KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

Japo nilikua na msupport kenyata lakini maamuzi ya mahakama yame nifurahisha sana kwa sababu zifuatazo.

1. Mahakama ya kenya ipo huru na haipo mfukoni mwa mtawala fulani kama hapa Tanzania

2. Kama mapungufu yalisababishwa na negligence ya tume ya uchaguzi basi itarekebisha na pia kama kenyata alishinda kihalali basi atashinda tena.

3. Nimefurahishwa na speed ambayo high court wameendesha na kutoa maamuzi ya kesi, sio kama kwetu kesi za uchaguzi zinachikua mpaka zaidi ya miaka miwili. .

4. Mahakama za Tanzania zina kitu cha kujifunza hapa, pia ni lazima hata kwetu tuwe na uwezo wa kupinga matokeo ya uraisi mahakamani.

Kenya nyie ni baba wa demokrasia Africa mashariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"The greatness of any nation is held with three pillars,the fidelity of a constitution, rule of law and above all the fear of God"

Chief Justice Maraga
 
Chadema tunaangalia lakini tunasema hiyo mahakama kuu ni lazima ipitie upya na kujiridhisha sisi tulikuwepo kwenye kampeni na tulijiridhisha demokrasia ilifuata na baba wa demokrasia!
 
Wakuu habari za hivi punde kutoka BBC World news zinasema Mahakama kuu nchini Kenya imefutilia Mbali matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Uhuru Kenyata.
#stay_up-to-date

Chanzo BBC

From Sir Korojani
 
Niliandika pia kuwa , Uhuru Kenyatta is a thief.

Nikamalizia kuwa, Once a thief always a thief.

Kenyatta aone aibu sasa .

Viva, Raila a.k.a. RAO.
 
Rest in Peace Msando. Sasa na tume itabadilishwa ama ? Sasa team ya UHURU itakubali au itakata rufaa ? Let us keep folllowing. Im proud to live seeing this.
Kuna rufaa juuya Supreme Court?
 
mkuu mngeweka na sababu za kufutwa maana kila mtu anaweka update kama hii tu juu juu tu
 
Sio wanasheria na majaji tu, kila mtu ana la kujifunza toka Kenya kuhusiana na mambo ya haki. Ikumbukwe mafanikio ya leo yamelipiwa gharama ya damu baada ya ujanja ujanja kama unaofanyika kwetu kutokea mwaka 2007. Wananchi hawakukubali ujanja ujanja wa watawala, wakaingia mtaani. Sasa sio lazima nasi tulipie damu, lakini tukatae kuporwa haki zetu.

Ni takribani mwaka umepita toka mwenye nchi apige marufuku mikutano ya hadhara ya siasa-uamuzi ambao ni kinyume na katiba aliyoapa kuilinda, lakini kila mtu yuko kimya na ni kama watu wote tumeridhia uvunjwaji wa sheria na katiba zetu. Tumemuachia Tundu Lissu ndo aseme na alale jela, tena hatuendi hata mahakamani kumpa moyo. Tunamuona ana kimbelembele, lakin wakati huohuo tunashangilia ya Kenya bila kujua kuwa mafanikio yao yamelipiwa na watu wote kwa kupaza sauti zao penye uonevu na wakati mwingine kupoteza maisha.

Suluhisho: Wananchi wote, wenye elimu na wasio na elimu, watawala na wapinzani, wa mjini na vijijini, wapenda siasa na wasiopenda siasa, sote tuna la kujifunza toka kwa jirani zetu.
 
Tume za uchaguzi Afrika ni somo ipo siku wafanyakazi wake watafungwa jela wakivuruga uchaguzi kwa nia ya kuwapa mgombea au chama fulani ushindi kwa kuendesha uchaguzi usio na haki wala huru na kutoa matokeo ya utata yenye upendeleo.

Muhimili wa Mahakama unatakiwa uwe huru na kuonekana huru mbele ya macho ya wananchi ili haki ipatikane pale muhimili wa (dola) yaani serikali unapojaribu kuburuza raia na Bunge. Hili ni muhimu kama mdau sooth alivyotuasa Tundu Lissu asiachwe mkiwa ktk kupigania haki, sheria na katiba zisikiukwe.
 
Niliandika pia kuwa , Uhuru Kenyatta is a thief.

Nikamalizia kuwa, Once a thief always a thief.

Kenyatta aone aibu sasa .

Viva, Raila a.k.a. RAO.
Umeisikia lakini ruling ya mahakama? haijasema Kenyatta ame cheat mahali bali tume ndio imefanya makosa ya kiutendaji kinyume na katiba ya Kenya. Muw mnafuatilia kwa umakini sio kuchukua mambo juujuu kama yale ya makinikia
 
Back
Top Bottom