Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Lakini kwa wanaofahamu vizuri Jaji huyo, hawakushangazwa na uamuzi wake wa kubatilisha uchaguzi wa nchi hiyo.
Jaji Maraga, amemjibu Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu ya nchini humo.
"Mimi siyo Mwanasiasa na nafanya kazi kulingana na misingi ya kiapo cha utii nilichochukua ili kuwatumikia Wakenya, siungi mkono JUBILEE wala NASA au mtu yeyote.
Nasimamia Katiba ya Kenya. Nendeni mkashindane kwenye uchaguzi na kama yeyote hataridhishwa na matokeo ni kiasi tu cha kuleta shauri/malalamiko yenye ushahidi mzuri/wa kutosha na mimi na wenzangu tutafanyia kazi bila kusita.
Kumbuka kwamba namuogopa Mungu peke yake".
Jaji Mkuu David Maraga.