Kenya mtammiss sana Uhuru Kenyatta

Kenya mtammiss sana Uhuru Kenyatta

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058
Hakuna kitu mwanadamu anapenda kama kuwa huru, it's human nature, hata kama unapigania uchumi wake kiasi gani, hata kama unalinda rasilimali kiasi gani hata kama unampa chakula cha bure ila unammbanabana automatically lazima akuchukie.

Uhuru Kenyatta licha ya mapungufu yake mengine ni Kiongozi poa ambaye habanibani sana watu, tukilinganisha na huku kwetu unaweza kusema yupo kama Jakaya Kikwete. Kenya ndio nchi inayoenjoy uhuru zaidi katika nchi zote za afrika mashariki (mtazamo wangu), nikiifikiria Rwanda, nikiifikiria Uganda kule ndio hali mbaya zaidi.

Wakenya wanaenjoy sana hivi sasa, kinachonifanya niamini wakenya watammiss Uhuru Kenyatta ni hao wanaotajwa kuwa warithi wa Uhuru, watu kama kina Ruto wanaonekana kabisa ni Power Mongers ambao hawataweza kuvumilia memes, kukosolewa au mtizamo kinzani.

Wakenya wasipoangalia watarudi hatua nyuma sana wakati walishatoka enzi za kina moi na kibaki, hamna raha kama kupata kiongozi ambaye amezoea utawala na mamlaka, asiyejali mambo madogo madogo kama Uhuru.
 
Watam-miss kama walivyomiss social gathering...
 
Attachments

  • Kenya.mp4
    2.3 MB
Kuruhusu rushwa itawale ndiyo Uhuru unaousema?
 
Ukitaka kujua madhara ya uhuru ajiri houseboy pale kwako halafu mpe uhuru sana, mchekee chekee.

Kuwatawala watu kwa Demokrasia kunahitaji akili, lazima uwakumbushe kuwa mambo si rahisi rahisi tu kama wanavyotaka.

Namkubali sana JK ila pia moja ya kitu ninachokumbuka kwe utawala wake ni lile swali la hivi wewe unanijua mimi ni nani? Hapo ni mtu ana tuvimilioni bank amesimama barabarani anaongea namwanamke umemuuliza mbona unaziba njia? .
 
tutakumissy sn mzee kenyatta....tufungulie basii mazee dah!

1591120690646.jpg
 
Ndio maana wakenya tulipigania na tukapata katiba mpya. Ambayo ilibuni mihimili na taasisi iliyo huru na inayojisimamia kisheria. Kisha rais akapunguziwa madaraka na yakasambazwa kwa mihimili na taasisi tofauti za kiserikali. Ugatuzi nao ukampokonya rais nguzu za kuwashika wananchi mateka kimaendeleo na gatuzi zote 47 zikapata uhuru wa kujiamulia maendeleo wanayoyataka, kwa asilimia flani kwenye baadhi ya sekta za kiuchumi. Kesho yake mwingine akija akalie kiti hicho kisha aanze kufanya mambo ya ajabu ajabu hataweza kustahimili mapigo yatakayofata. Sio kupenda kwake rais UK, anayoyafanya ni yale ambayo katiba inamlazimisha ayafanye na anajua akienda kombo katiba mpya ilirahisisha njia ya kumg'atua kupitia 'impeachment'.
 
tutakumissy sn mzee kenyatta....tufungulie basii mazee dah!

View attachment 1469991
[emoji1][emoji1][emoji1] Curfew ilegezwe ndio uende wapi usiku jombaa, kwenye madanguro au? [emoji23] Wengine wetu tunataka siku ziongezwe, maanake familia zimefaidi sana siku zote hizo ambazo tumekuwa tukilazimika kufika nyumbani kabla ya saa moja usiku.
 
Ndio maana wakenya tulipigania na tukapata katiba mpya. Ambayo ilibuni mihimili na taasisi iliyo huru na inayojisimamia kisheria. Kisha rais akapunguziwa madaraka na yakasambazwa kwa mihimili na taasisi tofauti za kiserikali. Ugatuzi nao ukampokonya rais nguzu za kuwashika wananchi mateka kimaendeleo na gatuzi zote 47 zikapata uhuru wa kujiamulia maendeleo wanayoyataka, kwa asilimia flani kwenye baadhi ya sekta za kiuchumi. Kesho yake mwingine akija akalie kiti hicho kisha aanze kufanya mambo ya ajabu ajabu hataweza kustahimili mapigo yatakayofata. Sio kupenda kwake rais UK, anayoyafanya ni yale ambayo katiba inamlazimisha ayafanye na anajua akienda kombo katiba mpya ilirahisisha njia ya kumg'atua kupitia 'impeachment'.

Shida sio katiba pekee mkuu , maana wapo viongozi wanaofanya mambo kinyume na katiba na hakuna wa kuwafanya kitu , mnaweza kuwa na katiba bora kabisa ila mkapata mtawala asiyeifuata katiba yeye pamoja na washirika wenzake walioshika mamlaka ya bunge, mhakama na kadhalika
 
Ukitaka kujua madhara ya uhuru ajiri houseboy pale kwako halafu mpe uhuru sana, mchekee chekee.

Kuwatawala watu kwa Demokrasia kunahitaji akili, lazima uwakumbushe kuwa mambo si rahisi rahisi tu kama wanavyotaka.

Namkubali sana JK ila pia moja ya kitu ninachokumbuka kwe utawala wake ni lile swali la hivi wewe unanijua mimi ni nani? Hapo ni mtu ana tuvimilioni bank amesimama barabarani anaongea namwanamke umemuuliza mbona unaziba njia? .
hayo mambo ya unanijua mi nani hayajaisha bado yapo tuu, tena kibabe zaidi
 
Ndio maana wakenya tulipigania na tukapata katiba mpya. Ambayo ilibuni mihimili na taasisi iliyo huru na inayojisimamia kisheria. Kisha rais akapunguziwa madaraka na yakasambazwa kwa mihimili na taasisi tofauti za kiserikali. Ugatuzi nao ukampokonya rais nguzu za kuwashika wananchi mateka kimaendeleo na gatuzi zote 47 zikapata uhuru wa kujiamulia maendeleo wanayoyataka, kwa asilimia flani kwenye baadhi ya sekta za kiuchumi. Kesho yake mwingine akija akalie kiti hicho kisha aanze kufanya mambo ya ajabu ajabu hataweza kustahimili mapigo yatakayofata. Sio kupenda kwake rais UK, anayoyafanya ni yale ambayo katiba inamlazimisha ayafanye na anajua akienda kombo katiba mpya ilirahisisha njia ya kumg'atua kupitia 'impeachment'.
Nimeipenda sana hii,jambo la kuigwa.
 
Uhuru gani mnaozungumzia kwamba upi Kenya kwingine haupo?au ndo tunalishana matango
 
Katiba katiba katiba!!!! Ndio kitu kinachotulinda, huyu rais Uhuru ni binadamu kama wengine na isingekua kwa katiba tungemkoma, katiba mpya na bora zaidi ya zote Afrika ndio ngao yetu, hata kesho aje mwingine, naye atanyooshwa na katiba.
Tanzania kama mlivyo wala huwa siwezi nikalaumu matamko ya marais wenu, tatizo lipo kwenye katiba mbovu, hata mimi ningekua rais wenu na unipe katiba kama ya Tanzania mbona mtanikoma ubishi, tena nitakua naajiri na kutumbua siku hiyo hiyo, nikikuajiri halafu hauimbi mapambio ya kuniisifia ipasavyo, nakutupia nje nje.
Mapesa nayatumia bila bajeti wala nini, nikitaka kununua mindege natoa amri tu....hamna cha bunge wala kajamba yeyote wa kunihoji, na ole wako ujaribu kunisema......iiiiiiiiiiuuuuuiiiii
 
Katiba ya Kenya inaelezeaje uchotwaji wa pesa unapofanya na Uhuru na kikundi chake.
 
Shida sio katiba pekee mkuu , maana wapo viongozi wanaofanya mambo kinyume na katiba na hakuna wa kuwafanya kitu , mnaweza kuwa na katiba bora kabisa ila mkapata mtawala asiyeifuata katiba yeye pamoja na washirika wenzake walioshika mamlaka ya bunge, mhakama na kadhalika
Katiba inachangia pakubwa, kwasababu kiongozi kama rais akipewa madaraka ambayo hayana mipaka ya kueleweka lazima atavimba kichwa. Kumbuka kwamba wakenya walipigania katiba mpya ili wabadilishe yote yaliyowafanya wapitie mengi kwenye miaka 24 ya udikteta wa Moi. Wakenya tayari wameonja matunda yake na wakaona manufaa mengi ya kuishi kwa uhuru uliopo sasa hivi. Sidhani kuna mtu yeyote yule ambaye anaweza akaja kuitawala Kenya kwa ubabe bila kuzingatia hayo na akafanikiwa kuwa madarakani baada ya hata mwaka mmoja tu. Kumbuka utamaduni wa kubebwa na wapambe ambao hawajakidhi vigezo vya kuwa viongozi ulitupiliwa kando. Maanake sasa hivi uteuzi wa rais hautoshi bila usaili wa bunge zote mbili.
 
Kibaki alikuwa poa tu hata ukimtukana atakuita mavi ya kuku lakini hataagiza polisi wakupige. Kibaki hakuwa dictator hata kidogo. Tazama hapa

[emoji1][emoji1][emoji1] Curfew ilegezwe ndio uende wapi usiku jombaa, kwenye madanguro au? [emoji23] Wengine wetu tunataka siku ziongezwe, maanake familia zimefaidi sana siku zote hizo ambazo tumekuwa tukilazimika kufika nyumbani kabla ya saa moja usiku.
Hapana Jombaa. Tutazaana sana. Wacha curfew ifunguliwe angalau tudunde mitaani
 
Back
Top Bottom