Kabla hujaingia Kenya forum utakuta intro pale saaafi kabisa "serious discussions on Kenyan politics and latest news from Kenya" hapo kama kichwa yako ipo makini kuchanganua lugha ya kimombo utaelewa kabisa hii forum ni kwa ajili ya wazawa
Nyie mwanzo mlikuwa mna mendeamendea humu kwa kusoma habari zetu tukaona isiwe taabu acha tuongeze forum special kwa ajili ya habari za EAC na nyie ndio mkapata nguvu hata ya kujadili mada zetu humu
Kama isingekuwa desturi yetu kuongea na kucheka na kila mtu kiwema(kiroho safi) hata kama nyangau inakudhihaki, humu mngeshakimbia kitambo sana...Si umeona sasa tumewakaribisa mkajisikia mpo nyumbani na kujisahau kabisa hadi kufikia kusema forum ni kwa ajili yenu.
Sent using
Jamii Forums mobile app