Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamani. Mtupe ka bureki kidogo.Tupo busy na kutimiza majukumu ya uenyekiti wa SADC.Tungeambiwa mara ya mwisho ilikuwa miaka zaidi ya 20 iliyopita. Au Victoire nadanganya? Maana nyie wasukuma kale kamsemo ka NIGUSE NINUKE kalizaliwa kwenu!
Kabudi tangia aambiwe kuwa anarithishwa kiti nahisi siku za mwisho mwisho za 2024 atawehuka kabisaaa. Any way alishajua kula na WASUKUMA ndiyo maana anaenda mule mule. Jamaa aliguswa kidogo tu kwa misifa kule diaspora na Kabudi akanuka balaa. Ona sasa Kabudi kahakikishiwa urithi.Jamani. Mtupe ka bureki kidogo.Tupo busy na kutimiza majukumu ya uenyekiti wa SADC.
Wasukuma mnatusingizia.
Jana nimemsikia Kabudi akimsifia Rais kwa kuwa mwenyekiti wa SADC. Kabudi ni mgogo jamani.
Ila wamesahau 2003 Mkapa alikuwa mwenyekiti wa SADC. Najaribu kurewind,hakukuwa na masifa kama haya.Any way hakukuwa na social media back then.
Kizungu kinaweza kutukimbiza mkuuMuhula ujao wa ''uchaguzi'' na sisi (Tanzania) ''tugombee''.
Hongera kwa majirani, watuwakilishe vyema, kila la heri.
Mweee!Fikiria hili tukio lililotokea Kenya kushinda kwa KURA huko UN, lingetokea kwa Tanzania, wale kasuku wa Lumumba wa kusifu na kuabudu wangefunga mitaa yote katika nchi na kututangazia kuwa huu ni ushindi wa Magufuli kama wanavyotwambia serikali ya Magufuli, Nchi ya Magufuli, Ccm ya Magufuli na kila kitu ni cha Magufuli. Ilimradi tu waonekane wanampenda huku ni wanafiki haijapata kutokea.
Leo Kenya imechaguliwa kuwa mwakilishi wa Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kwa kura 37 ikiishinda Djibouti iliyopata kura 13. Kenya imepata ushindi katika duru ya pili ya kura zilizopigwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa, Ethiopia.
Katika duru ya kwanza ya Agosti 5, Kenya ilipata kura 33 kati ya 49, hivyo kulazimika kuwepo duru ya pili kwani mshindi alitakiwa kupata angalu kura 36.
Licha ya ushindi huo, Kenya itashiriki katika uchaguzi utakaofanyika Juni 2020 jijini New York, kuwania nafasi ya kuwa mjumbe asiye wa kudumu wa Umoja wa Mataifa, nafasi itakayoitumikia kwa mwaka mmoja (2021-22). Lakini huoni mbwembwe wala kejeri huko Nairobi na kwingineko tofauti na wiki jana tu hapa Tz ilipopata uenyekiti wa SADC uliopo kwa mzunguko wa nchi 16, basi vibaka wa Lumumba wakaanzisha mapambio ya kusifu na kuabudu kuwa Rais kachaguliwa na kuwashinda marais wenzake wa SADC.
Ndugu zangu, kwamsiojua, kupata kura in AU kwa style ya Kenya ni kazi kubwa kweli kweli, lazima udeploy majasusi katika engle zote kuanzia mabalozi, mawaziri, experts not only in Addis Ababa na Nchi zote za Afrika, bali pia lazima ucheze trick kali pale New York.. I have seen this game!
Sasa kwa ile banana summit ya Dar, Yaani nilistaajabu kabisa kumuona mtu msomi wa Chuo kikuu kabisa anaweka mabango mitandaoni akisema Hongera Rais Magufuli kwakushinda uenyekiti wa SADC, Hili taifa idadi ya wajinga wasomi ni kubwa sana kuliko wajinga wasiosoma.
Bado haujachelewa, Nunua leo Kitabu cha Ujasusi kwa OFA MAALUMU YA 50,000 badala ya bei halisi ya 80,000/= Lipia 50,000 kwa 0715865544 au 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo.
Kwa Dar Kitabu kitaletwa ulipo Bureeee. Nje ya Dar utalipia usafiri 8,000/=
Na Yericko Nyerere
Ushamba mwingi hasa bavichaBongo sasa hiv ni kama WaCongo.....yaani kitu kidogo tunakikuza na kukipa sifa kedekede
Ndio maana nchi hujiunga na kufanya umoja ili kuongeza nguvu, nchi ndogo ni ndogo na udogo wake unamadhara yake , moja wapo ndio kama hilo la djibout kushindwa na kenya.Huko hakuna nchi kubwa na ndogo kwa sababu wapiga Kura ni wanachama wote toka nchi mbalimbali waliohudhuria kikao cha uchaguzi. Wewe unalinganisha na uchaguzi wa hovyo wa CCM ya Bongoland
Kizungu kinaweza kutukimbiza mkuu