Kenya kama Malawi, wapanga kupeleka vibarua wa Mashamba ya Israel kwa ujira wa Ksh. 228,000 (4,000,000Tsh)

Kenya kama Malawi, wapanga kupeleka vibarua wa Mashamba ya Israel kwa ujira wa Ksh. 228,000 (4,000,000Tsh)

Hata mimi wakija tanzania naenda,mshahara wa laki 6 ninazolipwa kama mwalimu niliyefanya kazi kwa zaidi ya miaka 10 hautoshi kabisa yaani ,watoto watatu,mke jumlisha mikopo ya bayput ,nmb,crdb,napaki na kiasi cha 200K,sasa mtu unalipwa 4M kwa mwezi mbona pesa ndefu,waje na tz, I will be the first
Aahaaaaaa

All the best mkuu
 
- Waje fasta na huku!
Shida ni pale bila ya refa wa nguvu kijana wa kawaida hatoonekana.
- Haya ni mambo ya kawaida, mkindoa udini na vita, kuwaonyesha vijana duniani kulivyo.
Ona vijana mlivyo wajinga hamfikirii mara 2 uliwahi kuona watu wanalima vitani?
 
Kenya inapanga Kupeleka Vijana wapatao 1,500 kuwa Vibarua wa Mashamba ua Wayahudi Kufuatia Vibarua zaidi ya 10,000 wengi wao kutoa Thailand kukimbia Vita vya Israel vs Hamas hivyo kuacha mashamba ya waloweso yakiwa hayana Vibarua.

Israel Kwa Sasa imekuwa inakimbilia Afrika ambako watu Wana shida na njaa Kali kupata Vibarua wa Mashamba Kwa kuingia makubaliano na Nchi zinazotaka kuwauza watu wake kuwa Manamba.Kenya imeungana na Malawi katika ku export Manamba bila kujalisha vita vinavyoendelea.

View: https://twitter.com/Kenyans/status/1732659113245409360?t=dKV8Sq3MVESiicFRnoy9vQ&s=19

Kwa mtu mweusi utu sio kipaombele akina pesa ndio maana wakati wa biashara ya utumwa mawakala walikuwa Weusi wenzetu.

Swali.
Je Wabongo mko tayari kuwa Manamba kwenye mashamba ya Wayahudi mlipwe Ujira wa Shilingi Milioni 4?

View: https://twitter.com/BBCAfrica/status/1732724178812387367?t=3YyJH021dtzxhz1K23xAdA&s=19

Pia soma Malawi: Rais Chakwera akosolewa kwa kutuma vijana 221 wa Malawi kufanya kazi katika mashamba nchini Israel

Mbona nyinyi mnapeleka mabinti zetu huko uarabuni kufanya kazi za ndani tena kwa mishahara midogo na wanafanyiwa unyanyasaji.
Screenshot_20231209-093744.png
 
Hivi ardhi ya Israel mnaijua lakini..?😂😂😂

wakuu hakuna kurudi nyuma hata kama ni changarawe tutalima tuu milioni 4 kwa siku 30 sio mchezo
 
Hao ni hamas political bureau ndio kazi yao kuongelea siasa. Hamas military hawana muda wa kuongea siasa

Sir Robert: Be logical jamaa yangu......! Hukatazwi kabisa kuitetea Hamas....but be sensible please.....Hivyo akina Ismail Haniyeh, Moussa Abu Marzuk na Khaled Mashal ambao ndio think tank ya Hamas ni wapuuzi? Hawajui wanachokisema......?
 
wakuu kwa aliyefanikiwa kwenda naomba anijuze na mm katumia njia ipi ili nami niweze kufaulu niende
 
Hata mimi wakija tanzania naenda,mshahara wa laki 6 ninazolipwa kama mwalimu niliyefanya kazi kwa zaidi ya miaka 10 hautoshi kabisa yaani ,watoto watatu,mke jumlisha mikopo ya bayput ,nmb,crdb,napaki na kiasi cha 200K,sasa mtu unalipwa 4M kwa mwezi mbona pesa ndefu,waje na tz, I will be the first
Gharama za maisha zipoje huko..usije tu kuconvert ukaiona 4m but unaweza kuta hapo kodi ni 60% bado matumizi
 
Jiandae kwenda kupigana vita dhidi ya hamas hakuna mashamba wala bustani huko. Unalima vipi rocket zinapita kila baada ya dk.1 ?kweli ujinga mzigo.
Kwani hao wanaopelekwa si watu wazima, kwani wanalazimishwa kwenda? Serikali inatoa utaratibu wa anayetaka aombe kazi hizo, hakika watajitokeza watu wengi
 
Kwani hao wanaopelekwa si watu wazima, kwani wanalazimishwa kwenda? Serikali inatoa utaratibu wa anayetaka aombe kazi hizo, hakika watajitokeza watu wengi
Kazi ya serikali ni kulinda usalama wa raia wake. Kuwa mtu mzima siyo sababu ndio maana wewe mtu mzima unaweza kuamua kujinyonga lakini serikali ikakushtaki. Israeli kwa sasa siyo salama kwa raia wetu kwenda kufanya kazi huko kuna vita.
 
Back
Top Bottom