Ukweli ni huu.
-Kiujumla huduma za Afya za Tanzania kwa sehemu kubwa ziko katika standards&cost affordable kulingana na ngazi husika ikiwa utalinganisha na Kenya.
-Ni rahisi zaidi kwa mkenya kuvuka boda kufuata matibabu Tz kuliko mtanzania kuvuka boda kwenda Kenya kufuata matibabu kwa sababu za Ukarimu (uko zaidi Tz), Urafiki huduma(uko zaidi Tz), unafuu (uko zaidi Tz) na uhakika (uko zaidi Tz). Siasa za chuki za Magufuli zilivuruga hii situation kwa sehemu.
-Hospitali nyingi za Kenya za pembezoni na mashambani zimepewa hadhi kama hospitali za rufaa lakini kiuhalisia hazina hadhi hiyo, na ukiweza kuzileta Tz hadhi yake ni sawa na hospitali za wilaya au hadhi ya vituo vya afya vilivyoboreshwa. Wakenya ni watu wanaopenda kujiboost na kubold mambo yao hata kama ni mambo madogo sana au madhaifu, lengo lao hasa ni kupata sifa au hadhi ya juu.
-Nairobi kuna hospitali nzuri na za kisasa sana (sawa na Dar au zaidi ya Dar), shida kubwa ni gharama yake kuwa kubwa sana ili kuweza kutibiwa pale. Wakenya wa hali ya chini na kati wanaona ni nafuu kukimbilia Tanzania kuja kutibiwa. Tiba ambayo ingemgharimu shilingi laki Tano hapa Tanzania basi Tiba hiyo hiyo angeipata Nairobi kwa kiasi kisichopungua Milioni Tano.
NOTE
Binafsi sioni kama ni utu, ubinadamu au heshima kumsengenya kwa utaifa wake mgonjwa anayetoka nchi yake kuja kutafuta tiba nchi nyingine ya jirani, ama kudhihaki huduma za tiba za nchi nyingine kisa tu kuna wagonjwa wanakimbia hiyo nchi kufuata tiba nchi nyingine. Haya ni mambo ya kutegemeana na sio kushindana kiushabiki. Uhai na Afya ya mtu ni neema za mwenyezi Mungu, ukipata fursa ya kuboresha uhai au afya ya mtu, basi umrudishie muumba utukufu huo.