Kenya imejitosheleza kijeshi kukabiliana na mikwara ya jeshi la Uganda? Can KDF supress the Ugandan forces??

😂Alioandika hii ni mwehu, Polisi tu kila mkoa wapo kuanzia elfu moja, sasa jwtz ndio iwe na active personnel elfu 26!!! ,Miaka ya 70 Congo tu ilikuwa na zaidi ya askari jeshi elfu kumi
Hizo Takwimu hua zinaandikwa na wehu tu,Kuna takwimu hata sa hivi zinaonyesha DRC jeshi lake liko Kwny top 10 ya majeshi bora Africa na Tz iko huko nje ya Top 20.

Na Gen. Wa DRC Kuna video Yuko anajisifia huko mitandaoni kwa wao kua Kwny Top 10.Wehu sana wale.
 
😂Vijana wakishapiga stories vijiweni wanakuja na tafiti zao,jeshi la DRC ni Mobutu tu ndiye aliliimarisha sana na likawa bora na badae akaliharibu, imagine katika jeshi zima alikosa pilots mwaka 1997 wa kuwatuma wakati jet fighters alikuwa nazo
Kwa sasa lile ni aibu hata kuliita jeshi,kuna clip nimeona juzi twitter wamevamiwa alafu wanabushana jinsi ya ku aim rocket launcher yani hakuna command
 
😄😄😄 Juzi Tshisekedi ameteua mkuu wa majeshi mpya,then Jana tu ikaachiwa video hewani huyo jamaa Yuko anakula zake Pombe na washikaji zake akisherekea kuteuliwa kua mkuu wa majeshi 😄😄😄. Seriousness hamna pale
 
Sababu kubwa ya Uganda kuishinda Kenya ni uimara wa jeshi la Uganda ukilinganisha na jeshi la Kenya, hakuna nchi yoyote katika ukanda huu ukiacha Ethiopia ambayo imewekeza na kuimarisha jeshi lao zaidi ya Uganda ikifuatiwa na Rwanda.

Kumbuka kwamba Ethiopia, Uganda na Rwanda hawana jeshi la majini/baharini ambalo linahitaji bajeti kubwa kuliko jeshi la angani na ardhini, kwahiyo bajeti ndogo tu inatosha kwa hizo nchi kuwa na jeshi kubwa na vifaa vingi vya kisasa kuliko nchi zenye jeshi la majini. Jeshi la Uganda halina mgawanyiko wa makabila Kama ilivyo Kenya, chakula ni jambo muhimu Sana kwa nchi kuweza kupigana vita, kumbuka nchi ikiwa vitani, pesa nyingi inatumika kugharamia vita, hakuna pesa ya kutosha kuagiza chakula toka nje ya nchi

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Unauliza nani atatumia bandari katika emergency.
Uganda ana silaha gani za kushambulia bandari yoyote ya Kenya?
 
Unatumia vigezo gani kusema jeshi la Kenya halina nidhamu?
Tena unalilinganisha na la Uganda ambalo limewahi asi zaidi ya mara tatu. Uganda ambayo ina waasi wa Lord's Resistance Army.
Kikubwa jeshi la kenya nidhamu ni 0,plus ukabila,updf wanajua udhaifu wa kdf,hao kdf kwenye operesheni zao nyingi wanafeli
Operations za KDF ni ngumu, Uganda hawajawahi kuzifanya. Al Shabaab kuna jeshi la AMISOM wameunganishwa majeshi kadhaa ya Afrika uko, wote wameshindwa kwahiyo Afrika nzima ina majeshi vilaza hamna kitu. Uganda yenyewe si ina operations Somalia, wameshinda?
 
1. Hizo ndege za kubeba vifaru airlifters Uganda wanazo? Hawana ndege ya kubeba hata tani 40 hao. Na sijasema kwa lengo la kijeshi, kiuchumi Kenya ikizima huduma za bandari kwa mizigo ya Uganda 80% ya mizigo yake itakosa la kupita. Bandari sio kama television channels kwamba watahamia Dar es Salaam siku hiyo hiyo, kwanini wasitumie Dar sasa watumie Nairobi mizigo yote hiyo. Kama unadhani Uganda imekuwa Israel kufanya airlifting ya bidhaa za kiraia kwenye vita basi sawa, wabebe petroli, madawa, magari, vyakula na matumizi mengine kwa cargo jets alafu mseme uchumi hautoathirika. Mpaka bandari ya Dar ije kusawazisha mambo washapigwa inflation ya hali ya juu.

2. Sasa kama hujui kitu kinacholikuza jeshi la Kenya ni Al Shabaab. Yani unaamini katika dunia hii al Qaeda na Taliban zilidhoofisha jeshi la Marekani? Unaamini ISIS ilidhoofisha jeshi la Urusi? Ushawahi ona Pentagon wakitaka hela za miradi na kununua silaha huwa wanatumia visingizio gani, ushaona Kenya ikinunua silaha kisingizio ni nini, unajua kisingizio walichotumia Kenya kumshawishi Trump aruhusu Marekani iwauzie helicopters wakati Obama alikataa ni nini. Hawakuwa na silaha walipoanza missions wakanunua kama hizo armmoured vehicles na helicopters.

Uganda ikishirikiana na Al Shabaab (jambo ambalo sio rahisi) si Kenya inawavutia Lord's Resistance Army kina Joseph Kony (rahisi zaidi).

3. Uganda haina intelligence ya kufanya hivyo, hakuna nchi unaivamia mwenyewe ukitarajia support ya local community wakati raia wanakubaliana na serikali yao. Ukabila hata Uganda upo, hapo unazungumzia nchi yenye Kabaka na mwenye vijana wake ambao hubishana na serikali, na Kabaka serikali haimfanyi chochote labda ijiandae kuuana na Baganda.

4. Vita ni vita, logistics ni sehemu ya vita. Offensive, defensive, counter offensive zina timelines zake ila mwisho wa siku Uganda anapigwa.
Kwamba kisa Muhoozi karopoka basi watashinda, Amin si ariropoka dhidi ya Tz, alishinda?
 
Hamna uwezo ninyi kupigana na Uganda (Empty stomach can't fight)

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Umekosa la kusema, unajibu ilimradi tu., get a life, umedhohofika ki fikra, hapa ni wivu na chuki kwa Kenya ndio zinasukuma hisia zako, nothing substantial, mwanaume jike😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 

Wao wapigane tu watuachilie mbali ss no bongo yetuView attachment 2379435

It's getting hot in here
 
Achana na huu utoporo Mkuu yani unaamini Tz ina Tanks 42 !!!,mimi zaidi ya mara moja nimeshuhudia vifaru vya JWTZ Mwanza vimeletwa kwa train vingi mno, je kambi zingine je, kwanza hamna nchi ina Tanks 42 unless uongelee Tanks zenye uwezo wa Nuclear
Hivyo 42 hata kambi moja tu za hapa hapa Dar zina vingi kuliko

Dar ina zaidi ya Kambi 10 za Jeshi
 
Kenya ina Jeshi kubwa lakini haliko well organised, limegawanyika pakubwa kutokana na siasa za ukabila pamoja na vitendo vya rushwa.
Kwasababu hiyo pamoja na kubebwa na factors kadhaa ulizozitaja hapo juu,
Jeshi lenye matabaka ni ngumu sana kutoboa dhidi ya Jeshi lenye linalozungumza lugha moja.


Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Jeshi la Kenya ni utopolo, wacha kutetea hao vilaza, operation zipi za Kenya ambazo ni ngumu?, KDF walishindwa hata Operations za UN huko South Sudan ambako nchi nyingi za Dunia zilikua na vikosi vyao huko, ni KDF pekee ndiyo walishindwa kazi wakatimuliwa na Ban Ki mon

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Umekosa la kusema, unajibu ilimradi tu., get a life, umedhohofika ki fikra, hapa ni wivu na chuki kwa Kenya ndio zinasukuma hisia zako, nothing substantial, mwanaume jike[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hamna uwezo wa kupigana na Uganda ninyi

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Achana na huu utoporo Mkuu yani unaamini Tz ina Tanks 42 !!!,mimi zaidi ya mara moja nimeshuhudia vifaru vya JWTZ Mwanza vimeletwa kwa train vingi mno, je kambi zingine je, kwanza hamna nchi ina Tanks 42 unless uongelee Tanks zenye uwezo wa Nuclear
Tz hana mazoea ya ku-publish taarifa zake online. Mambo mengi sana yanakuwa reserved.
Ushawahi kujiuliza kwanini vikosi vya jeshi vina namba mchanganyiko? Yaani 91KJ, 832K...n.k
 
Toka nione askari wa kenya wanaiba mikate supermarket nilisema hii nchi haiwezi kushinda vita yoyote labda kuwaonea tu raia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…