza wachache kupiga kura. Pia watu wa Bonde la Ufa wamefanya kweli. Tusubiri tu na K-T anatuletea updates
 
Wakuu,

Nawaombeni mtulie kidogo. Bado wapo kwenye uchanganuzi wao hapo studioni. Wanawaleta wanasheria, wanademokrasia na etc wakifanya nao analyses za kura.

Wakipumzika na waanze kuorodhesha hizo results mara moja ntaziandika na kuzileta hapa.


NB:MIMI NIMEANZA KUWA NA WASI WASI PIA!

1. Mh. Zitto, Mh. Dua na Mh. Kichuguu kuna ukweli ndani ya fikra zenu kwamba kunaeza kuwa na deal ambayo inapikwa gizani. Yaani unaeza imagine wanahabari walitangaza Njenga Karuma kashindwa saa tisa adhuhuri na eti sasa ndio ECK wanatangaza hilo. Kuna stori inaenea huku kwamba kamp ya Kibaki au PNU ilikuwa inachelewesha makusudi matokeo ya maeneo yao ili eneo za akina Raila zilite mabox na results zao asubuhi mapema. Kisha hawa waserikali wangeangalia results vile zinabishana ili wajue ni kura ngapi wataongeza kwa masanduku yaliyomo ndani za mikoa ngome zao na kushinda hivyo basi. Hii ni stori lakini wahenga wenyewe wakesema lisemwalo lipo. Haki ya nani pakafanyika hivi na ikagunduliwa na wanaODM basi ni fujo tuu. Hope yetu ODM ni kwamba pia kura za Raila nyingi huko Rift Valley na pia Nyanza na hata Western zote hazijaingia.


2. Mbona tu wale maafisa wa ECK pamoja na maajenti wa vyama mbali mbali wasitumie simu ya mkononi kuripoti zipo ngapi huko waliko? Mtindo ni wangoje mpaka zisafiri tuseme kutoka Bukoba mpaka Dar...sasa maanake teknolojia ni nini wakuu?

3. Halafu amini msiamini eti kura za maeneo bunge kadhaa hapa Nairobi pia bado hazijamalizika kuhesabiwa. Au accurately speaking zimehesabiwa lakini kukatokea vurumai na utata na ni lazima warizishe kila mmmgombeaji hata kama inamaanisha kuhesabu mabox mengine upya

4. Nahisi utangazaji wa mshindi ni kesho saa za jioni.

Tuko pamoja
 
Yaani mmeanza ku-doubt ushindi wa Raila??!! watu bwana.............wa-mount kenya walisema wata-put bonge ya fight kuzuia mluo kuingia kwa state house, but realistical, it was too late....now its a matter of time kabla "msee wa kamongo" kutangazwa rais wa kenya. Wakyuki walie tu, warudi kwao kula githeri!!!!.
 
Asante nimeshasahihisa; unajua nilikuwa najua kuwa aliwahi kuwa Waziri wa Fedha, Vice president, na Waziri wa Afya, ndiyo maana nilidhani alitoka KANU wakati huo. Sikuwa karibu sana na politics za Kenya tangu walipomwua Dr. Ouko.

Kweli kabisa Kichuguu, the guy ni kama vile hajawahi toka KANU ingawa amekuwa upinzani kuanzia miaka hiyo na chama chake cha DP. Wapinzani wengi walimuona Kibaki kama spoila kwenye uchaguzi wa 1992 kwani aligawa kura za wakikuyu mwaka huo.

Raila alivyotembelea jimbo letu hapa miaka mitatu iliyopita na mwezi wa sita mwaka huu alitetea sana uamuzi wake wa kumuunga mkono Kibaki 2002 kwa kusema kuwa alimpa heshima kwa vile yeye ni senior.

Kwa sasa Kibaki (miaka 76) inabidi aende nursing home hata kama akishindwa hizi kura ili amwachie Raila alimsaidia kushinda 2002
 
CNN wameripoti kuwa matokeo yatakuwa jumamosi jioni, latest raila bado anaongoza ingawa ni slim margin!!............mashabiki wa Raila ondoeni hofu jamaa anashinda hii kitu.
 
Nasikiliza BBC sasa hivi lakini naona taarifa zao ni re runs na sio current nuz. Kwa sababu wanasema Raila ana 3.3 million, Kibaki 2.4 na Kalonzo 0.4...
 
Habari za sasa ni kuwa Mawaziri 16 wa Kibaki wamedondoka akiwemo Makamu wa Rais Moody Awori. Raila anaongoza kwa tofauti ya kama kura laki saba hivi sasa.
 
Wacha tukalale tu maana kale kahistoria ka wizi wa kura hakajafutwa kwenye vichwa vya watawala, by morning mambo mengi yanaweza kuwa yamebadilika. Tusisahau kuwa kura nyingi za wizi huku Tz zilikuwa zinatengenezwa KQ; hao waliokuwa wanawatengenezea CCM huku kwetu wanaweza kuwa bado wako hai huko KQ, na bado wako pro-govt. Mpaka ifike mahali watu tukubali kushinda na kushindwa kwa halali tutakuwa tumekata tamaa ya haki..too bad
 
Kama Jeff Koinange angekuwa bado na CNN tungefaidi sana........hata hivyo vyombo vya habari vingi vya magharibi vilikuwa vimejipanga kwa Uchaguzi wa kenya kama "big nuz" ya kufunga mwaka................lakini mmmmmmh al qaeda wakaiba ze spotilaiti!!!!!. Binafsi, I got a feeling that no matter what, Raila anaibuka kidedea.
 

Kweli Zitto,

Inaonekana ni ngumu ila ushindi wa Raila unaonekana bado uko wazi na kumbuka pia kura za Nyanza karibu laki tano hazijaingia ingawa hii inaweza isiwe factor sana kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…