Kenya imechaguliwa kuwa mwakilishi wa bara la Afrika kwenye Baraza la Usalama la UN

Kenya imechaguliwa kuwa mwakilishi wa bara la Afrika kwenye Baraza la Usalama la UN

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kenya imeishinda Djibouti na kupata kura ya Umoja wa Afrika ambayo inatarajiwa kuongeza chachu ya kampeni ya nchi hiyo kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema, Kenya imepata kura 37 dhidi ya 13 za Djibouti wakati wa uchaguzi ulioandaliwa na Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi ya Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kenya inatarajiwa kuungana na Niger na Tunisia ambazo zilichaguliwa mwezi June kuwa wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameupongeza Umoja wa Afrika kwa kuidhinisha nia ya Kenya ya kuwa na nafasi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuzitaka nchi nyingine wanachama wa Umoja huo kuunga mkono kenya kupata nafasi hiyo.
 
Muhula ujao wa ''uchaguzi'' na sisi (Tanzania) ''tugombee''.
Hongera kwa majirani, watuwakilishe vyema, kila la heri.
 
Yaaaani ukifatilia Kenya jf iko Kama na watu wako ishi milele
 
2019-2020 ni Nani?
Nakumbuka kuna mwaka Tanzania ilikuwa Baraza la usalama ikiwakilishwa na balozi Mahiga
 
Kenya imeishinda Djibouti na kupata kura ya Umoja wa Afrika ambayo inatarajiwa kuongeza chachu ya kampeni ya nchi hiyo kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo imesema, Kenya imepata kura 37 dhidi ya 13 za Djibouti wakati wa uchaguzi ulioandaliwa na Kamati ya Kudumu ya Wawakilishi ya Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Kenya inatarajiwa kuungana na Niger na Tunisia ambazo zilichaguliwa mwezi June kuwa wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameupongeza Umoja wa Afrika kwa kuidhinisha nia ya Kenya ya kuwa na nafasi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuzitaka nchi nyingine wanachama wa Umoja huo kuunga mkono kenya kupata nafasi hiyo.
 
Hangera zao, ni nchi ambayo at least inaleta heshima flani internationally kwa East Africa.
Manake sasa hivi East Africa imejaa dictatorial regimes tupu, so sad. Tawala tulizokuwa tukizisema vibaya miaka michache iliyopita all of a sudden ndiyo wamekuwa mentors na ma'role model wetu, Tz tunaongoza kwa hypocrisy.
 
Yangetangazwa mapumziko ya wiki nzima. Maana hii ya SADC ni rotation ya kawaida tu kiasi kwamba hata angekuwa Dr Shika ndiiye Rais bado angekuwa ndiye mwenyekiti mpya wa SADC. Lkn huko ulimwengu wa sifa wanasifu hatari
 
Hahaa utazania Kulikuwa na achaguzi. na Tanzania imeibuka mshindi.
 
Wakuu sioni Wakenya wakipongezana kwa hili sijaona Raisi wao akipongezwa kwa hatua hii. Ila ingekuwa kwetu nahisi tusingelala kabisa na shughuri zingesimama.

Kuwa Mwenyekiti wa SADC tu ni shida kana kwamba tulikuwa tunashindanishwa na Nchi zingine basi Tanzania ikashinda.

View attachment 1187074
well deserved for our neighbour... kudos!

the good governance gap between Kenya vs the rest of the EAC block is widening by the day.

conversely, Tanzania is nosediving.... we're actually inching towards dire primitivity worse than what we witnessed under the "ujamaa" era!
 
Wakati wa Dr Jakaya tuliwahi kupata fursa hiyo baada ya lobbing ya kufa mtu ya Mkwere yule

Sasa hivi Uhuru anapitia mule mule alipokuwa anapita Jakaya kuanzia mahusiano mema na Wapinzani wake , safar nyingi za nje n.k
 
Back
Top Bottom