Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa ndipo walipovurunda kwa kudhani kuwa wao tu ndio walizaliwa wawe watawala wa Kenya. Ni kweli wangeweza kumwacha Odinga atinge Ikulu huku wakihakikisha kuwa atakuwa analinda msalahi yao. Tatizo lao ni lile la kuwadharau waluo japo ukweli ni kuwa per capita ya waluo waliokwenda shule ni kubwa sana kuliko ya wakikuyu.
ii) Option ya maana sana kwa sasa ni international community na viongozi wa kiafrika (AU) kumsuta Kibaki na kumshinikiza kukaa pembeni wakati hii mess ikiwa sorted out. Pamoja na kwamba hamna imani na Jaji Mkuu wa sasa, kama ndivyo katiba inavyosema itabidi ashike mamlaka kwa muda kama Kibaki ata-bow to pressure maana sio sawa kuwa na vacuumu kwenye uongozi na sidhani kama ni mwafaka sana kuwaachia wanajeshi. Wasiwasi wangu ni kwamba wanajeshi wakishika usukani sasa haitakuwa rahisi kuachia pindi watakapoonja tamu ya state house na huko mbele watajigeuza kuwa civilian leaders na kugombea uongozi na tutatengeneza M7 mwingine.
....jamani mbona mnasahau wakenya wanapiga kura kwa line za ukabila na sidhani kama kikuyu wanafikiria wao ndio watawala wa Kenya au sasa wote ni guilty kwa sababu Kibaki ni kikuyu lakini kumbuka hata ODM kuna wakikuyu ,ni kweli Kikuyu ndio wameshika njia za uchumi na utajiri mwingi kutokana na tabia zao lakini sio serikali imewapa utajiri,Kenya ukabila ni order of the day na wanachukiana waziwazi ila hii fraud ya kibaki ndio imewapatia sababu ya kuchapa kikuyu lakini sabau kubwa kwa wengi ni chuki za kikabila na wala sio wizi wa kura maana kura kaiba Kibaki na cronies wake anakuja kuuawa mama na mtoto kule Eldoret,ndugu wakenya nawaonya mkianza kuua kikuyus msifikiri kikuyu watakaa kimya na wao watawaua tuu tena sana maana watakuwa na hasira ya revenge mmewaua ndugu zao and they will kill you with a passion na sasa hivi wana serikali na wengi wao wana pesa sana,bora sasa mgundue mbaya sio kikuyu ila ni serikali ya Kibaki na muungane mumtoe ila mkiua kikuyu tuu mjue kitakachofuata is a full scale war!
Naomba waafrika wenzangu kuboresha katiba zetu,ili kupunguza nguvu ya taasisi ya Urais ili kuepusha wanasiasa waroho kusababisha machafuko.
Hivi Kalonzo kapotelea wapi? Ni kama yeye ana nafasi kubwa ya kusaidia kwenye hili suala.
Nasikia Kalonzo ni mlokole? Jamaa inaelekea alikuwa anataka kuwa makamu wa rais.
Mimi mawazo yangu ni kwamba tatizo hapo naliona kwenye electoral law inayoruhusu simple majority.Kwa uchaguzi huu wa Kenya,ilitakiwa first na second wachuane kwenye round ya pili baada ya siku 21. Hali hii wangeweza kumpata mshindi halali ambaye ana mandate ya watu wengi kama alivyopatikana rais wa Liberia Madame Hellen Sirleaf. Kwa mfano Liberia wangetumia mfumo wa Kenya,George Weah angekuwa Rais. Naomba waafrika wenzangu kuboresha katiba zetu,ili kupunguza nguvu ya taasisi ya Urais ili kuepusha wanasiasa waroho kusababisha machafuko.
Hivi Kalonzo kapotelea wapi? Ni kama yeye ana nafasi kubwa ya kusaidia kwenye hili suala.
Nasikia Kalonzo ni mlokole? Jamaa inaelekea alikuwa anataka kuwa makamu wa rais.
Nimesikitishwa na kitu kimoja kwamba vile viti 12 vya wabunge wa kuteuliwa siyo sheria, bali yalikuwa ni makubaliano tu. Kwa hiyo kuna hisia kwamba kwa kuwa Kibaka amepata viti 35 tu, anaweza kuvichukua viti vyote 12 akateuwa watu wake ili awape nafasi za uwaziri.
Hata mimi nimesikia hivyo juu ya hili la viti 12. Hapo kuna kasheshe kubwa sana.
I hope watawala wetu wanaona na watajifunza kwamba ni muhimu kweli mwaka huu
tuiangalie upya katiba yetu kwa faida ya nchi yetu, sisi wenyewe na vizazi vyetu.