Kenya kufungua Ubalozi katika jimbo linalotaka kujitenga na Somalia

Na wewe utakuwa vitani mstari wa mbele wa Escape, F1-F9 sio!? 🙂
 
Hao wanasiasa kutoka nchi ya Somalia wanafanya campaign hapa Nairobi. Wanapenda kuja Nairobi kufanya biashara na kustarehe. Nairobi ni muhimu kwao. Huyo PM wa Somalia Farmaajo anajua kuwa akifanya Kenya iwe adui basi atapata kura nyingi sana kushinda wapinzani wake ambao wote wapo Kenya sasa hivi. Wapinzani wake wanafanya campaign hapa Nairobi na mmoja wao ana campaign headquarters hapa Nairobi. Prime minister Farmaajo anataka kupaint Kenya as the bad guy ili aonekane kama kiongozi anayeweza kuprotect Somalia from other countries. Ni siasa tu
 
Sijasema hamstahili ila nyinyi mnaroho za korosho sana. Yule mama alipoenda AfDB tuu, zilianza chokochoko za kuondolewa Adesina, what a coincidence?
USA ndio wanaotaka kumuondoa Adesina. Tatizo lenu ni kuwa mnaongozwa na chuki hadi mnasingizia Kenya mambo ambayo hayapo. USA kuanzia zamani hawakumpenda Adesina na wamejaribu juu chini kumuondoa hata Kabla ya huyo Mkenya kuchaguliwa.
 
Sasa we unaona ni sahihi kampeni za Kenya zikafanywe Kampala!? U okay in your head!?
 
Sisi tulikua na nchi yetu na Somalia ilikua nchi tofauti wakati tunapata Uhuru....
Lakini mwaka 1962 tuliamua kuungana muungano ukawa wa ujanja ujanja na wenye kero nyingi afadhali hata ya Zanzibar na Tanganyika kero si nyingi sana
1989 said barre akatunga sheria kandamizi kwa wana Somaliland ikiwemo kupigamarufuku mtu kujenga nyumba nzuri YA GHOROFA kule Hargeisa GHOROFA zote zijengwe Mogadishu tu
Shule zetu ziwe za msingi tu endapo mtoto anataka kusoma sekondari lazima aende Mogadishu
Pia kama alivyo fanya Magufuli baraza la mawaziri kua la watanganyika pekee anafuata nyayo za Said Barre.....
Baada ya hapo alituma majeshi mengi kwenye maeneo yetu kama vile unavyoona majeshi yanavyotumwa Zanzibar kuua kubaka na kupora Mali za watu masikini wasio na hatia
Baada ya hapo Mungu akasikia kilio chetu Yale majeshi yalikua yanatunyayasa na kutudhalilisha.... Viongozi wao wakaita kikao na kujiuliza Hivi sisisi kama jeshi tunaonea watu bure kwa faida ya nani?
Mwaka 1991 jeshi lile lile likiongozwa na Jenerali Farah Aidiid wakapindua serikali Dhalim ya Mogadishu na kutokana na laana ya damu zetu mpaka Leo hawajapata amani tulionayo Sisi
Hivi tunavyo zungumza kuna watu wa Mogadishu wanaishi kwenye makambi ya wakimbizi yaliopo Somaliland
Hilo ni somo kwa Tanganyika pia.... Tusipende kutumia jeshi kudhulumu watu maana hata wanajeshi nao ni Binadamu na wanahisia za huruma
Haya majeshi tunapeleka Zanzibar wakati wa uchaguzi sio wote wanafurahia kuua. Kubaka na kupora Mali za wapemba
 
Sijasema kwamba ni vizuri au ni vibaya. I am just stating facts.
Na mimi nasema its wrong... Maswala ya nchi yasimamiwe na wananchi wakiwa huko huko kwao. Mr. Prime minister is simply paint an obvious bad picture...

Sovereign State should deal with it's issues and decide for itself. Unasikia Coast wanataka kujitenga na Kenya..then usikie Tanzania wanafungua ubalozi mdogo huko as a Kenyan unaichukuliaje Tanzania!?

Doing something wrong for a long time ..doesn't miraculously make it right.. and Kenya MUST Stop.
 
Faarmajo keep on blowing hot air.He just left for turkey via JKIA.
 
Kaka umekwisha kukaa na Wapemba wakakuthibitishia wanaporwa!? Hapa kariakoo wamejaa tele sijawahi sikia hata mmoja akisema haya.. au hawa wa bara.huku hawana ndugu wala koo Zanzibari!?

Kujitenga kutokana na manyanyaso ni swala moja.. lakini kujitenga hakuondoi umuhimu wa kuwepo kwenye umoja. Umoja huo huo ndio Somaliland inaulilia kutoka kwa international community..

Kwann kama kujitenga kunaleta faida Somaliland isikae tu kimya without ties na wengine wote!? Tunategemeana.. na shida kubwa huwa ni madaraka.. na kukipenda Umimi..

Clearly Tanzania imekupokea na inakuheshimu kama mtanzania na huenda siku moja tutakupa nafasi ya kutuongoza kama Akina Rage na Bashe.. shida ninayoiona hauna mapenzi na nchi hii umo kama haumo.. na kama jamii yenu yote ndivyo ilivyo we are doomed.

Na badala ya kuIdentify na kuishi kama Mtanzania unaishi kama Msomali aliye uhamishoni.. Tofauti hufanyiwa kazi akwa uvumilivu na kuchukuliana ndivyo tunaendelea kukua na kukomaa kwenye muungano..

Haimaanishi shida zote zinakwisha siku moja.. Once a quiter always a Quiter.
 
Sorry mkuu may be I was a little bit harsh but that is a reality even if it is very hard to swallow
Mimi ni Proudly Tanzanian but also ninayo haki ya kutahadharusha nchi yangu isijekua kama Somalia
Mkuu wapemba wa kariakoo ni tofauti na wapemba waliopo Wete au Chake Chake hususan wakati wa uchaguzi na ndio maana nyakati hizo tunashuhudia mamia kwa mamia yao wanakuja Bara mpaka uchaguzi upite
Mambo ya uonevu na udhalilishaji wa jamii fulani katika nchi yanamadhara sana na reaction yake hua ni mbaya sana mfano mzuri ni kule Sudan jinsi Albashir alivyokua anawanyanyasa watu wa kusini
Gaddafi alivyo kua anafanya uonevu kule Banghazi
Na Hivi karibu Ethiopia Watigry wanavuna walichopanda kwa kuwanyanyasa waoromo na Wa Eritrean mpaka wakajitenga
Kuhusu wapemba kweli hatuwarendei wema inafikia tunawatumia mpaka vifaru na ndege za kivita kwao
Narudia tena kama tutaendelea kuwaonea kwa sababu ya nguvu zetu ipo siku tutajuta na kusaga meno
That's me to you
Nobody knew Ethiopian Tigris would be in trouble like the way they are now
Fimbo ya mungu haikosi shabaha.
Wenzetu wananyolewa nasi tutie maji?
 
Mi naona hatua hii ni kama ku escalate the situation.

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
Keyboard warriors....
Somalia ni mziki mwingine . Alshabaab imewatoa kamasi hapo mlipo.
 
Ni kinyume cha sheria za kimataifa. Kuonesha uko upande fulani wa pande mahasimu ktk nchi fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…