Huwa wanajiaibisha hivyo, jamaa atakurupuka kuanzisha uzi bila kuangalia kwa makini kwanza na kuhakikisha kama anachodhania ndicho. Yaani picha iko wazi inaonyesha Mombasa imeizidi Dar kwa mwanga usiku, hapo hujataja maeneo mengine Kenya, kwa mfano naona Kisumu na viunga vyake imewaka kuzidi mji wowote Tanzania.
Ni wazi kwamba Kaskazini Kenya ni jangwa tupu, hivyo kiza huko ni jambo la kawaida, maana nusu ya Kenya ni kame tupu, lakini ukiangalia nusu ya Kenya ambayo tumewekeza na kuishi, ina mwanga zaidi ya mataifa yote ya mashariki mwa Afrika na Kati.