Kwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo mambo yanazidi kujiweka wazi zaidi na labda kutoa picha halisi ya wizi wa kura.
Makamishina 4 wamekiri kwamba kulikuwa na kasoro ambazo zilitolewa na vyama husika, lakini wakaweka pamba masikioni.
Mzee Kivuitu hatimaye jana kaongea na huku akiwa anasikika kama mtu mwenye jazba na woga, akasema wao kama ECK hawana kosa, walisoma kile walicholetewa kutoka kwenye majimbo. Lakini akakiri kwamba kuna baadhi ya majimbo ambayo yalikuwa na utata na hasa watu wa EU waliposema kwamba mbona figure iliyosomwa kwenye jimbo iko tofauti na ile ambayo imesomwa na wao ECK. Huyu jamaa hakusikiliza hiyo hoja, bali jana ndiyo kaiongelea eti ilimshitua, kwanini hakushituka tangu siku alipotangaza matokeo?
Kulikuwa na dalili zote za ukora wa kura na hasa baada ya kucheleweshwa kura kutoka majimboni na wahusika kuzima simu. Hizo zilikuwa dalili tosha kwamba watu walikuwa wanatengeneza matokeo, na hata yeye alisema kwamba labda wanaweza kuwa wanatengeneza matokeo! Kwanini hakuchukua hatua za haraka ili ajiridhishe kwamba data alizopewa zilikuwa ni sahihi kwa kuomba masanduku ya kura yahesabiwe upya ili kujua ukweli wa mambo? Pamoja na kelele zote za wapinzani pale KICC huyu mzee hakutaka kuwasikiliza na akaja kufanya alichojua yeye.
Amesema alishinikizwa kutangaza matokeo, lakini nakumbuka pia alishinikizwa asitangaze matokeo pale KICC lakini kwa jeuri aliyo nayo aliendelea kutangaza pamoja na makelele ya watu. Iweje akubali kushinikizwa na PNU lakini asikubali kushinikizwa na ODM? Huyu jamaa kweli yuko fair? Above all EU na watu wa human rights wa Kenya waliomba aahirishe kutangaza matokeo, lakini bado akaendelea kufanya hivyo! Je, jamii ya wakenya iendelee kuwa na imani na mtu kama huyu aliyeahidi kuacha legacy nzuri? Ninadhani ataondoka na aibu yake kwa kushindwa kutenda haki huku akijua wazi kwamba hakutimiza wajibu wake, may be alikuwa anasema kwamba kwa kuwa jamaa ni wapinzani hawawezi kufanya lolote zaidi ya kulalamika.
Swala jingine, hivi ni kwanini kila mara alikuwa akisema kwamba mtu asiporidhika na matokeo, aende Mahakamani ambako ni upande wa pili wa barabara, huko ndiyo haki itatendeka. Jana kasema ECK ikigundua kuna tatizo kubwa itaenda yenyewe mahakamani, swali ni kwenda kufanya nini? Kwenda kujishitaki wenyewe kwamba hawakutenda haki? Hata kama akienda mahakamani naona ni sawa na kesi ya nyani kuipeleka kwa nyani mwingine!
Kwa aliye na ufahamu wa wazo la wale makamishina 4, kwamba iundwe Judicial Commission of Inquiry, inaundwa na idara ya mahakama ama na watu gani? Ni nani anateua hao watakao unda hiyo tume? Ni Kibaki ambaye ni mtuhumiwa au ni nani anateua hiyo tume?
Naona mwisho wa siku Raila ataishia kupoteza kwa jinsi mazingaombwe ninavyoona yanaendelea kujitokeza. Ngoja tusubiri akina Tutu, JK, M7, Kufour na wengineo watafikia muafaka gani kwenye hii kadhia.