Kenyan-Tanzanian
JF-Expert Member
- Nov 7, 2006
- 302
- 2
WAKUU,
NEWS MPYA HII HAPA:
TIME: 9.03AM
SOURCE: KTN TV
NATIONAL RESULTS KUFIKIA SASA
a) Raila - 3, 974, 715
b) Kibaki - 3, 580, 602
c) Kalonzo - 535, 363
___
PERCENTAGE ZA KURA ZILIZOKWISHA HESABIWA TOKA KILA MKOA
90% of Central,
87% of Eastern,
65% of Rift Valley,
60% of Nyanza,
55% of Coast,
50% of North Eastern,
55% of Western,
45% of Nairobi results in.
VYAMA NA NAMBARI ZA VITI VILIZOSHINDA
1. ODM 91
2. PNU 32
3. ODM-K 12
4. SAFINA 4
5. FORD PEOPLE - 3
6. NARC - 3
__________________________
1. Hawa majamaa waserikali au PNU bado wanashikilia mabox za huku Eastern watokako wameru ambao ni ngome ya Rais Kibaki.
2. Ruto na Nyagah wa ODM PENTAGON wamewasili Nairobi kwa ofisi kuu za ECK na kuitisha mkutano na wanahabari. Wameomba Kibaki aingilie kati na kuwaeleza maafisa wa ECK wafanye hala hala na halali jili usalama wa nchi unatishiwa na kadri mda unavyozidi kuyoyoma bila mshindi kutolewa. Wameuliza swali: Kuna nini inaendelea huko Meru ambako sio mbali sana na Nairobi takriban safari ya masaa mawili kwa gari?
3. Wawili hao pia wameuliza ni kwanini mkuu wa ECK haonekani hewani au hadharani? Kwa masaa 9 imeyopita inasemekana kwamba mkuu huyo, Samuel KIvuitu hapatikani hewani hata kwenye simu. Wanaotangaza matokeo rasmi ni baadhi ya wale maafisa wapya wa tume hilo walioajiriwa na serikali chini ya madai ya upinzani kwamba wamewekwa huko awali ili wafanye wizi wa kura. Zaidi ni huyo ambaye ni makamu wa Kivuitu.
4. Nyagah alinukuliwa live na wanahabari akisema kwamba kumefanyika wizi mkubwa wa kura kwenye ngome za PNU huko Mikoa ya Central na Eastern jana baada ya kuonekana kwamba ODM ilikuwa inashinda tangu jana asubuhi. Kumbukeni yeye anatoka hizo sehemu ingawaje ako ndani ya timu ya Raila/ODM. Alisema hivi sasa amesikia fununu kwamba wapambe wa Kibaki ikulu wanasema eti kama "plani" iliweza kufanyika USA na NIGERIA mbona sio KENYA? Nyagah alidai kwamba polisi wamewekwa wengi sana nje ya eneo la makao makuu ya ECK na wananchi hawawezi hata kuja pale njee kusubili kura za viongozi wao. Kwa maoni yake, Nyaga aliona ni kana kwamba Serikali na ECK zinataka ku announce kura imeshindwa na Kibaki na wananchi wakitoa fujo basi polisi wapambane nao.
4. Hizi picha zaonyesha maaskari wanaopatrol njee ya makao ya ECK hivi sasa.
5. Wacha tuendelee kusubiri ila PNU ikiiba hizi kura basi na ole wao....nchi inaeza kubadilika.