Kenya imeshindwa kuwakinga Watu 400,000 na njaa Kenya

1. swali, kwanini Tanzania nchi ambayo haisumbuliwi Sana na ukame lakini imewekeza zaidi katika kilimo cha umwagiliaji kuliko ninyi ambao sehemu kubwa ya nchi haipati mvua za kutosha?

Tanzania eneo tulilojenga miundo mbinu ya umwagiliaji ni hekta laki 8, wakati Kenya ni laki 2 tu.

2. Kwanini Tanzania ambako Kuna eneo kubwa lenye rutuba lakini bado tumeweka Sheria ya kuhakikisha matajiri/wageni/wanasiasa hawawezi kujimilikisha ardhi kubwa na kuwaacha wananchi masikini wanaishi maeneo yasiyokua na rutuba Wala mvua za kutosha?

NB: Njia pekee ya kukabiliana na ukame ni kujenga miuondombinu ya umwagiliaji, sio kupiga kelele na kutangaza janga la njaa Kila mwaka[emoji23][emoji23][emoji23]
 
1. swali, kwanini Tanzania nchi ambayo haisumbuliwi Sana na ukame lakini imewekeza zaidi katika kilimo cha umwagiliaji kuliko ninyi ambao sehemu kubwa ya nchi haipati mvua za kutosha?

Tanzania eneo tulilojenga miundo mbinu ya umwagiliaji ni hekta laki 8, wakati Kenya ni laki 2 tu.

2. Kwanini Tanzania ambako Kuna eneo kubwa lenye rutuba lakini bado tumeweka Sheria ya kuhakikisha matajiri/wageni/wanasiasa hawawezi kujimilikisha ardhi kubwa na kuwaacha wananchi masikini wanaishi maeneo yasiyokua na rutuba Wala mvua za kutosha?

NB: Njia pekee ya kukabiliana na ukame ni kujenga miuondombinu ya umwagiliaji, sio kupiga kelele na kutangaza janga la njaa Kila mwaka[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wapi, Ule ukame wa kufanana na pale Masai mara si ukame, 70% ya Kenya inafana hivyo...

This is Chalbi, Kenya.. Nionyeshe eneo TZ ambalo liko hivi



Dawa ya ukame ni kujenga mifumo ya umwagiliaji Kama tunavyofanya Tanzania, Egypt na Nigeria. Kwanini msitumie maji ya Lake Turkana?, Punguzeni uzembe njaa itawamaliza.
 
Misri wana mto Nile ambayo nchi nyengine haziruhusiwi kuugusa,nyie mna maji maji maji kila kona.
Tatizo kuu Kenya ni MAJI ikifuatwa na ardhi isiyo weza kumudu hata umwagiliaji wenyewe(non-arable land), yaani ardhi yenye mawe mengi(rocks).
Mshukuru Mungu sana nyie.
 
😆😄
Bwana mdogo, yaani hako kaneno ka kilatini kamekuacha hooi. Sikiliza kijana mimi ni composite expert. Law naijua vizuri, though I'm not a lawyer.
🤣🤣🤣
Kwanza spelling yenyewe umefeli...bure kabisa,jikite kwenye uswahili weye kinjekitile.
 
Ziwa Victoria, Lake Turkana na mito ya msimu wa mvua, vyote vinatosha kuwa vyanzo vya maji kwa ajili ya kilimo na mifugo.

Kenya ardhi yenye rutuba Kama ingegawanywa kwa usawa(Equitable) Kama ilivyo Tanzania, hilo Tatizo la upungufu wa chakula lisingesumbua, tatizo ardhi yote nzuri imechukuliwa na matajiri na wanasiasa.
 
Huku Tanzania mbona mahindi yanaozea kwenye maghala kwa kukosa soko, wakenya mnakwama wapi kuja kuchukua huku au yana Aflatoxin?
 
Huku Tanzania mbona mahindi yanaozea kwenye maghala kwa kukosa soko, wakenya mnakwama wapi kuja kuchukua huku au yana Aflatoxin?
Tatizo ni maji kwa mifugo na wafugaji sio mahindi.
Ni maeneo ya wafugaji.
 
Tatizo ni maji kwa mifugo na wafugaji sio mahindi.
Ni maeneo ya wafugaji.
Mkuu nimeona jana BBC swahili wakihojiwa wakazi wa Kilifi, wanasisitiza kutaka msaada wa chakula hasa mahindi kutoka serikalini baada ya serikali ku-declare njaa eneo hilo kuwa ni janga la kitaifa. Sasa hao wakazi wa kilifi watasaidiwaje kama sio kuwapelekea hayo mahindi wapate japo githeri moja kwa siku?
 
Njaa na ukame Kenya ni fursa kwa wakulima wa Tanzania. Huko Songea na Mtwara wakulima hawana mahali pa kuhifadhia mahindi jinsi yalivyo mengi.

Serikali ya SSH imekalia tozo tu badala ya kuwasaidia wakulima kuuza mahindi yao huko Kenya kwenye njaa.
 
Hilo la kawaida sana. Serikali haijaanza leo kuwalisha wahanga,sema tu ndivyo ilivyo ardhi ya Kenya.
 
hili ndio tatizo la watanzania hasa hawa kindakindaki wa uvccm iv umeshaona wapi nchi zaidi ya asilimia 75 ni wakulima na wafugaji ikapiga hatua kimaendeleo??zaidi hao asilimia 75 wakalima tu kilimo kisicho na tija maana particularly watalima locally, je hapo mtakuwa mmefanya nini??_zaid ya kuharibu productive land, nakuwafanya wananchi hasa vijana kukichukia kilimo instead kilimo ni biashara,pia isitoshe hats soko hamuwatafutii ,nyinyi mmekalia tozo tu kwa huyu mkulima, hivi nyinyi wanatozo mnamchango UPI kwa mwananchi wa kawaida mmejaa umimi na undugunization na kujuanization
 
wanahangaika na BBI tu, huku wanakufa kwa njaa, kipindi kile walikataa mahindi ya 255 wakasema yana aflatoxin aka sumu kuvu sasa hivi waone sasa kama watakula mchanga, mahindi wauziwe hata milioni moja kwa debe moja
 
Tuwahurumie kwa kuwa na njaa kila mwaka lkn usihusianishe njaa na katiba ni Vitu ambavyo havina uhusiano. Wacha uboya, ntakuhtaki kama mc mbonile
 
Kwa hiyo katiba mpya ikiyatambua haya ya kila mtu kuwa na uwezo wa kumiliki ardhi ni vibaya? Katiba mpya kuboresha na kuzilinda maliasili ni vibaya?

Angalia tofauti ya magufuli na waliomtangulia, huini tofauti na utofauti huo ni udhaifu wa katiba?

Leo hii pato la madini limeongezeka kwa zaidi ya 100% magufuli kaondoka, limeanza kushuka, huoni tunahitaji katiba mpya ili kila kiongozi akiingia alinde mali za taifa?

Magufuli kafariki petrol ni 2200/- leo ni 2600/- huoni ni udhaifu wa katiba iliyopo?
 
Mimi mtanzania nimekupa.like. Hawa ni misukule wa ccm. Maadam wanakula na kunya, basi akili zao zimelala. Ndiyo maana ukame kenya anatumia kama hoja ya kukataa katiba mpya Tanzania. Zero thinking
 
Kaka katiba iliyopo inalinda rasilimali zetu vizuri Sana, tatizo ni viongozi wenye upeo, uwezo na wenye nia ya kweli na uthubutu wa kuitekeleza katiba bila kuionea haya.

Tatizo la Africa ni viongozi Bora, sio katiba, kumbuka kwamba hata vitabu vitakatifu Biblia na Quran ni vitabu Bora lakini sisi binadamu hatuvifuati, hilo mbona hatudai mabadiliko ya Biblia au Quran viandikwe upya?.

Kenya tatizo lao ni uongozi Bora sio katiba, hata baada ya kuandika katiba mpya Kenya, hakuna mabadiliko yoyote katika Mambo ya msingi yanayogusa raia wa kawaida, Hali ndio inazidi kuwa mbaya kila kukicha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…