Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

If they rigged the vote count, then a recount can rectify the situation but if they stuffed ballot boxes with illegal votes then probably this measure will not repair the damage.

Re-count itasaidia maana matokeo yaliyo kwenye boxes ni tofauti na matokeo waliyopeleka ECK Nairobi. Walichofanya ni election doctoring. Ni philosophy mpya iliyogunduliwa Afrika, nafikiri ilianzia Zanzibar 1995, sasa inaenea kote.

Tunapoteza muda kuja na mbinu mpya za kuua jamii zetu badala ya mbinu mpya za maendeleo.
 
Hivi kuna njia yoyote ya amani ambayo inaweza kuitoa Kenya kwenye hii "vita ya wenyewe kwa wenyewe"?

Kama tetesi zinazodai kwamba jeshi la Kenya limegawanyika ni za kweli basi nadhani kuna balaa kubwa zaidi ambayo inaweza kuwakumba majirani zetu. CDF (Chief of Defence Forces) wa Kenya ana ubavu wa kuzuia uasi wa wanajeshi wanaosemekana wanam-supportt Raila na ODM?

Wanaojua lolote, je msimamo wa Tanzania kwenye huu uchaguzi wa Kenya ni upi? (Kama serikali imeishatoa msimamo)

Kuna tetesi kwamba Mkuu wa Jeshi la Polisi amejiuzulu na hajasema lolote tangu jana na hiyo inasemekana ni kutokana na kugoma kusupport ku-declare state of emergency. Je, ni nani ana-declare na kuna uhusiano gani na Mkuu wa Polisi?

Pia kuna tetesi kwamba Jeshi la Ulinzi la Kenya liliombwa litoe askari ili waingie mtaani kwa ajili ya kuwashughulikia wanaofanya fujo, limetoa msimamo kwamba haliwezi kufanya kazi ya polisi.

Kwa walio Kenya and if at all wana access na mtandao wanaweza kutupa updates ya hizo tetesi and what is going on. Ninadhani hali ni mbaya zaidi na ndiyo radio, magazeti na TV za binafsi zote zimezuiwa kurusha matangazo.
 
Kenyan Tanzanian
Nasubiri kwa hamu kusikia what will be the next step, kwa sababu sasa ivi inaonekana imedhihirika wazi kuwa watu wa Kibaki wameiba kura. Tunawapa pole sana ndugu zetu, wizi huo huku Tanzania tumeuzoea. Tupo kama una updates tupatie!
 
Kuna mahali nimesoma kwenye hii thread kwamba "watu walio karibu na Kibaki" baada ya kuona wameelemewa na Raila kwenye kura za urais, walimshauri Kibaki a.k.a Kibaka, kwamba watumie janja ya kuiba kura ili jamaa ashinde. Kuna sehemu nyingine nimesoma wakenya wanadai haya yote yamesababishwa na Mzee Michuki (zama zile alikuwa waziri wa mambo ya ndani). Kuna ukweli wowote kwenye hili?
 
Mkuu Keil

Kwa sasa sijui nani atakuwa muamuzi wa mambo ya kenya solution ni Jeshi kuchukua nchi tu. Bado nafikiria nini kitatokea saa nane ambapo Raila amesema anaapishwa na wakenya kuwa Raisi.

Hiyo ndiyo itakuwa mwisho wa maneno nafikiri Kibaki anacheza na Demokrasia, sasa amelikoroga lazima alinywe.

Watu waliokuwa wanaona mbali ushauri uliotolewa wa kutotangaza rais ulikuwa wa maana sana.

Sasa sijui Internationals, African Union wako wapi. Au wanasubiri watu wafe wengi ndio watoe matamuko ya kumwambia Kibaki aondoke madarakani.

Mimi namtabilia Kibaki mabaya.

Kibaki will go, forever
 
Sasa sijui Internationals, African Union wako wapi. Au wanasubiri watu wafe wengi ndio watoe matamuko ya kumwambia Kibaki aondoke madarakani.

Sioni kati ya hao uliowataja ambaye ana ubavu wa kumwambi Kibaka Kibaki aondoke madarakani. Haya mambo ya politics ni ya ajabu sana. US tayari imeishatoa msimamo wake, sidhani hata kama waliwasiliana na Balozi wao ambaye ameshinda pale KICC kwa siku mbili mfululizo akifuatilia matokeo na alitoa dukuduku lake kwa ECK lakini hakusikilizwa.

AU ndo usiseme kabisa, maana kama kumshughulikia Mugabe wameshindwa unategemea waseme nini kwa Kibaka? Unajua viongozi wengi wa Afrika ni wanafiki sana na wote agenda zao zinafanana na ndiyo wanaogopa kusema ukweli maana nafsi zao zinawasuta. Huwezi kumwambia mwenzako aache wizi wakati na wewe uliingia madarakani kwa wizi ama unategemea kurudi Ikulu kwa kutumia wizi huo huo. Term ya kwanza unaweza kuingia kwa haki, lakini term ya pili kurudi ni ngoma nzito. Hata JK sasa hivi anaendelea kutafakari juu ya uchaguzi wa 2010, maana hajui nini kitatokea. Nimeona Kipanya leo hii nikacheka kweli. Kibaki amekaa kwenye kiti ananyolewa halafu JK yuko kwenye deep thinking, Kipanya anamuuliza vipi una baridi???????????????
 
Where are the African presidents? AU hili sio swala la Kenya peke yake hivi sasa. Mbona wako kimya badala ya kutoa hukumu yao hivi sasa wakati raia wasio na hatia wanateketea.

JK, M7, Mbeki etc. Where are you? Stand up to be counted.
 
Hivi hawa Inernational Obsevers kazi yao hasa ni nini?? Maana mara nyingi huwa hawako very open na taarifa zao kuhusu matokeo ya uchaguzi. Mambo yao wanayafanya kisiasa siasa tu!!! KIBAKA ilaaniwe mara mia moja!!!!! Kama MOI aliachia madaraka baada ya kushindwa yeye anataka kuleta nini??? Kumbe MOI NI BORA KULIKO KIBAKA!!!
 
Kibaki amekaa kwenye kiti ananyolewa halafu JK yuko kwenye deep thinking, Kipanya anamuuliza vipi una baridi???????????????


Kuna watu wanasema kwetu hayawezi kutokea. Hila hatujapata upinzani wa kutosha ukifika ndipo tutaona Kipanya alichokuwa anafikiria.

Hatuna budi kuwa na katiba zenye kuangalia mbali. Leo ni Kenya kesho ni sisi.

Urais jamani ni mtamu mno. Angalia sasa Kibaki yuko Ikulu sijui anakula kuku kwa mrija na wananchi wake wako hoi.

AU nafikiri angalau kutoa tu msimamo lakini labda cha kuuliza AU ni akina nani? Ndio wale wale aliyowachora kipanya?
 
Where are the African presidents? AU hili sio swala la Kenya peke yake hivi sasa. Mbona wako kimya badala ya kutoa hukumu yao hivi sasa wakati raia wasio na hatia wanateketea.

JK, M7, Mbeki etc. Where are you? Stand up to be counted.

Mbeki si ulimuona alivyo na uroho wa madaraka wakati wa ANC. It's only that he is in RSA. Angekuwa kwenye hizi nchi zetu I am sure I could have gone beyond what people could have imagened. M7 ndiyo kabisa!!! Nafikiri kwa sasa jamaa wanafikiria hata namna ya kumpongeza wanashindwa. Maybe wanasubiri mkutano wa Raila wapate mwelekeo!!!
 
Watu wa Kubeba lawama Kenya
1. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi - Huyu ametumia madaraka aliyopewa vibaya-FISADI (Mshitakiwa number moja)
2. Mteule wa mwenyekiti aliyeko Ikulu ya Kenya akishikiria kiti kwa Muda- Mwai Kibaki(Huyu jamaa lazima afikishwe Arusha kwenye mahakama akiwa mshitakiwa number mbili)
 
Kuna watu wanasema kwetu hayawezi kutokea. Hila hatujapata upinzani wa kutosha ukifika ndipo tutaona Kipanya alichokuwa anafikiria.

Hatuna budi kuwa na katiba zenye kuangalia mbali. Leo ni Kenya kesho ni sisi.

Urais jamani ni mtamu mno. Angalia sasa Kibaki yuko Ikulu sijui anakula kuku kwa mrija na wananchi wake wako hoi.

AU nafikiri angalau kutoa tu msimamo lakini labda cha kuuliza AU ni akina nani? Ndio wale wale aliyowachora kipanya?

Hayo mambo yametokea hata Tanzania, huko Zanzibar. Tofauti tu ni moja kwamba kule Zanzibat wana wajomba wao wa bara ambao wanapeleka jeshi na polisi ambao wako tayari kuua kila anayekuja.

Kenya ni tofauti maana hata hao polisi walioko mitaani na wenyewe ni stakeholders kwenye politics za nchi yao, wengine wana ndugu wanaoandamana na wengine wamempigia kura Odinga na wanajua haki zao zinaibiwa.

Kwa Tanzania itakavyofikia kwamba nchi nzima kuna upinzani wenye nguvu kama huu wa Kenya na serikali inataka kuiba, yatatokea.

Nafikiri mnajua jinsi Sierra leone ilivyokuwa peaceful na sasa miaka 10 wanahangaika kurudisha amani.

Ni rahisi sana kuvunja amani na utulivu lakini sio rahisi kuvijenga hivyo vitu viwili.

Mtaji wa nchi maskini lazima uwe a fair sytem for all. Kama akina JK wanaangalia, tafadhali hiyo tume ya uchaguzi na katiba vitakuja kutuweka na sisi hapo walipo Kenya.

Nimeona majibu ya Spika kwa Zitto, kweli inaudhi, sijui hawa viongozi wetu wanajifanya miungu?
 
Lakini hapa Kibaki asilaumiwe sana, ni kama ameburuzwa na watu kuingia kwenye hiyo hali. Unajua mtu ukifikia ngazi ay urais there is nothing to worry about, utamu unaendelea tu hata ukistep down, halafu mkumbuke kuwa Mzee Kibaki sio kijana mwenye uchu wa madaraka. Kuna watu ambao wana wasiwasi(Sio Kibaki)kuwa Odinga akiingia madarakani basi wao watakuwa na hali mbaya, hao ndio wamefanya mambo ili kuhakikisha Kibaki anarudi madarakani kwa wizi wa kura!
 
Kuna mtu kaleta rumors kwamba Raila amekamatwa, na William Ruto ameumizwa kwa risasi. Any verification for this please?
 
Where are the African presidents? AU hili sio swala la Kenya peke yake hivi sasa. Mbona wako kimya badala ya kutoa hukumu yao hivi sasa wakati raia wasio na hatia wanateketea.

JK, M7, Mbeki etc. Where are you? Stand up to be counted.

Dua,

sahau umoja wa Afrika au umoja wa East Afrika. Sisi Watanzania lazima tujitahidi kuanzia sasa kuzuia yanayotokea Kenya yasije kwetu. Huwezi kuunganisha nchi wakati kuna mijitu ambayo haiheshimu demokrasia na haki za watu wengine. Huko ni sawa na
kuijiingiza kwenye vita ya Watusi na Wahuti.

Hakuna nchi ya Afrika ambayo itamlaani Kibaki, yeye ni mmoja wao, ni jambazi kama wao, ni fisadi kama wao.

Wananchi wa kawaida tuko na Wakenya kwenye hilo na tuombee wafanikiwe hata kama itakuwa kwa nguvu ya upanga.

Inabidi ifike mahali hawa wakuu wetu wafundishwe kwamba demokrasia ni lazima whether wanapenda au hawapendi kwani ndio njia pekee itakayosaidia kuondoa vuruga na umaskini mkubwa tulio nao.
 
Kuna mtu kaniambiwa kuwa Odinga amekamatwa kwa uhaini,

kuna mwenye maelezo zaidi ya kilichotokea?
 
I want JK to say something on behalf of Tanzanians. He is the one who's the President.
 
Back
Top Bottom