Ni ukweli kabisa, kilichoipumbaza Tanzania ni uhuru wa kupewa bila kutumia nguvu
Kenya na nchi nyingine zilipigania uhuru kwa nguvu hata kama Tanzania ilienda kusaidia kijeshi lakini hakuna vita vya kidai uhuru Tanzania mwenye historia alete hapa.
Machifu ndio walikua wanapigana na sio Tanzania kwa ujumla, watz tuache ushabiki mandazi, ndio maana mpaka leo CCM inatuona mabumbunda na hatuna cha kuwafanya
Watu wenye fikra kuwa Uhuru wa Tanganyika ulipatikana bila ya kumwaga damu, ni mazalia ya kizazi kipya ambacho kimejazwa historia potofu iliyotungwana jopo lililoongozwa na Pius Msekwa, baada ya Uhuru kwa kuagizwa kufanya hivyo na TANU, kwa madai kuwa historia iliyokuwepo iliandikwa na wakoloni kwa mtazamo wa kikoloni.
Kwa bahati mbaya, jopo hilo lilifanya jinai ya kusadikisha watu kuwa uhuru wa Tanganyika ulitokana na harakati za kudai uhuru zilizofanywa na TANU, chini ya Mwalimu Julius Nyerere, na kwamba haukupatikana kwa kumwaga damu.
Kwa utotofu huo wa maksudi Watanzania wa kizazi cha sasa wanasadikishwa, tena kwa maksudi, kuwa harakati za kujinasua na ukoloni Tanganyika, hazikuanza tangu zama za akina Mtemi Mirambo wa Unyanyembe, Mangi Mweri, Chief Mkwawa, Vita vya majimaji, kutaja kwa uchache!
Harakati hizo ambazo, wakoloni waliziita, 'native resistance or rebellion' zilisababisha umwagaji mkubwa wa damu za mashujaa wetu wazalendo, licha ya andiko rasmi la historia kutotambua umuhimu wa michango ya mashujaa huo, katika harakati za kupigania uhuru wa kujitawala, hata kama kila mwaka tunawakumbuka na kuadhimisha siku ya Mashujaa.
Bado tunahitaji wanahistoria makini waandike histori ya Tanzania anayoakisi harakati za kupigania uhuru tangu enzi za akina Abushiri, Chifu Chaburuma, nk, hadi enzi za T.A.A na TANU iliyotamatisha mchakato huo.