Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

Kama unakumbuka mapambano ya Afrika kusini ili kuondoa ubaguzi. Waafrika wengi sana walikufa ikiwemo wazungu wasio na hatia. Watu waliuwawa wakiwa mashuleni na makanisani kama hawa wakenya.

Wakati yote yakiendelea, kuna watu walishauri kuwa damu inayomwagika ni muhimu kuliko mandela na kutaka waafrika wakubali tu waendelee kuishi na wazungu kama red indians walivyokubali yaishe na wakaendelea kuishi na wazungu america.

Ulichokisema hapo, hakina tofauti kabisa na wakatishaji tamaa walichosema wakati wa kupigania uhuru. Hakuna anayefurahia damu kumwagika lakini pia si kweli kusema kuwa isipomwagika basi ndio mwisho wa vifo. Madikiteta wasipoua kwa bunduki, basi wanauwa kwa starvation na magonjwa kama anavyofanya Mugabe huko Zimbabwe.

Chaguo ni je, watu wafe sasa hivi kupigania haki au wasubiri hapo baadaye watakapokufa kwa njaa na magonjwa yanayotibika?

OK. Lets shed some blood; why not start by the root cause, that is Kibaki? kwanini kila mara manyang'au yanayosababisha mauaji na migogoro huwa yanabaki hai wakati wachovu ambao ndio huwa wanawaweka madarakani wanakufa; then this time afe Kibaki!
 
Mwendapole:
Hakuna anayependa damu ya watu maskini na wasio na hatia kumwagwa. Lakini inaelekea wewe ni 'pacifist' wa ajabu mno. Marekani kila leo wanakubali kwenda nje ya nchi yao kwenda kumwaga damu za watoto na maskini wa nchi zingine - ulishajiuliza kuwa wao hawaoni kuwa watu maskini na wasio na hatia wanauawa katika kutimiza malengo ya nchi yao?

Sasa niambie, kwa mtu anayekuonea hapo hapo nyumbani kwako kwa maksudi, halafu anauonyesha kuwa huna lolote utakaloweza kumfanyia. Yaani wewe una maana huyo jambazi haoni kuwa watu maskini wanakufa? Na akijua dhahiri kuwa sababu ya maskini hao kupoteza maisha ni kwa sababu ya upuuzi anaoendelea kuwafanyia?
 
Jamani Africa tueleweni Kenyans at the moment are fighting for their independence and nothing else. kwani tulipokuwa tunamfukuza beberu tulijali mambo ya blood shed. Jueni kabisa kwamba akishinda kibaki Africa will be doomed wakubwa wataendelea kuwa wakubwa milele.

tutakufa tukilalammika ooooh mikataba mibovu ooooh hakuna kazi oooh kuna upendeleo. kwani unadhani the Royals of England are now toothless dogs kwakuwa ilikuja yenyewe, it took people like Olive Cromwell kuweka mambo sawa.
 
Huu uchomaji wa nyumba za ibada na mauaji ya kiholela hayakubaliki kamwe, kibaki&co + raila&co, ni warloads wanastahili kujibu mashitaka ICC. Nashukuru EU & U.S kuingilia kati mzozo huu.
 
OK. Lets shed some blood; why not start by the root cause, that is Kibaki? kwanini kila mara manyang'au yanayosababisha mauaji na migogoro huwa yanabaki hai wakati wachovu ambao ndio huwa wanawaweka madarakani wanakufa; then this time afe Kibaki!

Mwendapole,

Zaidi ya nusu ya raia wa Zimbabwe wanaishi nje ya nchi yao. Those guys wanapenda sana Mugabe afe na wangefanya chochote ili kumuua. Unadhani kwa nini Mugabe bado yuko na anazidi kuchapisha pesa mpya kila leo?

The answer is simple, It is very hard to kill or remove a dictator once the reasonable time has passed on.

Madikiteta wengi wanaanza taratibu kama Kibaki na wakikaa madarakani long enough, wanajenga security system ambayo ni ngumu sana kuwaua wao peke yao. Unakumbuka kina Taylor, Doe na wengine?

Nirahisi sana kusema kuwa Kibaki auwawe kama ilivyo rahisi kusema kuwa Mugabe auwawe lakini ukweli unaonyesha kuwa haya hayatokei kwa urahisi hivi.
 
Amani haipatikani bila ncha ya upanga! Bila Raila kuingia msituni hakuna kitakacho eleweka, mabavu pekee kwa sasa ndio yanayoweza kumtoa kibaka ikulu, vinginevyo tutashuhudia msururu wa miafaka. Nawasihi wakenya kuendeleza mapambano kwa gharama yeyote hata kama ni damu wacha imwagike tu.
Kuna taarifa kuwa kenyetta kabla hajafa alimwabia moi kuhakikisha kenya isije tawaliwa na the Luo hence the death of Mboya and Ouko. Kwamba watawala wawe kikuyu na kalenjin, ndio kisa cha moi kumpigania uhuru 2002 hata kama hakuwa na uwezo, na aka wasa sideline akina Raila, Saitoti, Musyoka etc watu walikuwa more expirienced than uhuru. Believe me handleover in 2002 ilikuwa smooth kwa sababu it was a kikuyu!!
 
Huu uchomaji wa nyumba za ibada na mauaji ya kiholela hayakubaliki kamwe, kibaki&co + raila&co, ni warloads wanastahili kujibu mashitaka ICC. Nashukuru EU & U.S kuingilia kati mzozo huu.

katika EU na US unaota mkuu,

hawa jamaa ni wazuri sana kwa kusema lakini utekelezaji ni kazi. Usikute hata jamaa ndio wanachochoea mambo ili wauze silaha? wake up and smell the coffee.

Marekani iliitambua serikali ya Kibaki wakati nchi nyingi tu zikikataaa hadi walipoona aibu wakabadilisha msimamo.

Mabepari wengi hawataki Raila awe madarakani maana ameahidi kuwafyagilia mbali. Just wait and see utasikia France nayo imemkubali Kibaki!

Afrika ni yetu na sisi wenyewe ndio tutawatoa hawa wakoloni weusi wanaoneemeka huku mamilioni ya watoto wetu wakifa kwa magonjwa yanayotibika.
 
Raila alishinda uchaguzi wa urais, lakini ameshindwa kuulinda ushindi wake usiporwe. Na hata baada ya kuporwa, ameshindwa kabisa kuurejesha. Na sasa hivi ameshindwa rasmi. Kosa lake ni moja, na nililisema toka mwanzo, kuchelewa. Waswahili husema "chelewa chelewa utamkuta mwana si wako", naye kwa kosa hili, tayari "kamkosa mwana na maji ya moto"! Hiyo rally alitakiwa kuifanya siku ileile alipoapishwa Kibaki, au kesho yake na si zaidi ya hapo. Sasa hivi hamwezi tena, keshachelewa, maana amemsubiri hadi akajiimarisha upya. Sasa hivi nasikitika kusema, Raila atabakia mlalamishi tu, na kina Kibaki watakuwa wanabeza tu kelele zake wakisaidiwa na methali ya "kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji".

Inasikitisha, lakini imeshakuwa hivyo. Poleni sana ndugu zetu.
 
Kumuondoa Kibaki ni sawa; but at whose/what cost?
Kuondoka kwa njia ya amani,kwamba atakubali kaiba kura ajiuzulu hiyo haipo; kumuondoa kwingine ni kwa mabavu, na mabavu yanayotumika sasa sio ya kumuondoa Kibaki kama Raisi, ni ya kuondoa uhai wa wananchi wasio na hatia; ingekuwa wanamuondoa kwa njia ya bloodless coup, ambapo mwathirika angekuwa yeye mwenyewe Kibaki na wezi wenzake hapo ningekubali; as it is; kweli jamani what did the people in the church had to do with Kibaki's robbery if we call it that? hivi vifo vya walalahoi vitasaidiaje kumtoa kibaki madarakani...I mean, there are better ways of handling the matter..Kibaki kaiba kura sawa; yeye na wezi wenzie ndo washughulikiwe; hakuna mtu ataenda kwa Kibaki nyumbani au ikulu kumuuua so why the senseless killings in the street. Kwa idadi ya watu wanaokufa na kuathirika kwa mambo haya ni heri Kibaki angekufa if that would restore Kenya's peace and stability; but we can be sure kwamba hata Kibaki akiuawa leo damu ya innocent Kenyans ndo itamwagika vibaya in the name of tribalism and other stupid excuses.

Kwa maana nyingine ni kwamba kuondoka Kibaki madarakani leo kama sio kwa hiari yake basi ni kwa gharama vifo vya ya mamilioni ya wakenya; so if you are to choose a better evil you better make your calculations right

Mwendapole,

Hata kule SA, ni viongozi wachache sana wa makaburu walikuwa wanaguswa.

Ni makosa kuchoma makanisa na kuua wanawake na watoto lakini vijana inabidi waendelee kwenda mitaani hata kama uchumi utaharibika kwa muda. Wasipofanikiwa sasa, yatakuja kutokea tena, ni bora kutibu kansa moja kwa moja ili isije ikarudi tena baada ya miaka 5, 10 au 15.

Viongozi wengi sana wa Afrika akiwemo Mugabe wanaangalia kinachotokea Kenya.

Sisi waafrika waoga sana na tunakimbilia kusema amani wakati in real sense hakuna amani yoyote. Ni amani gani wakati tunaibiwa na wanaotuibia wapo, eti tunawaangalia tu.

Si umeona Yugoslovakia, walimalizana na yule dikteta lakini wangemwacha kwa kuogopa vifa, mpaka leo bado kungelikuwa na matatizo.

Wakishindwa kumwondoa Kibaki baada ya mambo yaliyotokea itakuwa balaa kubwa kwa Afrika. Inabidi kila siku waendelee kwenda na wafuasi wake wataanza kumsaliti mmoja baada ya mwingine, mpaka itabidi afunge mizigo yake na kukimbia.
 
Tuseme ukweli, panga na marugu hayakumzuia gen.kagame kuingia kigali, wala hayajamtoa gen.M7 kampala! kenya hakuna Garamba hideout, labda martin ojul amsaport kwani yuko hapohapo nrb. Jeshi la kenya halitazidiwa nguvu simple like that. Angetaka vita angeanza tu kama Joseph Kony au Laurent Nkundabasazi.
 
lazima kibaki aondoke, hii ni lazima he cant force kenyans to accept him aondoke na michuki tumuone sasa.
 
A recount should be conducted by an independent person transparently and with close supervision from both parties and ultimately a recount to be done.
 
Mimi namshangaa sana huyu Kenyan - Tanzanian kwa kum support Raila katika njama zake za kuigawa Kenya. Kibaki anaweza kuwa mkabila lakini huyu Raila ni muuaji ana organise watu wake waenda kuua wakikuyu kanisani! jamani hata Kanisani? Hii ni hatari sana, we are carried away na hizi events zinazojiri Kenya na lakini hatari iliyopo mbele yetu ni Kenya wanaweza kumtoa mkabila Kibaki na kumuingiza muuaji Raila.

Raila kama unaona aliyekunyima urais ni Kibaki chonde chonde waache in peace wakikuyu kuendelea kulazimisha wauawe hakukusaidii, hivi utakapo ingia huko Ikulu utatawala waluo na wakalenjin tu?

Kenyan - Tanzanian naomba nikupe polite ombi pamoja na hamasa na ufurukutwa wako kwa Raila nakuhakikishia huyu mtu hana heri na Kenya, mwanzoni hata mimi nilikuwa nina sympathize nae lakini as the days goes on the man is showing his true colour hawafai wakenya na hatufai wa east africa.

All said and done si support foul alizofanya Kibaki (if any) lakini ndugu zangu wa Kenya yasije yakawakuta ya Wazambia walipomtupia virago mzee Kaunda na kumuingiza Chiluba what happened next kila mtu anajua....

Mungu Ibariki Kenya
 
Kenyan Attorney General Amos Wako has called for an independent investigation into vote results that led to President Mwai Kibaki's disputed re-election.
Mr Wako said on national television that "a proper tally of the valid certificates returned and confirmed should be undertaken immediately".

His call came as a planned opposition rally in Nairobi was postponed amid clashes between supporters and police.

More than 300 people have been killed and some 70,000 displaced since Sunday.

The violence was triggered by claims of vote rigging in the 27 December presidential election.


See an aerial map of Nairobi and the city centre
Mr Kibaki on Thursday called for an end to the unrest and said that once that had happened he would be prepared to speak to the opposition.

"I am ready to have dialogue with the concerned parties once the nation is calm and the political temperatures are lowered enough for constructive and productive engagement," Mr Kibaki told journalists at his State House residence in Nairobi.

The EU and US have agreed to push Mr Kibaki and his opposition rival to consider a coalition government, a spokeswoman for the EU's foreign policy chief said after he spoke to the US secretary of state.

Source: http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7169720.stm
 
Raila alishinda uchaguzi wa urais, lakini ameshindwa kuulinda ushindi wake usiporwe. Na hata baada ya kuporwa, ameshindwa kabisa kuurejesha. Na sasa hivi ameshindwa rasmi. Kosa lake ni moja, na nililisema toka mwanzo, kuchelewa. Waswahili husema "chelewa chelewa utamkuta mwana si wako", naye kwa kosa hili, tayari "kamkosa mwana na maji ya moto"! Hiyo rally alitakiwa kuifanya siku ileile alipoapishwa Kibaki, au kesho yake na si zaidi ya hapo. Sasa hivi hamwezi tena, keshachelewa, maana amemsubiri hadi akajiimarisha upya. Sasa hivi nasikitika kusema, Raila atabakia mlalamishi tu, na kina Kibaki watakuwa wanabeza tu kelele zake wakisaidiwa na methali ya "kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji".

Inasikitisha, lakini imeshakuwa hivyo. Poleni sana ndugu zetu.

Hapa umesema ukweli Kithuku na ninashawishika kukubaliana nawe.

Kitu kimoja inabidi ukumbuke hapa ni kuwa, kinachoendelea Kenya sasa hivi ni zaidi ya Raila. Nadhani una taarifa kuwa nyumba ya moi na mali zake kibao za Eldoret zimechomwa moto au kuporwa. Kuna habari kuwa Moi kakimbia nchi.

Kama ilidhaniwa kuwa hii issue ni kati ya wajaluo na wakikuyu, inabidi dunia ijue kuwa sasa hivi imekuwa ni kati ya wananchi dhidi ya manyangau. Kuna wakati moi alidhani kuwa yeye ni mungu na kuwa atalindwa daima na Kalenjin. Kilichotokea ni fundisho kwa hata huyu kibaki asipokuwa makini ataondolewa na kikuyus ingawa sitegemei sana hili kutokea.

Waliotaka Raila ashindwe watadhani kuwa wameshida kwa sasa. Hata kama Raila kesho akifa au akubali yaishe kwa sasa roho ya chuki dhidi ya mafisadi wa kenya imeshapandwa na itakuwa the matter of time b4 yalipuke makubwa zaidi. Tatizo kwa wakikiyu ni kuwa wengi wao itabidi warudi central province kuishi maana kwa sasa hawatakiwi kabisa anywhere. Kama ulisikia bbc juzi nadhani ulimsikia yule bwana mombasa alivyokuwa akisema kuhusu mpango wa vijana wa kuchukua kila kitu chenye uhusiano na kikuyu.

Kazi ipo, huu ni mwanzo tu. Kibaki atadhani kuwa ameshinda mara hii lakini amejenga nchi ambayo yeye na jamii yake wataishi kwa wasiwasi kwa miaka mingi sana ijayo.
 
All of the UK's major tour operators have suspended holidays to Kenya for the next two days, the Federation of Tour Operators has said.
Operators began cancelling flights following Foreign Office advice that people should only take essential journeys to the East African country.

More than 300 people have been killed in Kenya and at least 70,000 driven from their homes since Sunday.

The crisis flared after claims of vote rigging in the presidential election.

The Federation of Tour Operators (FTO) is also assessing the need to make alternative travel arrangements for 7,000 Britons who are already on holiday in Kenya.
 
Masatu si RAILA anae organize watu waue..its people emotinals..yeye kama hawezi kuwazuia. yeye alishatoa KAULI ya kuwataka wafuasi wawe COOL. sina hakika kama katoa kauli yoyote ya KULAANI tukio la kuwawa watu KANISANI, kama hakufanya..pls wale watu wakaribu wamwambie.
Viongozi wa CUF wanastahili pongezi au Nature ya watanzania hawataki magomvi kwani kwa chaguzi zote za ZNZ situation zote zilikuwa mbaya..its Good today Raila amezuia yale maandamano kwani Police watiifu kwa KIBAKI walishajiandaa kuongeza namba za maiti na mahututi...Sijui Role wa JK aliepo ARUSHA alau kwenda ku-mediate...
 
Kenya violence unsettles markets

There are fears that Kenya's economy may be derailed by the violence
Violent protests against the outcome of Kenya's presidential election have caused a sell-off in the country's currency and sent key stocks falling.
The Kenyan shilling dropped 7% against the US dollar after the opening of the foreign exchange market was delayed.

Kenya's stock exchange also opened late, while the world's biggest tea auction, held weekly in the port city of Mombasa, has been postponed.

President Mwai Kibaki has been accused of vote-rigging to win the election.

Violence has broken out across Kenya with at least 250 people killed as Mr Kibaki's supporters have clashed with those of opposition leader Raila Odinga.
 
Mimi namshangaa sana huyu Kenyan - Tanzanian kwa kum support Raila katika njama zake za kuigawa Kenya. Kibaki anaweza kuwa mkabila lakini huyu Raila ni muuaji ana organise watu wake waenda kuua wakikuyu kanisani! jamani hata Kanisani? Hii ni hatari sana, we are carried away na hizi events zinazojiri Kenya na lakini hatari iliyopo mbele yetu ni Kenya wanaweza kumtoa mkabila Kibaki na kumuingiza muuaji Raila.

Huu ni uongo mkubwa sana na inabidi upingwe kwa nguvu zote hapa JF. Raila na wajaluo kwa ujumla hawakuwa marafiki wa kalenjin kwa sababu ya moi kuhusika na kifo cha ouko. Wakati wa Moi, watu wengi wa kalenjin walikuwa wanatumia lugha ya kashfa dhidi ya waluo kuwa hawajatahiri kama wakikuyu wanavyofanya sasa hivi. urafiki wa wajaluo na wakalenjin umeanza juzi tu baada ya wote kugundua kuwa wanacommon enemy - few people in kikuyu tribe.

Mtu mwenye influence kubwa sana kalenjin sasa hivi ni Ruto na the guy is articulate kama umeona news conference yake. Haya mambo ya kumuhusisha Raila na kilichotokea Eldoret ambapo vijana wa kikalenjini waliua kikuyu ni makosa na propaganda za western media. Kama ni ODM wangelaumiwa basi watu wangemlaumu Ruto lakini hii ni uongo kwa sababu bila machinery ya GOVT, There is no way mtu wa upinzani ambaye yuko nairobi kama Raila na Ruto sasa hivi akaongoza mauaji yanayoendelea huko mikoani.

Raila kama unaona aliyekunyima urais ni Kibaki chonde chonde waache in peace wakikuyu kuendelea kulazimisha wauawe hakukusaidii, hivi utakapo ingia huko Ikulu utatawala waluo na wakalenjin tu?

Raila amepigiwa kura na makabila zaidi ya 40 ya kenya. Nenda kasome facts zako vizuri. Una taarifa kuwa waliokufa kwa kuuwawa na polisi ni nusu ya wote waliokufa kenya sasa hivi?

Kenyan - Tanzanian naomba nikupe polite ombi pamoja na hamasa na ufurukutwa wako kwa Raila nakuhakikishia huyu mtu hana heri na Kenya, mwanzoni hata mimi nilikuwa nina sympathize nae lakini as the days goes on the man is showing his true colour hawafai wakenya na hatufai wa east africa.

Unasema the same thing alichosema Museven jana wakati akihojiwa kuhusu uamuzi wake wa kumuunga mkono Kibaki

All said and done si support foul alizofanya Kibaki (if any) lakini ndugu zangu wa Kenya yasije yakawakuta ya Wazambia walipomtupia virago mzee Kaunda na kumuingiza Chiluba what happened next kila mtu anajua....

Mungu Ibariki Kenya

Wewe unasapoti mafisadi Tanzania kwa hiyo si ajabu ukisapoti mafisadi wa Kenya. Soon utasema kuwa Mugabe ni bora huko Zimbabwe kuliko wanaupinzani!
 
Pamoja na maovu yanayotokana na vurugu, maasi na fujo za huu uchaguzi wa Kenya, Kibaki amefanya kitu kimoja kikubwa (bila yeye kujua) na kitabadili mfumo na mtazamo wa ki-siasa wa Kenya milele.

Bila kujua, Kibaki ameweka doa kwa kila mwanasiasa wa Central (GEMA) na uzao wao. Kila mwanasiasa wa aina hiyo atapata wakati mgumu sana kupata ushindi halali au haramu katika ngazi za kitaifa kutokana na perception kuwa ushindi huo ni matokeo ya wizi wa kura (kweli au la).

Kwa mantiki hiyo, uwezekano wa Uhuru Kenyatta kuingia ikulu 2012, kama ilivyokuwa inazungumzwa, ni sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano.
 
Back
Top Bottom