joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Vikosi vya Kenya na Somalia jana vilikabiliana katika ufyatulianaji risasi wa dakika kadhaa katika mpaka wa pamoja wa mataifa hayo mawili baada ya upande wa Kenya kufyatua risasi kuwazuia waandamanaji wa Somalia kutokaribia.
Haya ni kwa mujibu wa maafisa wa serikali katika eneo hilo pamoja na walioshuhudia. Tukio hilo lilifanyika katika mpaka kati ya mji wa Somalia wa Bulo Hawo na Mandera kwa upande wa Kenya karibu na eneo ambalo mpaka huo unashikana na Ethiopia katika eneo la Kaskazini.
Shirika la habari la Ufaransa AFP limeripoti kwamba hakukuwa na waathiriwa wowote kutokana na makabiliano hayo.Afisa mmoja wa polisi katika eneo hilo la Bulo Hawo Mohamed Abdirahman ameliambia shirika hilo la AFP kwamba waandamanaji hao wanaamini kuwa raia watatu ''waliotekwa nyara siku moja kabla'' katika mji wa mpakani wa El Wak, Kusini mwa Bulo Hawo waliuawa na polisi wa kukabiliana na ugaidi nchini Kenya.
=======
MY TAKE: Kule mpakani mwa Uganda chokochoko haziishi, mpakani na Ethiopia nako sio shwari, risasi zinarindima mara kwa mara, Somalia nako kuameanza, wakenya somo la kuishi kwa amani na majirani wenu darasani mlipata "F".