Kenya kufungua Ubalozi katika jimbo linalotaka kujitenga na Somalia

Kenya kufungua Ubalozi katika jimbo linalotaka kujitenga na Somalia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Somaliland inataka kutambuliwa kama nchi huru.

Kenya itafungua ubalozi mdogo katika jimbo la Somaliland kufikia mwisho wa mwezi Machi wakati Somaliland nayo ikipanga kupandisha hadhi ofisi yake ya Kenya kuwa ubalozi mdogo.

Tangazo hilo la pamoja limetolea na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somaliland Muse Bihi Abdi mwisho wa ziara yake nchini humo.

Viongozi hao wawili pia walikubaliana ndege ya Shirika la ndege la Kenya Airways kufanya safari ya moja kwa moja kutoka mji mkuu wa Nairobi, Kenya hadi mji wa Hargeisa ambao ni mji mkuuwa Somaliland kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

Hatua hiyo inaonekana kuikera Somalia, ambayo imetangaza kukatiza uhusiano wake wa kidiplomasia na Kenya.

Somaliland ilijitenga na Somalia in 1991, lakini juhudi zake za kutaka kutambuliwa kimataifa kama taifa huru hazifanikiwa huku Somalia ikisisitiza kuwa bado ni sehemu ya eneo lake.

Somalia imewaita nyumbani wanadiplomasia wake kutoka Kenya na kuwapatia muda wa siku saba wanadiplomasia wa Kenya kuondoka nchini humo.

Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna amesema kamati ilikuwa imebuniwa kutatua mzozo kati ya nchi hizo, kwani zina uhusiano wa muda mrefu ambao unastahili kulindwa.
 
🔥🔥🔥
Nothing to say rather than saying, we especting more fire.
 
Unakata uhusiano na Nchi kubwa kama Somalia ili uhalalishe uhusiano na kajimbo kadogo hako! Kenya bhana!
Somalia ni wajinga, wanasumbua sana. Lazima tuwafunze adabu.
 
The situation is fast escalating. Kuna habari kuwa Somalia National Army (SNA) wanachukua position katika border ya Kenya na Somalia. Sijui wanapanga kufanya nini. Lakini wajue kitu kimoja, wakijaribu kuingia Kenya tutafinya mak*nde zao hadi zipasuke.


 
Hahaha naona Wabongo mumeanza kutetemeka kwa uoga. Tulieni muone ngoma inavyochezwa.

Hiyo haitusaidii, tumegombana sana lkn hatuoni maisha ya wananchi wetu yakibadilika.
 
Back
Top Bottom