Mkuu naomba niambie ni wakenya wa aina gani ambao wana uwezo wa kuwekeza Tanzania? Nina uhakika humaanishi mabantu na waswahili kama sisi bali ni wakenya wenye asili nyingine ndiyo wanao weza kuwekeza Tanzania. Mbantu wa Kenya na mswahili wa Kenya ana hela gani ya kuwekeza Tanzania? Tusidanganyane hapa.
Mkitaka kujua watu gani wanamaisha mazuri kati ya hizo nchi mbili angalieni idadi ya watu waliokimbia nchi yao na kwenda kutafuta maisha kwenye nchi nyingine.
Kuna idadi ya wakenya wengi sana kwenye nchi zifuatazo kuliko watanzani; Amerika, England, Ujerumani, Uholanzi, Dubai, Qatar, Saud Arabia na South Africa, ni kwanini hasa wakenya wengi wameikimbia nchi yao na kuishi ng'ambo?
Ni kitu ambacho kinaeleweka kuwa wakenya wachache sana wanamiliki ardhi Kenya, sehemu kubwa ya ardhi inamilikiwa na wazungu, zamani tuliwaita setllers; waingereza, wajerumani na waholanzi. Viwanda vingi nchini Kenya ni vya wazungu na wahindi na wafanya biashara wakubwa nchini Kenya ni wazungu na wahindi pia.
Wakenya wengi utawakuta kwenye mambo ya siasa, utumishi serikalini, kwenye serikali kuu na local government, majaji, mahakamani, polisi, jeshini na walimu na wafanya kazi kwenye makampuni na NGOs za wazungu na kwenye mabank.