Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Jamani eeehTanzania kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje, January Makamba, ameahidi kutatua na kusuluhisha mzozo wa Kenya na Tanzania Airways.
Kupitia chapisho kwenye X, January alifichua kuwa alizungumza na waziri mkuu wa Kenya, Musalia Mudavadi, na kuahidi kusuluhisha suala hilo ndani ya siku 3 kulingana na makubaliano yaliyopo.
Pia Soma:
- Tanzania yazuia ndege za shirika la ndege la Kenya kutua nchini. Ni baada ya Kenya kutoruhusu ndege za Tanzania kubeba mizigo Kenya
View attachment 2872849
Nchi inakosa viongozi wenye msimamo. Wao ndiyo waje kutuomba maana kila siku wanachokoza wao.
Kuna ujinga mwingi sana kwenye haya mambo na Tanzania tufocus kwenye tija. Wanalitaka soko letu wakati lao wamelifungia.
Tuongeze wigo wa kupata washirika wa kibiashara zaidi kuliko jirani peleche