Kenya kuwa na Marais 2, Muungano wa Upinzani NASA watishia kumuapisha Raila Odinga kama Rais

NASA wamechanganyikiwa. Raila ataapishwa kama Rais kwa kura zipi? Na mamlaka ipi kisheria? Ana vyombo vya dola? Na katiba ipi itamruhusu?

Amepoteza dira mkuu
Nguvu ya umma ni kubwa kuliko dola unayosema....na popote pale duniani hakuna dola iliyowahi shinda nguvu ya umma.so msiwe mnaandika kwa jazba tu bila kushirikisha ubongo...
 
Nguvu ya umma ni kubwa kuliko dola unayosema....na popote pale duniani hakuna dola iliyowahi shinda nguvu ya umma.so msiwe mnaandika kwa jazba tu bila kushirikisha ubongo...
Kwa akili yako nguvu ya umma ndo itamsimika Odinga pale Ikulu siyo? Acha porojo jibu ataapishwa kama Rais kwa kura zipi? Na mamlaka ipi ya kisheria?
 
Wasiishie hapo waende mbele zaidi baada ya kumuapisha wagawane nchi mwingine kaskazini mwingine kusini Taifa kubwa Afrika mashariki libaki moja tu
 
hapo ndipo tunaona kuna haja ya Uhuru kutumia nguvu yake ya dola kama Magufuri anavyofanya,Ukiropoka uchechezi ndani,
Akuwaweka ndani kila anayefanya uchochezi muda huu ataituliza nchi.
 
Hata mwenyekiti Mao tse tung aliwahi kusema [emoji117] VITA NI MUENDELEZO WA SIASA ILI KUTATUA YALE MATATIZO YALIYO SHINDIKANA KISIASA YAPATE WEPESI [emoji106]
Wakenya wakifa/ wakipiga vita Uhuru kenyata amekua /atakua ni mpumbavu aliye vuka mipaka kwa kushidwa kusimamia swala la AMANI kwa kuwa yy ndo amiri jeshi Mkuu
 
Hizi ni siasa au visasi!

Cha ajabu wanaoumizwa na matokeo ya siasa za aina hii ni watu walewale wanasema wanataka kuwakwanyua kwenye matatizo.

Kuna mda mtu unashindwa kujua hawa wanasiasa wetu wanawazaga nini kichwani mwao.
 
Nguvu ya umma ni kubwa kuliko dola unayosema....na popote pale duniani hakuna dola iliyowahi shinda nguvu ya umma.so msiwe mnaandika kwa jazba tu bila kushirikisha ubongo...
Hiyo nguvu ya umm ipo NASA tu au pia Jubilee? Kama NASA wakifanya hivyo na Jubilee wakiamua hivyo ambao inasadikiwa kuwa wengi kama wale wa NASA unafikiri nini kitatokea?
Matumizi ya nguvu ya umma ni pale wananchi kwa asilimia kubwa wanapoungana kupinga jambo au uongozi dhalimu, sasa hebu fikiria idadi ya NASA na Jubilee ndio utajua hakuna nguvu yoyote ya umma zaidi ya mapigano baina yao na sio serikali tena.
 
Bila shaka atakuwa amekuelewa. Maana ameongea kama NASA ndo Kenya yote kwa asilimia 100%
 
Ama huyu mzee laila anatoa mpya aapishwe kwa kutumia katiba ipi. Atakuwa rais wa wajaruo Labda.
 
Mkuu from tarehe nane nafatilia uchaguzi WA Kenya tangia ule uchaguzi WA kwanza....msisikilize zile taarifa za sekunde mbili za ITV na TBC mkadhan mnainfo ya kujitosheleza...
Nampenda Uhuru sana awe rais kwa miaka mitano tena, ila kwa upumbafu anaoufanya kwa mtu wenye akili nzuri huwezi sapoti.mkuu techolojia ni kubwa mno ,watu walio jitokeza kwa uchaguzi WA marudio ni kati ya asilimia 22~33 ya watu million 19 waliojiandikisha kupiga kura.kwa hiki wanachokifanya ni ujinga WA kiwango cha lami kuudanganya ulimwengu kuwa Uhuru kapata kura almost milion Tisa sasa.yaani hii imemvua Nguo kuonesha ni jinsi gani kule kwenye server wanavyo ichezea.
Mkuu kwa logic ndogo tu ,hata Uhuru angepata kura laki moja ni halali yake na angeapishwa kwasababu watu hawalazimishwi kupiga kura ,sasa hizi manipulations anafanya kwa faida ya nani na ili iweje????
Watu kwenye vituo vya kupiga kura unaona kabisa hawapo ,halafu eti mtu anakwambia mifumo ilikuwa fasta sana watu walikuwa wakija wanavote fasta kwa sekunde chache na kuondoka, ndiyo maana kulikuwa hakuna foleni na watu watu vituoni. Kweli Leo ndiyo mifumo imekuwa fastaa????
KWA SISI WAPENDA HAKI ,HATA KAMA UNAONA RAFIKI YAKO ANAKOSEA HUWEZI KUSAPOTI UJINGA ANAOFANYA ETI KISA UNAMPENDA UKAFUMBIA MACHO UJINGA ANAOFANYA ,MWAMBIE UKWELI. LET'S CALL A SPADE , SPADE...NOT A SPOON.
 
Ama huyu mzee laila anatoa mpya aapishwe kwa kutumia katiba ipi. Atakuwa rais wa wajaruo Labda.
Nia yake ni kugawa Taifa la Kenya kuwa pande mbili na amesema wazi kuwa wataanza uasi.

Kususia mambo muhimu kwenye Serikali, watasusia bidhaa na huduma kutoka kwa kampuni zinazounga mkono utawala na wataendelea kushinikiza uchaguzi utafanyika katika siku 90.
 
Haya yote suluhisho sio NASA kumuapisha RAO, kuna tofauti kubwa sana kati ya kupiga kura na kumpenda mtu, kujitokeza kwa watu wachache bado sio kilelezo tosha kuwa Wakenya wote wapo tayari kumpinga Uhuru na serikali yake kwa umoja wao kama nchi moja.
Hapa hatuzungumzii kupendwa kwa Uhuru au Raila, ila tunazungumzia madhara ya NASA kutaka kumuapisha RAO, sasa unaweza ukaona RAO ana watu wengi kuliko Uhuru lakini unajiuliza wale wa Jubilee je hawapo? Jibu ni kwamba unawaona wafuasi wa NASA wakiwa mtaani kwa wingi kwasababu hayo ndio maazimio yao, yaani kuandamana. Jubilee wapo kimya kwasababu wameambiwa watulie na mipango yao haikuwa kuingia mtaani, sasa hebu fikiria Jubilee nao wawahamasishe wafuasi wao kupambana na NASA huko mtaani.
Na hili sijui la kuchezea server za IEBC bado sio kipimo kizur cha kujihakikishia kuwa RAO alishinda ndio maana hukumu ya kesi ya uchaguzi ili base sana kwenye formalities na sio numbers.
Nafikiri mabaya ya Uhuru yaondolewe kwa njia za kikatiba kama walivyofanya mwanzo ila hili la kutaka kumuapisha sijui nani, huu ni uhaini wa kiwango kikubwa na wataujutia wanaotaka kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…