Kenya: Jaji Mkuu amjibu Kenyatta. Nendeni mkashindane kwenye uchaguzi

Kenya: Jaji Mkuu amjibu Kenyatta. Nendeni mkashindane kwenye uchaguzi

Huyu ndio jaji. Sio wale wengine anatoa hukumu huku mfukoni ana kadi ya chama ambaye kwa vyovyote atai-favor mamlaka iliyompa hicho cheo tuache kufanyana wajinga.

Kuna mmoja alifikia hadi hatua ya kugombea uongozi kupitia chama chake mara baada ya kustaafu. This is truly separation of power among the state organs.
Unajuaje kama na huyu akistaafu atajiunga na NASA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi Tundu kawaambia wanasheria wote wagome... wamekataa tena wametishiwa kufutiwa lesi zao... Huyu Jaji ahamie Tanzania
 
Huyu ndio jaji. Sio wale wengine anatoa hukumu huku mfukoni ana kadi ya chama ambaye kwa vyovyote atai-favor mamlaka iliyompa hicho cheo tuache kufanyana wajinga.

Kuna mmoja alifikia hadi hatua ya kugombea uongozi kupitia chama chake mara baada ya kustaafu. This is truly separation of power among the state organs.
Unafahamu katiba ya nchi yako inasema nini juu ya hao unaodhani hawapo sahihi kama hao wa Kenya?
Watanzania acheni kutamani vitu ambavyo hamuwezi kuvifanyia kazi, Jeuri ya Maraga imetokana na Katiba iliyopatikana kwa Umwagaji damu! je nanyi mpo tayari kufanya hivyo?

Msipende kutamani mafanikio ya wengine ilihali maogopa kuving'oa visiki vya kuyafikia yale mtamaniyo
 
😀😀😀😀😀😀😀 nimecheka sana MKUU, kukurupuka kubaya sana
Sasa mtu hata haelewi anasimamia hoja gani utajadili nini naye mkuu?

Unajua tunapojadili kuhusu uhuru wa mahakama/majaji tunajadili kitu tofauti kabisa na siasa!

Mimi ukiniambia majaji hawako huru kwasababu ya katiba nitakushangaa na nitajua husomi bali unaakunywa sana kahawa vijiweni..lakini ukisema labda unaona hawafai kutokana na uteuaji wao upo kikada kada ndio naweza kuelewa..

Sasa huyo kijana hajengi hoja yeye anazungumzia mara makinikia.. Sasa hapa yanahusikaje hayo?
 
Huku kwetu bado kaimu Jaji mkuu anusibiri huruma za Magu ili ateuliwe!
 
01bf2118b990b2cd0e4aff7aad489aa0.jpg
Jaji Mkuu nchini Kenya, David Maraga aliudhihirishia ulimwengu kuwa kuna uhuru wa mahakama katika bara la Afrika ambako agharabu majaji wanaonekana kutetea walio madarakani.

Lakini kwa wanaofahamu vizuri Jaji huyo, hawakushangazwa na uamuzi wake wa kubatilisha uchaguzi wa nchi hiyo.

Jaji Maraga, amemjibu Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu ya nchini humo.

"Mimi siyo Mwanasiasa na nafanya kazi kulingana na misingi ya kiapo cha utii nilichochukua ili kuwatumikia Wakenya, siungi mkono JUBILEE wala NASA au mtu yeyote.

Nasimamia Katiba ya Kenya. Nendeni mkashindane kwenye uchaguzi na kama yeyote hataridhishwa na matokeo ni kiasi tu cha kuleta shauri/malalamiko yenye ushahidi mzuri/wa kutosha na mimi na wenzangu tutafanyia kazi bila kusita.

Kumbuka kwamba namuogopa Mungu peke yake".

Jaji Mkuu David Maraga.

Wonderful and admirable Justice Maraga, may the Almighty God(Jehovah) Bless you. Naamini Justice Maraga and his court was fair what remains is for Kenyans to vote again as God had spoken, I believe the same God will prove on 17/10/2017 to the world that God of Abraham, God of Jacob and Isaak maintains His Word! No changes, as Vox Populi Vox Dei shall prevail.
 
Lubuva...ccm
Tulia....ccm
Augustin... Ccm
Mtungi...ccm
Kanali shimbo...ccm
Mawazri wote...ccm
Wakuu wa mikoa...ccm
Wakuu wa wilaya...ccm

Nknk
Tanzania...mali ya ccm

Mrema .....CCM
Seif............CCM
Lipumba..................CCM
Hamad Rashid..............CCM
Momose..............CCM
Sumaye................CCM
Ngoyai...................CCM
Mgwila...............CCM
Zuberi ...............CCM

kwahiyo mnataka nini?
watanzania wote ni ndugu na familia moja, msimu wa uchaguzi ukifika tunavaa jezi tofauti tunacheza mechi ya kirafiki.

msitufananishe na Kenya, Jomo Kenyata hajawahi kuwa rafiki wa Jaramongi- hili hamuhitaji kufundishwa, hivyo majaji nao lazima wajipambanue na wakae upande unaowafaa.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Huyo unayemsema alipata wapi kadi ya chama na kisha yeyw kugombea uongozi (RAIS) km yeye alikuwa JAJI?

HAYA NI MAAJABU YA 10 YA DUNIA HII

Sent using Jamii Forums mobile app
wewe kama ni mtanzania basi umezaliwa baada ya kwaka 1994.
Kwafaida yako, jifunze yafuatayo:
baada ya uhuru, kama huna kadi ya chama(TANU) ulikuwa huwezi kupata scholarship. kwahiyo wote waliosoma elimu ya juu walikuwa na kadi ya TANU .
Tulipoenda JKT kwa mujibu wa sheria tuligawiwa kadi za CCM, kwahiyo sisi wote tulioenda JKT kabla ya multparty tunazo kadi za CCM, kwahiyo ujue kuwa viongozi wote wa vyama wanakadi za ccm ikiwemo kiongozi wako if and only if alikuwa na sifa za kujiunga na JKT kama compulsory
 
Wanalindwa na dola kwa mbwembwe, maigizo na maelekezo ya mwenyekiti wa ccm.

Ijulikane kabisa hawafati katiba hata kidogo

Mfano
AUGUSTNE RAMADHAN....kuacha ujaji na kugombea urais ngazi ya chama ccm

Tulia naibu spika kuacha ujaji na kupewa ubunge kisha uspika vyote kupitia ccm

Je hawa wanaifuata na kuitii katiba?......

Kuwa wanachama wa ccm wakiwa majaji...kuna kupona hapo akishitakiwa wa upinzani?..... Kunahaki?.....je conflict of interest???

Mmeona wenyewe bunge lilivonajisiwa.... AIBUUU
Mkuu tuweke kumbu kumbu sawasawa Tulia hajawahi kuwa Judge bali alikuwa naibu mwanasheria mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
01bf2118b990b2cd0e4aff7aad489aa0.jpg
Jaji Mkuu nchini Kenya, David Maraga aliudhihirishia ulimwengu kuwa kuna uhuru wa mahakama katika bara la Afrika ambako agharabu majaji wanaonekana kutetea walio madarakani.

Lakini kwa wanaofahamu vizuri Jaji huyo, hawakushangazwa na uamuzi wake wa kubatilisha uchaguzi wa nchi hiyo.

Jaji Maraga, amemjibu Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu ya nchini humo.

"Mimi siyo Mwanasiasa na nafanya kazi kulingana na misingi ya kiapo cha utii nilichochukua ili kuwatumikia Wakenya, siungi mkono JUBILEE wala NASA au mtu yeyote.

Nasimamia Katiba ya Kenya. Nendeni mkashindane kwenye uchaguzi na kama yeyote hataridhishwa na matokeo ni kiasi tu cha kuleta shauri/malalamiko yenye ushahidi mzuri/wa kutosha na mimi na wenzangu tutafanyia kazi bila kusita.

Kumbuka kwamba namuogopa Mungu peke yake".

Jaji Mkuu David Maraga.
Life and death,ni mara chache sana kukuta mtu wa imani kama hii katika uongozi,unakula kiapo na unakifanyia kazi,haijalishi kama utakufa au utateswa lakini imani yako kwa Mungu ndio itakuweka huru.
 
Back
Top Bottom