Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Swadakta kabisa mkuu, kinachoigharimu Tz yetu ni mifumo ya hovyo na ujanja² wa kiswahili. Mtoa mada + MATAGA wanahangaika sana kulinda legacy ya Jiwe, hawataki kusema ukweli kwamba uchumi wa Tz kudorora ni matokeo ya;
  • Sheria kandamizi
  • siasa chafu
  • ulimbukeni wa viongozi
  • visasi
  • wivu wa kitoto kwa wenzetu n.k n.k
Hamna cha ujasusi wala nini.
Aliyekuwa akikwamisha biashara hayupo sasa ni miaka miwili sasa, Kuna kiwanda kipya kipi kimejengwa?
 
..nadhani tunakosea sana kuwakweza TISS na kukabidhi maisha yetu mikononi mwao.

..suala la viwanda kufa au kustawi linategemeana na mazingira ya kibiashara yaliyoko Tz.
Huwezi kuitenganisha TISS na uchumi wa nchi yoyote duniani.

Changamoto kwa Afrika ni hizi taasisi kusimamiwa kwa maslahi ya kikundi cha watu fulani badala y maslahi mapana ya taifa.

Yale mashirika ya umoja wa mataifa yote kazi yake ni hiyo. Kutengeneza mazingira ya kuinua uchumi wa baadhi ya nchi na kudumaza nchi nyingine.

Ndicho kilichoikuta Tanzania kila walipokuja na wazo la kujenga bwawa la Stigglers tangu baada ya uhuru hadi kiburi cha Magufuli kiliposaidia kuanza ujenzi licha ya mtangulizi wake kuanzisha wazo hilo.
 
Muhimu ni ushindani. Na kwenye dunia kama hii huwezi kukwepa ushindani kwasababu ndicho kichocheo cha ubora.

Mfano kwenye tenders, watanzania wangapi wanapata?

Ukiwapa wabongo, ndio hao kama kina Lugumi.

Tender nyingi hasa za ujenzi wachina wanachukua, sasa kuna tofauti yeyote hata wakipata wakenya?

Mfano: Kwenye banking sector, nini kinafanya banks kubwa na kongwe kama NMB, NBCna CRDB kushindwa kufungua matawi hata Kenya huko?

Huduma mbovu balaa.

Tanzania hapa kuna mabenki ya Kenya kibao: KCB, Equity,

Sisi tumebaki kulalamika tu. Ukimwajiri mbongo yaani Jumatatu anaumwa, Jumanne, kafiwa na bibi yake, Jumatano baba yake wa babu yake ana birthday, Alhamisi amepata dhatula mke wake anaumwa, Ijumaa akijitahidi atakuja kazini lakini ataomba ruhusa saa 4 asubuhi.

Wakati huo atakuwa analalamika sana mshahara hautoshi.

Wabongo tubadilike, hatuwezi kuishi hivi siku zote.

Tumekuwa kama Wazulu wa South Africa.

Unabagua kazi za kufanya, akizifanya mtu mwingine unaona wivu na chuki.
[emoji867][emoji867][emoji867]
Pale Zenji tatizo hili limeota na mizizi kabisa yaani mpaka huwa najiuliza Tanzania tutaendelea kwa staili hii kweli??
 
[emoji867][emoji867][emoji867]
Pale Zenji tatizo hili limeota na mizizi kabisa yaani mpaka huwa najiuliza Tanzania tutaendelea kwa staili hii kweli??
Inasemekana asilimia kubwa ya watu wa muwambao wa bahari ya Hindi ni wavivu
 
Back
Top Bottom