Kenya ilikosewa, maendeleo yake yana limitations!

Kenya ilikosewa, maendeleo yake yana limitations!

Hata waswahili walisema mwacha mila ni mtumwa, na mwacha asili? I celebrate my language, i celebrate my tribe, i celebrate our diversity, i shun the negative ethnicity brought about by one Raila Odinga to show how divided we are. Remove Rao from the equation and the perceived divisions are minor. How many times have i been in a place where the language they speak is alien but never received any hate? Why is the hate only when there are elections? We have our minor divisions but 41 against 1 was the game changer that hopefully will not recur. A nation doesn't have to be monolingual to thrive; Somalia is one tribe, why has it experienced warfare for decades?

You cant be real ..blaming Raila for TRIBALISM??? Remember the one guy CALLED JOMO KENYATTA..HE STARTED IT ALL
 
Acha kuwaombea wenzako mabaya, Wakenya ni Ndugu zetu. Mimi elimu ya msingi nimesoma Kenya na kubahati kushi huko kwa kuwa nina ndugu huko, mipaka ya Kikoloni iligawa Kenya na Tanzania bila kujali jamii zilizokuwa mipakani zinavyohusiana, unashangaa watu wa familia (Babu mmoja) walihawanywa wengine wako Tanzania na wengine wako Kenya, shughuli za kijamii katika shida na raha kama vile arusi, misiba na n.k tuko pamoja. Ninachofahamu ni kwamba nchi ya Kenya iko mbele kimaendeleo, nenda Nairobi uone watu walivyo na pesa, majumba yanvavyojenga, angalia watu wanavyotembea kwa haraka barabarani wakiwa katika maeneo yao ya kazi; rudi hapo Dar uone mnavyotembea kizembe, mnavyopoteza muda kucheza pool siku nzima, hala unarudi kula nyumbani bila kuzalisha kitu !! Wacha wewe kuombea wenzako mabaya, rekebisha ya kwako. Sawa ni kweli hao watu wana vituo vya runinga vya kikabila, hata shuleni tulikuwa tunafundishwa lugha ya Mama katika madarasa ya awali, je, unawazidi nini katika maendeleo ??


Hakuna mahali nilipowaombea vibaya, kwanza ni kinyume chake, mimi girlfriend wangu anatoka Kenya hivyo siwezi kuwaombea mabaya ila nimesema hali halisi kwa yale niliyoyaona huko, kwamba nchi ya Kenya ina limitations yaani kuna mahali watafika watagota kama vile Nigeria, AK au hata Uganda wataendelea lkn watafika mahali watakwama na hawataweza kwenda mbele na hili siyo geni hapa Duniani hutokea Dunia nzima nchi zote zilizoshindwa kujenga Taifa hufikia mahali huanza kubomoa nyumba na kugawana fito!

Sioni ni jinsi gani nchi ya Kenya kwa hali jinsi ilivyo inaweza kubakia jinsi ilivyo kwa miaka 50 ijayo!
 
Rich Kenyans !! Bado sijaona ni kwa nini tunawalaum ndugu zetu Wakenya kwa kiasi hiki, mimi binafsi ni ndugu zangu Kenya na nimesomea Kenya elimu ya Msingi, hawa watu wana uzalendo sana na nchi yao kitu ambacho ni tofauti na nchi nyingine. Ukiigusa Kenya, wanaondoa tofauti zao na kukushambulia wewe, sio rahisi hicho kitu kinachohusu ukabila kikavunja umoja wao katika ngazi ya Kimataifa, angalia hata michezoni - riadha n.k wanashiriki kama Kenya sio kabila wala Ukanda fulani, angalia maendeleo yao hata barabara, watu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoka Tz wamekuwa wakitumia barabara za kenya muda mrefu kwenda Nairobi, angalia kule Rorya na Tarime - Cement, mabati, sukari, nondo, sabuni mafuta ya kupikia vyote vyatoka Kenya. Watanzania ndio wanabaguana nje ya nchi, hao wakenya wakiwa nje ya nchi wanavaa nguo zenye rangi ya bendera ya nchi yao, ni vizuri Watz tukajifunza mazuri kutoka kwao kama vile kufanya kazi kwa bidii, kutumia fursa yoyote inayojitokeza nje ya nchi na kurudi kuwekeza kwetu na kuipenda nchi yetu, yale mabaya tuwaachie wayashughulike wenyewe, maana dawa yake wanayo wenyewe.


Na ndiyo maana kama umenielewa vizuri nimesema kwamba maendeleo ya Kenya yana limitations, ni kama vile India huwezi kufananisha na Uchina, kwa maana maendeleo ya India pia yana limitation kuna mahali hawawezi kuvuka kwa maana tofauti baina ya jamii iishiyo India ni kubwa sana, sasa India pia ni matokeo ya British Raj ambapo walilazimisha jamii mbali mbali ambazo hazikuwa na uhusiano wowote ule kabla kuishi pmj hivyo ni swala la muda kabla India hawajaanza kugawana fito, hilo hata Kenya haliepukiki!

Fikiria tu hivi sasa Viongozi wa Kenya wanasema kwamba kuwe na Uraisi wa kuzunguka, yaani kipindi hiki kundi hili, kinachofwata kundi lingine sasa uliona wapi mfumo wa namna hii? Na unajua ni kipi kinafuata kama watu wanataka nchi yao iendeshwe hivyo?

Kitakachofwatia ni kugawana fito tu tena na sasa wamerahisisha wenyewe wameleta county!
 
Hakuna mahali nilipowaombea vibaya, kwanza ni kinyume chake, mimi girlfriend anatoka Kenya hivyo siwezi kuwaombea mabaya ila nimesema hali halisi kwa yale niliyoyaona huko, kwamba nchi ya Kenya ina limitations yaani kuna mahali watafika watagota kama vile Nigeria, AK au hata Uganda wataendela lkn watafika mahali watakwamba na hawataweza kwenda mbele na hili siya geni hapa Duniani hutokea Dunia nzima nchi zote zilizoshindwa kujenga Taifa hufikia mahali huanza kubomoa nyumba na kugawana fito!

Sioni ni jinsi gani nchi ya Kenya kwa hali jinsi ilivyo inaweza kubakia jinsi ilivyo kwa miaka 50 ijayo!
Huko ndo kuwaombea vinaya nilikoona, unaposema kuna mahala watafika watagota, hayo ndo mabaya yenyewe !!! Hata kama tunfahamu kwamba hakuna binadamu atayeishi milele, lakini huwa hatumwambii mtu kuwa utaishi kwa jumla ya miaka 80 tu, halafu utakufa tunamwombea aishi milele hata kama tunajua kuwa hawezi ishi milele. Sasa na wewe hao wakwe zako watarajiwa, usiwaombee kuwa ifafika mahali maendeleo yao yasimame au waporomoke. Kimbe hata kuoa hujaoa, bado hujui maisha, unakula kwa wazazi.
 
You had first painted Raila as a the poster-child of tribalism in in Kenya in your comment here, in support of Dhuks senseless comment

And now, upon being confronted over ur argument, u turn around to state that u meant that Raila is the man who creates crises in Kenya, which he capitalizes on for his political advancements. Do u then realize the contradictions in your arguments? Just bcos he spawns all these crises for his political ends, does that make him a tribalist? Does he preach hatred btwn tribes? Those two are very different things.

Raila is not the epitome of tribalism in Kenya, it exists in all us, and all our leaders merely capitalize on them for their own goals in politics. It is a problem that had begun long before Raila had indeed gained any foothold in politics.

Raila has no hand in Kikuyu Kalenjin enmity over land or Kikuyus vs masais or the cushites vs bantus, luo vs Kalenjins, or the bitter rivalries btwn tribes in the coastal regions etc. This is a problem we Kenyans must face and resolve with an open mind, not by laying the blame on one individual or group.

Mkuu Iconoclastes, achana na huyu jamaa. I know people like him. They can't and won't change. Let's move on with the thread.
 
Hata mie nmeshangaa sana kauli yake!....jamani tujirekebishe, mleta mada yupo sahihi.
Hakuna kitu kiitwacho positive ethnicity, waingereza walilitumia hili kututawala (tribesmen in village reserves)
Ethnic identity haina maana in an advanced technological modern world.
Nchi kama Marekani watu wana asilia tofauti lakini lugha moja.....isipokuwa tu kuliko tengwa kwa red indian natives / tribal folk wanaodhaniwa kuwa primitives/savages.
If you identify yourself with TRIBE in these era then you are simply unevolved or primitive.
Nashangaa mpaka mna televisheni za kilugha khaah!
Hakuna kinachoniudhi ndani ya nchi yangu kama hili.
Ni dhahiri mwanzilishi wa taifa letu,Mhe. hayati Jomo alinoa kwenye sera hii,mheshimiwa Nyerere/hayati alitinga goli 100% score) kwenye swala hili katika uogozi wa taifa lake.
Nashangaa pia ni kwa nini hoja la kufutilia mbali vikabila na vijilugha havijawahi kujadiliwa bungeni.
Raisi wa Marekani mhe. Obama alipowahutubia wakenya wakati wa ziara yake Kenya alisema hivi........"politics of ethnicity is doomed to fail a nation"
Badala ya kufukia vichwa vyetu , huku tukijidanganya kuwa mambo shwari ni upumbavu kama vile leo hii ubaguzi wa rangi unatokota Marekani na kutishia machafuko ya ndani kwa ndani nchini humo.
Ni kweli tutaungana tukiwa na adui wa nje , hilo lipo kwenye taifa lolote lile, lakini adui wa nje hasipokuwepo basi tutajitafuna wenyewe ndani kwa ndani kama ilivyo Somalia......adui wa ndani kwa ndani ni hatari kuliko wa nje.
Nawasilisha!
 
Sijasema Kuwa Raila is the sole cause of Tribalism. Nimesema kuwa Tribalism ni ugonjwa wa viongozi na Raila ndiye epitome of that doctrine.

Tatizo la Raila ni kuwa yeye huwa na politics of Brinkmanship. Anapenda nchi iwe in a crisis wakati wote ndiposa ajifanye kiongozi. Hata wetangula naye anakaa keshaanza upumbavu huo.

Hahahaha!....eti Raila ndiye chanzo.....hahahahahaha!
Sijui ni wapi Odinga hukaa vikao na vizee vya kikikuyu GEMA akawaongelesha kilugha eti wawe wakabila.....umenichekesha sana, kauli kama hizi zakudhalilisha mwenyewe.
The person that laid that nations foundations takes the blame squarely for shoddy work and lack of vision on the said matter!
 
Where is MK254 aje hapa .....comfront these issues!....tuache kutoroka matatizo yetu!
 
You cant be real ..blaming Raila for TRIBALISM??? Remember the one guy CALLED JOMO KENYATTA..HE STARTED IT ALL
I am very real, we always had our differences but tell me when they were used so efficiently to divide us. We always looked at the ethnic composition of Moi and Kibaki cabinet but tell me when they were used on a national scale to vilify a community. Tell me of any uprising to wards the Kalenjin community during Moi era or Kenyattas rule against the Kikuyu. You should look at the composition of the Kenyan tribes and start seeing the fallacy of 41 against 1
 
Kwanza kabisa, natanguliza kwa kusema huyu mleta mada mzushi na amekosolewa mara nyingi humu JF kwa kauli zake. Anajiachilia na kuropokwa na huo ushambuliaji wake linamwacha bila beki, wakati wa counter attack. ndiposa anafungwa mabao utadhani yeye aston villa wa JF. Na hapa kwenye hii mada, sio tofauti. Labda atuelezee haya madai:

1. Anansema Mombasa pekee yake ndo lina historia ya utaifa kabla ya enzi ya ukoloni. Je, anayafahamu mataifa yaliyotangulia Kenya kwenye eneo liitwalo Kenya?

2. Anasema kuwepo kwa vikundi vya kikabila ndo changamoto namba 1 kwenye harakati za maendeleo nchini Kenya. Nafurahi kusikia hatimaye umekubali vitu humu Kenya ni vya kusonga mbele na kwa kasi. Je, kuyaondoa ndo dawa lake?? Utaifanya vipi?? Na kuwa na asili ya kikabila ni kitu kibaya? Nani kakwambia eti huo mfumo wenu wa kudunisha lugha na tamaduni zenu ni wa kuigwa barani??

3. Fafanua haya "limitations" unayodai yatatufika. Hivi unadhani maendeleo ni "process" ama ni"event".

4.Usitudanganye na ya girlfriend wako ni mkenya bila kutupa uhakikisho. Kama shemeji mtarajiwa, unajipa ripoti mbofu. Kwa maisha yangu nimegunda kitu kimoja " penye ngombe wanapatikana kupe, japo maadui". Nadhani ulitangulia na hii ya mchumba wako ili uonekane rafiki wetu, na ukweli lipo wazi haswa baada ya ule uongo uliotuwekea kuhusu yule dada mwanariadha wa Ethiopia mwenye uraia wa uturuki.

Kazi kwako Barbarosa
 
Hakuna mahali nilipowaombea vibaya, kwanza ni kinyume chake, mimi girlfriend wangu anatoka Kenya hivyo siwezi kuwaombea mabaya ila nimesema hali halisi kwa yale niliyoyaona huko, kwamba nchi ya Kenya ina limitations yaani kuna mahali watafika watagota kama vile Nigeria, AK au hata Uganda wataendelea lkn watafika mahali watakwama na hawataweza kwenda mbele na hili siyo geni hapa Duniani hutokea Dunia nzima nchi zote zilizoshindwa kujenga Taifa hufikia mahali huanza kubomoa nyumba na kugawana fito!

Sioni ni jinsi gani nchi ya Kenya kwa hali jinsi ilivyo inaweza kubakia jinsi ilivyo kwa miaka 50 ijayo!
My ans can be summarized to 3 letters:- USA.

It can be elongated to :- red Indians have not only been discriminated against, they've been called aliens in their own land and almost eliminated to extinction, blacks and Latinos are treated very violently by the police, Asians are seen there as if they're attempting to take everything from whites and lastly whites are called the most racist and viewed as if they want to control and own virtually everything. In short, it is one of the most divided but actually among the most successful nations currently

I am very real, we always had our differences but tell me when they were used so efficiently to divide us. We always looked at the ethnic composition of Moi and Kibaki cabinet but tell me when they were used on a national scale to vilify a community. Tell me of any uprising to wards the Kalenjin community during Moi era or Kenyattas rule against the Kikuyu. You should look at the composition of the Kenyan tribes and start seeing the fallacy of 41 against 1
I'll give you examples, kenyatta's (snr) violent réception in kisumu led to the 1st tribal discrimination between Luos and kikuyus. Moi as a minow and vp was openly derided by the likes of njonjo and after he clinched the seat, he went on a revenge mission by taking them out of power, marking the start of kikuyu-kalenjin beef it is these 2 enmities that culminated to the 2007 tragedy. Actions of Kibaki, Raila, etc to not budge in their views just worsened things
 
Hivyo nchi ya Kenya itajitahidi kupiga hatua kubwa kimaendeleo inavyotaka lkn kuna limitations, yaani kuna mahali hawawezi kuvuka, nitatoa mfano mdogo sana ni kawaida kwa kiongozi wa Kenya kusema ,,my people" akimaanisha watu wa ethnic group yake na siyo Taifa la Kenya, kitu ambacho Tanzania sijawahi kusikia Kiongozi akisema my people, kwa kawaida sisi tukisema my people tunamaansha Watanzania!

Hivyo kama ilivyo pia nchi ya Nigeria ambapo kwa mfano wa Igbo wanakwambia wako tofauti na Wayoruba na hawawezi kuishi pmj kwa maana hakuna kinachowaunganisha, nchi ya Kenya ni ngumu sana kuona huko mbele itasimama vp kwa maana matatizo waliyo nayo ni makubwa sana chukulia tu mfano hapa Tanzania Vyuo vikuu tuna wawakiishi wa vyama vya Kisiasa labda hata Mkoa wanayotoka lkn Kenya kuna wawakilishi wa ethnic groups vyuoni, kuna TV stations za ethnics groups, kuna Radio stations za ethnics group, kuna mpaka Hospital ingawaje siyo official lkn unaweza kusema ni za kiethnics mpaka Benki, ukienda restaurant kuna Migahawa ya kiethnics, bar ha kiethnics n.k sasa unawezaje kuondoa tofauti hizi zote?
Kinachonishangaza, Kenya na Nigeria wako mbele yetu. Kinachonishangaza, tuko bize kufanya research juu ya maisha ya Wakenya tukiacha ya kwetu.

Mimi katika tafakuri yangu, ukimsikia kiongozi wa Tanzania anasema 'watu wangu' huyu anamaanisha 'familia yake'. Ndio maana kuna watu wamejazana kwenye taasisi nyeti za umma ilhali wengine wasio na surname za kufanana nao wanasukuma mkokoteni kila uchao.

Saa nyingine tunakosa ushindani ndio maana tunabweteka. Tutakaa na kusema 'aah, Wahaya bwana wanapenda sana elimu'...pambaf, badala ya kushindana nao tunawapongeza, SHIT! Hatuna wivu, tunabweteka. Haya majamaa yanasonga mbele sababu yanaoneana wivu. Hebu tujadili mambo yetu, Kenya Kenya, so what! Acha mihemko wewe Mamarosa
 
Hata waswahili walisema mwacha mila ni mtumwa, na mwacha asili? I celebrate my language, i celebrate my tribe, i celebrate our diversity, i shun the negative ethnicity brought about by one Raila Odinga to show how divided we are. Remove Rao from the equation and the perceived divisions are minor. How many times have i been in a place where the language they speak is alien but never received any hate? Why is the hate only when there are elections? We have our minor divisions but 41 against 1 was the game changer that hopefully will not recur. A nation doesn't have to be monolingual to thrive; Somalia is one tribe, why has it experienced warfare for decades?
Interesting... So before Raila was born Kenya wasnt tribal? Very weird.😵
 
Back
Top Bottom