Kwa nini Somalia yote isiwe nchi moja kama ilivyokuwa kipindi cha Siad Barre ili muweze kuitawala pembe yote ya Africa? Na muweze kuwa na ushawishi katika siasa za dunia? Hamuoni mnagombanishwa na kugawanywa makusudi ili sehemu ile isishikiliwe na dola ya kiafrika yenye nguvu? Unafikiri ni kwa nini pembe yote hiyo inashikiliwa na vinchi vidogo vidongo?
Sisi tulikua na nchi yetu na Somalia ilikua nchi tofauti wakati tunapata Uhuru....
Lakini mwaka 1962 tuliamua kuungana muungano ukawa wa ujanja ujanja na wenye kero nyingi afadhali hata ya Zanzibar na Tanganyika kero si nyingi sana
1989 said barre akatunga sheria kandamizi kwa wana Somaliland ikiwemo kupigamarufuku mtu kujenga nyumba nzuri YA GHOROFA kule Hargeisa GHOROFA zote zijengwe Mogadishu tu
Shule zetu ziwe za msingi tu endapo mtoto anataka kusoma sekondari lazima aende Mogadishu
Pia kama alivyo fanya Magufuli baraza la mawaziri kua la watanganyika pekee anafuata nyayo za Said Barre.....
Baada ya hapo alituma majeshi mengi kwenye maeneo yetu kama vile unavyoona majeshi yanavyotumwa Zanzibar kuua kubaka na kupora Mali za watu masikini wasio na hatia
Baada ya hapo Mungu akasikia kilio chetu Yale majeshi yalikua yanatunyayasa na kutudhalilisha.... Viongozi wao wakaita kikao na kujiuliza Hivi sisisi kama jeshi tunaonea watu bure kwa faida ya nani?
Mwaka 1991 jeshi lile lile likiongozwa na Jenerali Farah Aidiid wakapindua serikali Dhalim ya Mogadishu na kutokana na laana ya damu zetu mpaka Leo hawajapata amani tulionayo Sisi
Hivi tunavyo zungumza kuna watu wa Mogadishu wanaishi kwenye makambi ya wakimbizi yaliopo Somaliland
Hilo ni somo kwa Tanganyika pia.... Tusipende kutumia jeshi kudhulumu watu maana hata wanajeshi nao ni Binadamu na wanahisia za huruma
Haya majeshi tunapeleka Zanzibar wakati wa uchaguzi sio wote wanafurahia kuua. Kubaka na kupora Mali za wapemba