Sio wanasheria na majaji tu, kila mtu ana la kujifunza toka Kenya kuhusiana na mambo ya haki. Ikumbukwe mafanikio ya leo yamelipiwa gharama ya damu baada ya ujanja ujanja kama unaofanyika kwetu kutokea mwaka 2007. Wananchi hawakukubali ujanja ujanja wa watawala, wakaingia mtaani. Sasa sio lazima nasi tulipie damu, lakini tukatae kuporwa haki zetu.
Ni takribani mwaka umepita toka mwenye nchi apige marufuku mikutano ya hadhara ya siasa-uamuzi ambao ni kinyume na katiba aliyoapa kuilinda, lakini kila mtu yuko kimya na ni kama watu wote tumeridhia uvunjwaji wa sheria na katiba zetu. Tumemuachia Tundu Lissu ndo aseme na alale jela, tena hatuendi hata mahakamani kumpa moyo. Tunamuona ana kimbelembele, lakin wakati huohuo tunashangilia ya Kenya bila kujua kuwa mafanikio yao yamelipiwa na watu wote kwa kupaza sauti zao penye uonevu na wakati mwingine kupoteza maisha.
Suluhisho: Wananchi wote, wenye elimu na wasio na elimu, watawala na wapinzani, wa mjini na vijijini, wapenda siasa na wasiopenda siasa, sote tuna la kujifunza toka kwa jirani zetu.