Kenya ilipopinduliwa mwaka 1982, Nyerere aliokoa Taifa lililomchukia

Na unajua pia na sisi Nchi yetu ilifanyiwa jaribio la mapinduzi na hao wanamapinduzi wakakimbilia Kenya ,lakini Kenya hiii hii nayo ikawakabidhi kwa Tanzania unalijua hilo?
Mkuu ndio sababu ya Nyerere kuwarudisha wakenya hao.
Wako watanzania waliokuwa wametoroka maximum security prison Ukonga wakatolokea Kenya. Hao watanzania walihusika katika jaribio la kutaka kumuua Raisi Nyerere kupindua serikali yake.
Kwa hiyo ilikuwa exchange ya watu waliotaka kupindua Moi na Nyerere.
 
Umeandika tu lakini bila kufahamu kwamba wale wanajeshi wa anga wa Kenya walioteka nyara ndege na kuja nayo Tanzania Hezekiah Ochuka na Pancras Oteyo Okumu walirejeshwa nchini kwao Kenya kwa makubaliano maalum kati ya aliyekuwa rais wa Kenya marehemu Daniel arap Moi na Julius Nyerere wa Tanzania.

Kipindi hicho ndio Nyerere naye alinusurika kupinduliwa na wanajeshi wa JWTZ na baada ya watuhumiwa kuwekwa kwenye gereza la Keko na baadhi yao walifanikiwa kutorokea Kenya.

Ndipo makubaliano yalipofanyika kati ya Tanzania na Kenya na kupelekea watoro wa Tanzania akina marehemu Mac Ghee na wenzake kurejeshwa Tanzania kutoka Kenya na wale wa Kenya kurejeshwa Kenya kutoka Tanzania.

Hivyo kama mtu anatoa simulizi kinyume na hili nililolitoa hapa basi ijulikane wazi kwamba ni upotoshaji mkubwa hivyo sio kweli kabisa kwamba Nyerere aliisaidia Kenya, ilikuwa ni nipe nikupe approach.
 
Ilipofika Agosti 1 mwaka 1982, alfajiri ilianza kwa kimya kilichojaa tafakari ya taifa. Lakini katika kiza cha mapambazuko, lilizuka tone la radi la kisiasa, jaribio la kumpindua Rais Daniel arap Moi.

Kiongozi wa mpango huu wa kisasi hakuwa jenerali wala kamanda wa juu, bali askari wa hadhi ya chini, Hezekiah Rabala Ochuka, mwanajeshi wa Jeshi la Anga.

Kwa sauti ya uthubutu na nafsi ya kuandamwa na njozi za utawala, Ochuka na kundi dogo la wanajeshi waliivamia redio ya taifa na kutangaza kuikalia serikali.

Kwa masaa sita, Kenya ilikuwa chini ya kivuli cha mapinduzi. Lakini kama kivuli cha jioni kisicho na mwanga wa kweli, mapinduzi hayo yalizimwa haraka na majeshi halali.

Ndipo Ochuka, aliyekuwa sasa adui wa dola, akakimbilia mji wa Dar es Salaam kwa siri, akivuka mipaka ya Uganda akiwa na tumaini la hifadhi.

Huko Tanzania, alikumbana na ukimya wa busara ya uongozi.

Mwalimu Julius Nyerere, kiongozi wa nchi ya kijamaa, alipokea simu kutoka kwa Rais Moi, simu iliyojaa maumivu ya usaliti na hofu ya maangamizi.

“Yuko kwenu,” alisema Moi, “ametorokea Dar es Salaam.”
“Ni nani huyo?” akauliza Nyerere kwa sauti ya kiongozi anayefahamu uzito wa maneno.
“Ezekia Wachaura Ochuka,” akajibu Moi kwa sauti ya uchovu, sauti ya mtu aliyeokoka janga la kisiasa.

Nyerere, licha ya kuwa Tanzania na Kenya hazikuwa na mahusiano mazuri katika miaka ya sabini hadi themanini kutokana na upinzani wa mifumo yaani ubepali na ujamaa, hakuona busara ya kukumbatia waasi.

Kwa msingi wa mshikamano wa taifa na amani ya kanda, alikataa kumpa hifadhi Ochuka.

Ni ajabu sana leo hii kuwaona ndugu zetu Wakenya wakiwakumbatia wanaharakati wanaomtukana Rais wetu wa nchi na kueneza chuki, uzushi na uzandiki dhidi yake kwa mataifa mengine.

Ochuka alikabidhiwa rasmi kwa Kenya akisindikizwa na upepo wa kisasi wa dola yake.

Alihukumiwa na hatimaye kunyongwa mwaka 1987. Akafa akiwa na hadhi ya pekee, Rais wa Kenya wa masaa sita tu.

Simulizi yake sasa huishi kama kivuli kinachopita katika historia ya Afrika Mashariki, kielelezo cha jinsi mamlaka, ndoto na usaliti huweza kumtupa mwanadamu kutoka utukufu wa ndoto hadi kwenye kaburi la kusahaulika.

Hili ndilo simulizi la mtu aliyetamani kutawala kwa nguvu lakini akabaki kuwa somo la historia, somo la kisasi cha dola na busara ya viongozi waliokataa kugeuza udugu wa taifa kuwa shimo la hifadhi ya waasi.

Rais wa Kenya anapaswa kurudi maktaba ajifunze historia vizuri kabla ya kujifanya mwanasiasa sana kwa kuunga mkono Gen Z wa Kenya kumtukana na kuchafua heshima ya Rais wa Tanzania.

Kama alipinduliwa Daniel Moi kwa masaa sita licha ya kuwa shababi, sembuse huyu Kasongo mdhaifu.

Tanzania huwa tunaua nyoka lakini hatutupi fimbo kwa sababu nyoka huzaliana.
Ngoja nikujibu Ochuka alipewa hifadhi ya kisiasa Tanzania ila mwaka 1983,wanajeshi wetu walipotaka kupindua Serikali yetu na baadhi yao kukimbilia Kenya basi ikabidi yafanyike mazungumzo ya kubadilishana wafungwa ndio ikabidi Moi awakabidhi wakina Luten Eugen Maganga na wenzake na Nyerere awakabidhi wakenya waliokimbilia Tanzania
 
Unafaidika nini na kudanganya watu?

Story yako imekaa upande mmoja sababu hutaki kukubali yalifikiwa makubaliano ya kubadilishana waliotaka kumpindua Moi 1982 na waliotaka kumpindua Nyerere 1983 ,Kina Ochuka walibadilishwa na Hatty McGhee waliokuwa wamepata hifadhi kwnye nchi husika.
 
Point Of Correction: Ochuka na Akumu walirudishwa Kenya kupitia Namanga November 11, 1983. bila ya knowledge ya Nyerere.. Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Moringe Sokoine (ambae by that time alikuwa anafanya kazi nyingi za raisi) alitoa amri warudishwe Kenya.. Nyerere alikuja kustuka baadae baada ya Jumuiya za kimataifa ikiwa pamoja na mashirika ya wakimbizi na haki za binadamu zilivyoanza kupiga kelele.. Ochuka alifariki kwa kunyongwa tarehe 9 July 1987 akiwa na miaka 33.. Tukio alilolifanya Moringe lilirudisha mahusiano rasmi kati ya kenya na Tanzania, na mipaka ikafunguliwa rasmi..
Sidhani kama ilifanyika bila idhini ya Nyerere, indeed,amri ya Nyerere.
Pale nadhani lilikuwepo carelessness.
Mtu kupata political asylum inapaswa atulizane,siyo aanze kuwazomea kule alikotoka.
 
Ilipofika Agosti 1 mwaka 1982, alfajiri ilianza kwa kimya kilichojaa tafakari ya taifa. Lakini katika kiza cha mapambazuko, lilizuka tone la radi la kisiasa, jaribio la kumpindua Rais Daniel arap Moi.

Kiongozi wa mpango huu wa kisasi hakuwa jenerali wala kamanda wa juu, bali askari wa hadhi ya chini, Hezekiah Rabala Ochuka, mwanajeshi wa Jeshi la Anga.

Kwa sauti ya uthubutu na nafsi ya kuandamwa na njozi za utawala, Ochuka na kundi dogo la wanajeshi waliivamia redio ya taifa na kutangaza kuikalia serikali.

Kwa masaa sita, Kenya ilikuwa chini ya kivuli cha mapinduzi. Lakini kama kivuli cha jioni kisicho na mwanga wa kweli, mapinduzi hayo yalizimwa haraka na majeshi halali.

Ndipo Ochuka, aliyekuwa sasa adui wa dola, akakimbilia mji wa Dar es Salaam kwa siri, akivuka mipaka ya Uganda akiwa na tumaini la hifadhi.

Huko Tanzania, alikumbana na ukimya wa busara ya uongozi.

Mwalimu Julius Nyerere, kiongozi wa nchi ya kijamaa, alipokea simu kutoka kwa Rais Moi, simu iliyojaa maumivu ya usaliti na hofu ya maangamizi.

“Yuko kwenu,” alisema Moi, “ametorokea Dar es Salaam.”
“Ni nani huyo?” akauliza Nyerere kwa sauti ya kiongozi anayefahamu uzito wa maneno.
“Ezekia Wachaura Ochuka,” akajibu Moi kwa sauti ya uchovu, sauti ya mtu aliyeokoka janga la kisiasa.

Nyerere, licha ya kuwa Tanzania na Kenya hazikuwa na mahusiano mazuri katika miaka ya sabini hadi themanini kutokana na upinzani wa mifumo yaani ubepali na ujamaa, hakuona busara ya kukumbatia waasi.

Kwa msingi wa mshikamano wa taifa na amani ya kanda, alikataa kumpa hifadhi Ochuka.

Ni ajabu sana leo hii kuwaona ndugu zetu Wakenya wakiwakumbatia wanaharakati wanaomtukana Rais wetu wa nchi na kueneza chuki, uzushi na uzandiki dhidi yake kwa mataifa mengine.

Ochuka alikabidhiwa rasmi kwa Kenya akisindikizwa na upepo wa kisasi wa dola yake.

Alihukumiwa na hatimaye kunyongwa mwaka 1987. Akafa akiwa na hadhi ya pekee, Rais wa Kenya wa masaa sita tu.

Simulizi yake sasa huishi kama kivuli kinachopita katika historia ya Afrika Mashariki, kielelezo cha jinsi mamlaka, ndoto na usaliti huweza kumtupa mwanadamu kutoka utukufu wa ndoto hadi kwenye kaburi la kusahaulika.

Hili ndilo simulizi la mtu aliyetamani kutawala kwa nguvu lakini akabaki kuwa somo la historia, somo la kisasi cha dola na busara ya viongozi waliokataa kugeuza udugu wa taifa kuwa shimo la hifadhi ya waasi.

Rais wa Kenya anapaswa kurudi maktaba ajifunze historia vizuri kabla ya kujifanya mwanasiasa sana kwa kuunga mkono Gen Z wa Kenya kumtukana na kuchafua heshima ya Rais wa Tanzania.

Kama alipinduliwa Daniel Moi kwa masaa sita licha ya kuwa shababi, sembuse huyu Kasongo mdhaifu.

Tanzania huwa tunaua nyoka lakini hatutupi fimbo kwa sababu nyoka huzaliana.
Ila leo Wagambia wametulipizia kisasi cha kumdahalilisha Zuchu wetu! Ahsante sana Gambia!!
 
Back
Top Bottom