KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

Wakuu habari za hivi punde kutoka BBC World news zinasema Mahakama kuu nchini Kenya imefutilia Mbali matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Uhuru Kenyata.
#stay_up-to-date

Chanzo BBC

From Sir Korojani
Ndo unaamka?
 
Sawa mkuu si maana kuviomba tena kusimamia uchaguzi kama vimesifia ila mahakama imekataa uchaguzi
 
Habarini!
Kwanza kabisa napenda niwapongeze wakenya kwa hatua kubwa ambayo system yao ya democrasia upande wa kuchagua rais wamefikia!
Kitendo cha mahakama ya juu kutengua matokea ya urais ambayo yalisema Uhuru Kenyatta ndo mshindi kwa kigezo kuwa hayakuwa halali ni cha kupongezwa.

Kura za wakenya zilidukuliwa ktk computer.
Kitendo hili kimewahi tokea pia Tanzania ingawa huku kwetu matokeo yalitenguliwa na ZEC badala ya mahakama kwa sababu hizi hizi za udukuzi. Hivyo Jecha na team yake wanastahili pongezi nyingi sana kwa kutengua ule ushindi batili wa Seif ktk uchaguzi wa rais Zanzibar 2015.

Tanzania nasi tulikataa huu upuuzi wa kudukua matokeo ya uchaguzi kama majirani zetu walivyofanya! Demokrasia ni kuwaacha wananchi wake wachague viongozi wao wanaowataka wao sio kutumia komputer kwa njia za panya.
Heko to Tanzania na Kenya.
 
Hapo supreme court ingetoa pendekezo kwa tume huru ya uchaguzi ya kenya kuvunjwa na kuundwa mpya kabla ya fresh elections.
kumbuka ni tume huru.... labda kama kuna sheria itakayo fanya hivyo kupelekea kuvunjwa kwake
 
mkuu mngeweka na sababu za kufutwa maana kila mtu anaweka update kama hii tu juu juu tu
Wametaja sababu za kuufuta kuwa haukuwa wa haki hivyo utarudiwa baada ya siku 60 toka leo. Kwa mara ya kwanza hili linatokea katika aridhi ya afrika ni dhahiri kuwa democrasia inaanza kukua katika Kenya na Afrika kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DIoVniaXgAA_Mkk.jpg
 
Wametaja sababu za kuufuta kuwa haukuwa wa haki hivyo utarudiwa baada ya siku 60 toka leo. Kwa mara ya kwanza hili linatokea katika aridhi ya afrika ni dhahiri kuwa democrasia inaanza kukua katika Kenya na Afrika kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wale Wazee wa Africa waliosema "Uchaguzi ulikua huru na haki kasoro matatizo machache" tuendelee kuwaamini!??
 
Kenya wanajitambua sana. Na ili kuhakikisha hakuna figisu, proceedings za kesi zilikuwa live bila chenga huku Advocates wa Kenyatta/IEBC wakijiumauma tu. Ni kazi sana kutetea wizi uliofanyika asubuhi huku aliyeibiwa yupo calm na ana almost evidence zote
 
Chris Msando (Director of ICT at IECB)
May your Great Soul Rest in Peace.

Kenyans will not leave your blood in vain/void.

Uhuru Kenyatta, why did you quench the life of Chris Msando the ICT expert at IECB!?

Msando's blood will not leave you safe Mr Uhuru Kenyatta wherever you will be.
 
tatizo sio katiba,tatizo ni majaji,plain and simple, jaji anapofanya kazi huko anahofia nikifukuzwa kazi wanangu watakula nini,jaji huyo hawezi kutenda haki, daima atapokea maagizo kutoka juu

Ndo maana nakwambia kuwa ttz ni katiba, maana hapo kuna suala la mchakato wa uteuzi, na kuhakikishiwa uhuru wa maamuzi yao. Sasa kama mteuliwa lazima awe mwanachama wa chama tawala unatarajia nini? Katiba ndo mzizi wa tatizo na siyo watu.
 
Back
Top Bottom