Wanajukwaa kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, mahakama ya juu nchini Kenya imeamuru time ya uchaguzi IEBC kuandaa uchaguzi mwingine ndani ya siku 60.
Rest in Peace Msando. Sasa na tume itabadilishwa ama ? Sasa team ya UHURU itakubali au itakata rufaa ? Let us keep folllowing. Im proud to live seeing this.
Mahakama imeufuta uchaguzi wa kenya kwa kua ulikua na dosari kubwa muda mfupi uliopita naamini kuna la kujifunza kwa hawa jirani zetu haswa serkali na mahakama zetu!!
Mpaka pale wanasiasa wa Tanzania na wananchi kwa ujumla watakapofahamu kuwa democrasia ndio yaleta maendeleo katika nchi hapo ndipo tutakuwa tumejitawala,lakini haya yanayoendelea hivi sasa Tanzania ni sawa na utawala wa kikoloni wenye sura ya mwafrika..
Wakenya wako mbele kiuchumi,kimawazo na sasa wametuonyesha mpaka kwa demokrasia wametupita,hii nchi tuiangalie kwa mbali,hii nchi ni ya kupigiwa mfano Afrika Mashariki.