Kenya mtoto auzwa kwa Tsh. 65,000

Kenya mtoto auzwa kwa Tsh. 65,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Binti wa miaka 17, wa kidato cha pili mkazi wa Butere Kaunti ya Kakamega, amelazimika kumuuza mwanaye mara baada ya kujifungua, baada ya kufukuzwa na baba yake mlezi kwa kuwa na ujauzito huo.

Taarifa zinasema binti huyo alifukuzwa kwa kuwa alipewa mimba na nduguye wa karibu hivyo mtoto ambaye angezaliwa alionekana kuwa kama ‘laana’ kwa jamii yao na linakiuka tamaduni na desturi zao.

Mama wa binti huyo alilazimika kutafuta mtu wa kumuuzia, na alilipwa kabla ya binti huyo hajajifungua. Mama wa binti huyo anasema walilazimika kumuuza mtoto kwa kuwa wasingeweza kumlea mtoto huyo na ndio sababu wakaamua kumuuza.

Polisi eneo hilo wanachunguza tukio hilo

Citizen TV
 
Sasa hapo unakuwa ushalipia na V.A.T au ukitoa hiyo Sitini na tano elfu ulipe na V.A.T?
 
Back
Top Bottom