Kenya: Mke wa Sheikh Aboud Rogo, Haniya Said Saggar ahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani

Kenya: Mke wa Sheikh Aboud Rogo, Haniya Said Saggar ahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
HANIYA-SAID-SAGGAR.jpg

Haniya Said Saggar
Mke wa Marehemu Sheikh Aboud Rogo Mohamed amehukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani kwa kosa la kushindwa kuzuia uvamizi wa kituo cha Polisi cha Central kilichotokea mwaka 2016.

Akitoa uamuzi huo Diana Mochache amesema kuwa Mke wa Rogo alishindwa kupiga ripoti kwa Polisi kuhusiana na mpango wa washukiwa wa ugaidi kuvamia kituo hicho cha Polisi.

Aidha, Hakimu huyo amemuondolea mashtaka mengine ya kuwa Mwanachama wa kundi la ugaidi akisema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha madai hayo.

Haniya Said Saggar, alikamatwa na kutiwa mbaroni mwaka 2016, akiwa nyumbani kwake huko Kanamai, Kaunti ya Kilifi.

Kwenye uvamizi huo wasichana watatu walioshukiwa kuwa magaidi waliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa Polisi.

Chanzo: Radio Rahma /TaifaLeo

Kuhusu Aboud Rogo soma...
Tension in Mombasa as Al-Shabaab suspect Rogo killed
Ghasia zazuka Mombasa baada ya kuuawa kwa Sheikh Aboud Rogo
Jicho Pevu: Waliomua Aboud Rogo na wenziwe ni Usalama wa Serikali kenya
 
Ladies and gentlemen I introduce to you to the Religion of peace
 
Innalillah wainna ilayh rajiun tulitaraji hayo tokana na serikal ya kigaidi ya Kenya na muendelezo wa kupambana na kuua na kufunga waislamu

According to aljazeera ktk documentary ilorushwa December 2014 wakifanya mahojiano na kikos cha kupambana na uislamu a.k.a antiterror magaidi wa kikosi hiki huku wakiwa wamezibwa nyuso zao walikir kumuua sheikh aboud rogo kinyama kwa risasi 17 kwa kile walichodai kila wakimpeleka mahakaman anashinda. Baada ya hapo wamemgeukia mke wake mama yetu kipenzi. Tunasema hasbunallahu waneemal wakili na majarbio haya yanawakumba waumini

"Mnafikir mtaingia peponi burebure baada y kusema nyie n waumini yaliwakuta kabla yenu madhila ...dhiki na mabalaa hta wakasema nusra Ya Allah itakuja lini "

Wazidi kusubiri na sisi tunasubiri mlango waliokwsha ufungua umeshawashinda kuufunga.
 
Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu mwamamke mmoja kifungo cha miaka kumi kwa kosa la kupanga njama ya kufanya shambulizi la kigaidi.
_91207637_haniarogoabubakaryusuf.jpg

Hania Rogo na wakili wake Aboubakar Yusuf kortini 2016

Mahakama imempata na hatia Haniya Said Saggar ya kuratibu shambulio la bomu la petroli lililotekelezwa dhidi ya kituo cha polisi jijini Mombasa miaka miwili iliyopita. Haniya ni mjane wake Aboud Rogo, ambaye aliaminika kuandaa shughuli za kundi la wanamgambo wa Al Shabaab nchini Kenya.

Kwenye hukumu yake, hakimu alisema kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba Haniya aliwasiliana na mmoja wa wanawake watatu waliolitekeleza shambulio hilo.

Mwanamke huyo, Tasnim Yakub, alikuwa amesilimu kutoka Ukristo miezi mitatu kabla ya shambulio, ikiwa ndio muda pia ambao alipata kujuana na Haniya.

Mahakama imefahamishwa pia kwamba wawili hao waliendelea kuwasiliana hadi muda mfupi kabla ya shambulio hilo.

Inadhaniwa pia kwamba Tasnim aliwavutia wanawake wawili aliojiunga nao kukiteketeza moto kituo cha polisi na hata kujaribu kumdunga kisu askari. Wote watatu walipigwa risasi na kuuawa.

Ripoti ya ushahidi uliotokana na uchunguzi umebaini kwamba kipakatilishi cha Tasnim kilikuwa na fasihi zenye itikadi kali baadi ambazo zilichapishwa na kiongozi wa kidini mweye misimamo mikali Aboud Rogo - marehemu mumewe mshtakiwa.

Sheikh Rogo aliunga mkono wazi wazi kundi la Al Shabaab na pia alitetea mauaji ya wakristo.

Rogo mwenyewe aliuawa kwa kupigwa risasi mara kumi na sita na watu wasiojulikana mnamo mwaka 2012 , tukio ambalo lilizua maandamano na tafrani jijini Mombasa.

_100057526_6b04ab76-0015-4a46-a98a-c09340dd1e25.jpg

Aboud Rogo

Rogo aliaminika kuwa na uhusiano wa karibu na raia wa Uingereza Samantha Lethwaite, al Maarufu 'white widow', anayetuhumiwa kufadhili mauaji nchini Kenya, na ambaye angali anasakwa vikali na Polisi wa kimataifa, Interpol.
 
Innalillah wainna ilayh rajiun ........tulitaraji hayo tokana na serikal ya kigaidi ya Kenya na muendelezo wa kupambana na kuua na kufunga waislamu .....according to aljazeera ktk documentary ilorushwa December 2014 wakifanya mahojiano na kikos cha kupambana na uislamu a.k.a antiterror ...magaid wa kikosi hiki huku wakiwa wamezibwa nyuso zao walikir kumuua sheikh aboud rogo kinyama kwa risasi 17 kwa kile walichodai kila wakimpeleka mahakaman anashinda ...,......baada ya hapo wamemgeukia mke wake mama yetu kipenzi ........tunasema hasbunallahu waneemal wakil .....na majarbio haya yanawakumba waumini
...... .....

Huyu mama Allah ampe subra. Angewezaje kuzuia ilhali yeye hajui, ni dhulma tu anafanyiwa.
 
Huyu mama Allah ampe subra. Angewezaje kuzuia ilhali yeye hajui, ni dhulma tu anafanyiwa.
Wewe ndio unasema hajui, lakini mahakama imeona kuwa alikuwa anajua. Dini ya haki!
 
Mke wa Marehemu Sheikh Aboud Rogo Mohamed amehukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani kwa kosa la kushindwa kuzuia uvamizi wa kituo cha Polisi cha Central kilichotokea mwaka 2016.

Akitoa uamuzi huo Diana Mochache amesema kuwa Mke wa Rogo alishindwa kupiga ripoti kwa Polisi kuhusiana na mpango wa washukiwa wa ugaidi kuvamia kituo hicho cha Polisi.

Aidha, Hakimu huyo amemuondolea mashtaka mengine ya kuwa Mwanachama wa kundi la ugaidi akisema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha madai hayo.

Haniya Said Saggar, alikamatwa na kutiwa mbaroni mwaka 2016, akiwa nyumbani kwake huko Kanamai, Kaunti ya Kilifi.

Kwenye uvamizi huo wasichana watatu walioshukiwa kuwa magaidi waliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa Polisi.

Chanzo: Radio Rahma /TaifaLeo
Tatizo alikuwa Rogo na sio huyo mama lakini ndo hivyo tena naye amesha nasibishwa na Mumewe aliyejaza vijana wetu fikra chafu na potevu za Jihadi feki
 
Mahakama gan zpo chini ya nan sio serikal inayoua waislamu ...hii mahakama zenu n upumbavu na ushenz mtupu .......
Kila kitu kipo chini ya serikali, huwezi kukwepa haki ya mahakamani, labda uhamie nchi nyingine isiyoendeshwa na sheria
 
Huyu mama Allah ampe subra. Angewezaje kuzuia ilhali yeye hajui, ni dhulma tu anafanyiwa.
Umesahau mauaji ya wakrito yaliyo kuwa yakiungwa mkono waziwazi na mmewe au ndo mkuki kwa nguruwe
 
Umesahau mauaji ya wakrito yaliyo kuwa yakiungwa mkono waziwazi na mmewe au ndo mkuki kwa nguruwe
Halafu ulishawahi kunitukania mzazi wangu kwenye thread fulani, nakuona unawashwa sana na michango yangu hapa JF. Kuna kitu unakitafuta na utakipata soon!
 
Halafu ulishawahi kunitukania mzazi wangu kwenye thread fulani, nakuona unawashwa sana na michango yangu hapa JF. Kuna kitu unakitafuta na utakipata soon!
Sio ukweli huwa situkani kama ndo ivo am sorry na hata id yako kwangu ni mpya

Sent from my GT-I9082 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom