Kenya ilipopinduliwa mwaka 1982, Nyerere aliokoa Taifa lililomchukia

Na unajua pia na sisi Nchi yetu ilifanyiwa jaribio la mapinduzi na hao wanamapinduzi wakakimbilia Kenya ,lakini Kenya hiii hii nayo ikawakabidhi kwa Tanzania unalijua hilo?
Mkuu ndio sababu ya Nyerere kuwarudisha wakenya hao.
Wako watanzania waliokuwa wametoroka maximum security prison Ukonga wakatolokea Kenya. Hao watanzania walihusika katika jaribio la kutaka kumuua Raisi Nyerere kupindua serikali yake.
Kwa hiyo ilikuwa exchange ya watu waliotaka kupindua Moi na Nyerere.
 
Umeandika tu lakini bila kufahamu kwamba wale wanajeshi wa anga wa Kenya walioteka nyara ndege na kuja nayo Tanzania Hezekiah Ochuka na Pancras Oteyo Okumu walirejeshwa nchini kwao Kenya kwa makubaliano maalum kati ya aliyekuwa rais wa Kenya marehemu Daniel arap Moi na Julius Nyerere wa Tanzania.

Kipindi hicho ndio Nyerere naye alinusurika kupinduliwa na wanajeshi wa JWTZ na baada ya watuhumiwa kuwekwa kwenye gereza la Keko na baadhi yao walifanikiwa kutorokea Kenya.

Ndipo makubaliano yalipofanyika kati ya Tanzania na Kenya na kupelekea watoro wa Tanzania akina marehemu Mac Ghee na wenzake kurejeshwa Tanzania kutoka Kenya na wale wa Kenya kurejeshwa Kenya kutoka Tanzania.

Hivyo kama mtu anatoa simulizi kinyume na hili nililolitoa hapa basi ijulikane wazi kwamba ni upotoshaji mkubwa hivyo sio kweli kabisa kwamba Nyerere aliisaidia Kenya, ilikuwa ni nipe nikupe approach.
 
Ngoja nikujibu Ochuka alipewa hifadhi ya kisiasa Tanzania ila mwaka 1983,wanajeshi wetu walipotaka kupindua Serikali yetu na baadhi yao kukimbilia Kenya basi ikabidi yafanyike mazungumzo ya kubadilishana wafungwa ndio ikabidi Moi awakabidhi wakina Luten Eugen Maganga na wenzake na Nyerere awakabidhi wakenya waliokimbilia Tanzania
 
Unafaidika nini na kudanganya watu?

Story yako imekaa upande mmoja sababu hutaki kukubali yalifikiwa makubaliano ya kubadilishana waliotaka kumpindua Moi 1982 na waliotaka kumpindua Nyerere 1983 ,Kina Ochuka walibadilishwa na Hatty McGhee waliokuwa wamepata hifadhi kwnye nchi husika.
 
Sidhani kama ilifanyika bila idhini ya Nyerere, indeed,amri ya Nyerere.
Pale nadhani lilikuwepo carelessness.
Mtu kupata political asylum inapaswa atulizane,siyo aanze kuwazomea kule alikotoka.
 
Ila leo Wagambia wametulipizia kisasi cha kumdahalilisha Zuchu wetu! Ahsante sana Gambia!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…