Kenya na Somalia zaanza kuchapatana risasi mpakani

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Vikosi vya Kenya na Somalia jana vilikabiliana katika ufyatulianaji risasi wa dakika kadhaa katika mpaka wa pamoja wa mataifa hayo mawili baada ya upande wa Kenya kufyatua risasi kuwazuia waandamanaji wa Somalia kutokaribia.

Haya ni kwa mujibu wa maafisa wa serikali katika eneo hilo pamoja na walioshuhudia. Tukio hilo lilifanyika katika mpaka kati ya mji wa Somalia wa Bulo Hawo na Mandera kwa upande wa Kenya karibu na eneo ambalo mpaka huo unashikana na Ethiopia katika eneo la Kaskazini.

Shirika la habari la Ufaransa AFP limeripoti kwamba hakukuwa na waathiriwa wowote kutokana na makabiliano hayo.Afisa mmoja wa polisi katika eneo hilo la Bulo Hawo Mohamed Abdirahman ameliambia shirika hilo la AFP kwamba waandamanaji hao wanaamini kuwa raia watatu ''waliotekwa nyara siku moja kabla'' katika mji wa mpakani wa El Wak, Kusini mwa Bulo Hawo waliuawa na polisi wa kukabiliana na ugaidi nchini Kenya.

=======

MY TAKE: Kule mpakani mwa Uganda chokochoko haziishi, mpakani na Ethiopia nako sio shwari, risasi zinarindima mara kwa mara, Somalia nako kuameanza, wakenya somo la kuishi kwa amani na majirani wenu darasani mlipata "F".
 
Wakenya wanapenda vurugu sana wasomali wapole
 
Somalia na Ethiopia walilimana vita kali sana miaka kadhaa iliyopita. Kenya ndio nchi pekee Afrika Mashariki ambayo haijawahi kupigana na nchi nyingine tangu tupate uhuru
Vita gani iliyotokea Kati ya Ethiopia na Somalia?, Kenya ndio nchi pekee ambayo inagombana na majirani zake wote ukanda huu.
 
Bwana shemeji, Kwa kifupi hamjui hata uwezo wenu kijeshi maana hamjawahi kuingia vitani. Ndio maana Alshababu wanawaonea kumbe.
 
Kwa hivyo sisi kutopenda vita imekuwa ni unyonge tena shemeji? Nyinyi si mlipigana na Uganda?
 
Vita gani iliyotokea Kati ya Ethiopia na Somalia?, Kenya ndio nchi pekee ambayo inagombana na majirani zake wote ukanda huu.
Nabakia kwa wazo langu la awali kuwa Kenya ndio nchi pekee Africa Mashariki ambayo haijawahi kupigana na serikali ya nchi nyingine. Kwa hivyo sisi hatupendi ugomvi.
Wacha nijibu swali lako la vita la Ethiopia na Somalia. Liko hata kwenye Wikipedia na kwenye websites nyingi kwenye mtandao. Natumai utasoma hii link ili ujifunze jambo. Leo ndio utajuwa kuwa Kenya hatupendi ugomvi.

Ogaden War - Wikipedia
 
Huwezo wenyewe hamna sasa mtapigana na nani.
Kama wagambo tuu wa Alishabab wanawasumbua
Hio haibadilishi ukweli kwamba Kenya sisi hatupendi ugomvi na ndio maana hatujawahi kupigana na nchi nyingine. Tukija kwenye suala la nguvu la jeshi la Kenya, basi kwenye rankings za jeshi hapa Afrika Mashariki, Ethiopia tu ndio imeshinda Kenya kwenye rankings. Kenya imeishinda Tanzania kwenye rankings. Sisi ni wapole lakini msituchokoze. Usione simba kanyeshewa ukadhani paka.
 
Nyie endeleeni kuongelea takwimu tuu mkitegemea mabwana zenu wa hapo Mombasa (USA navy)
Kifupi itoshe kusema nyie ni taifa korofi ila ndo dhaifu kuliko mataifa yote kwa EA labda mtawasumbua burundi na Rwanda
 
Wewe najua huelewi mambo ya rankings.
 
Nabakia kwa wazo langu la awali kuwa Kenya ndio nchi pekee Africa Mashariki ambayo haijawahi kupigana na serikali ya nchi nyingine. Kwa hivyo sisi hatupendi ugomvi.
Wacha nijibu swali lako la vita la Ethiopia na Somalia. Liko hata kwenye Wikipedia na kwenye websites nyingi kwenye mtandao. Natumai utasoma hii link ili ujifunze jambo. Leo ndio utajuwa kuwa Kenya hatupendi ugomvi.

Ogaden War - Wikipedia
KwahiyoKDF huko Somalia hawapo vitani?
 
Back
Top Bottom