Hivi kuna njia yoyote ya amani ambayo inaweza kuitoa Kenya kwenye hii "vita ya wenyewe kwa wenyewe"?
Kama tetesi zinazodai kwamba jeshi la Kenya limegawanyika ni za kweli basi nadhani kuna balaa kubwa zaidi ambayo inaweza kuwakumba majirani zetu. CDF (Chief of Defence Forces) wa Kenya ana ubavu wa kuzuia uasi wa wanajeshi wanaosemekana wanam-supportt Raila na ODM?
Wanaojua lolote, je msimamo wa Tanzania kwenye huu uchaguzi wa Kenya ni upi? (Kama serikali imeishatoa msimamo)
Kuna tetesi kwamba Mkuu wa Jeshi la Polisi amejiuzulu na hajasema lolote tangu jana na hiyo inasemekana ni kutokana na kugoma kusupport ku-declare state of emergency. Je, ni nani ana-declare na kuna uhusiano gani na Mkuu wa Polisi?
Pia kuna tetesi kwamba Jeshi la Ulinzi la Kenya liliombwa litoe askari ili waingie mtaani kwa ajili ya kuwashughulikia wanaofanya fujo, limetoa msimamo kwamba haliwezi kufanya kazi ya polisi.
Kwa walio Kenya and if at all wana access na mtandao wanaweza kutupa updates ya hizo tetesi and what is going on. Ninadhani hali ni mbaya zaidi na ndiyo radio, magazeti na TV za binafsi zote zimezuiwa kurusha matangazo.