Lile bomba la mafuta ya Uganda lililomfanya Uhuru kwenda mpaka Paris na kurudi mikono mitupu unafikiri bila ushawishi wa nje tungeweza?
Tulipo wakarabatia Uganda reli pale portbell na kukarabati meli ya mabehewa ili tuweze kuwashawishi UN kutumia bandari ya Dar kupeleka mizigo yao South Sudan, unafikiri ni siasa za ndani zile?
Ujenzi wa reli mpya toka Mpanda mpaka bandari mpya ya Karema ili mizigo inayoenda Lubumbashi na kusini mashariki mwa Congo isilazimike kupitia Zambia, huoni tunaongeza ushawishi?
Meli mpya ziwa Nyasa, Tanganyika, Nyanza na kule bahari ya Hindi, huoni huo ni mkakati wa kuzivuta nchi zote zinazotuzunguka kututegemea sisi?
Kenya hawakuanza leo, wamekuwa wanatumika sana kutuharibia mambo yetu. Hata hivi karibuni, baada ya kuona tunapata mikopo kutoka AfDB wakampenyeza mtu wao kuwa makamu kule AfDB ili atuwekee kauzibe.